• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

KIWANJA CHA NDEGE SONGEA KUBEBA NDEGE SITA KWA WAKATI MMOJA,SASA NDEGE KUTUA SAA 24

Posted on: October 21st, 2020

SERIKALI  ya awamu ya tano imetenga  kiasi cha shilingi bilioni 37 kukarabati uwanja wa ndege wa Songea ambao utawezesha kwa wakati mmoja kubeba ndege sita aina ya bombardier.

Akitoa taarifa ya ukarabati wa kiwanja hicho kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme,Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Songea Jordan Mchami,amesema kazi ya  ujenzi wa barabara ya kutua ndege yenye urefu wa  meta 1740 na upana wa meta 30 imeshakamilika.

Amesema ujenzi wa maegesho ya ndege yenye ukubwa wa meta 139 kwa 126 ipo kwenye hatua za mwisho kukamilika na inatarajia kukamilika katikati ya mwezi Novemba mwaka huu hivyo kumudu kuegesha ndege kubwa zaidi ya  sita.

Meneja huyo wa Kiwanja cha ndege Songea amesema pia yamejengwa maegesho maalum ya kuegesha ndege za dharura yenye ukubwa wa meta 70 kwa 40  na kwamba katika kiwanja hicho zimejengwa taa za kisasa za kuongozea ndege wakati wa usiku  hivyo kuwezesha ndege kutua saa 24 yaani usiku na mchana.

“Ndege aina ya bombardier sasa zitaanza kutua wakati wowote katika kiwanja cha ndege cha Songea,tunatarajia ndege ya kwanza itatua kabla ya mwisho wa mwezi huu Oktoba’’,alisema Mchami.

Amesema jengo jipya la abiria lenye uwezo wa kuchukua abiria 150 kwa wakati mmoja limejengwa na kukamilika katika uwanja wa ndege wa Songea  hali ambayo inaweza kumudu abiria wa ndege mbili za bombardier kwa wakati mmoja.

Amesema gharama za nauli katika ndege hizo za serikali zitakuwa chini ukilinganisha na ndege ndogo za watu binfasi ambazo nauli yake ni kati ya shilingi 500,000 hadi 600,000  hali ambayo wananchi wengi hawawezi kumudu.

Amesema ujio wa ndege ya bombardier utakuwa ni ukombozi kwa wananchi wa Mkoa wa Ruvuma kwa sababu wananchi watalipa shilingi 400,000 toka Songea hadi Dar es salaam, kwenda na kurudi.

Akizungumza mara baada ya kukagua ukarabati wa uwanja huo,Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme ameipongeza Kampuni ya CHICCO ambayo inakarabati kiwanja hicho,ambacho ukarabati wake unatarajia kukamilika kwa asilimia 100 Desemba mwaka huu.

Mndeme amesema kiwanja cha ndege  wa Songea ni rasilimali adimu inayoweza kusaidia kukuza uchumi wa mji wa Songea na Mkoa mzima wa Ruvuma hasa kukuza sekta ya utalii,baada ya kuanzishwa mpango mkakati wa kukuza utalii katika mkoa wa Ruvuma.

Kiwanja cha ndege wa Songea ni miongoni mwa viwanja  bora vya ndege Tanzania ambacho kilijengwa kati ya mwaka 1974 hadi 1980 na kiliwekewa lami hivyo kuwa na uwezo wa kutua ndege majira yote masika na kiangazi.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma

Oktoba 21,2020

 

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • Jela maisha Kwa Ubakaji

    May 27, 2025
  • Msigwa aipongeza Tamisemi kikao maafisa habari

    May 24, 2025
  • SERIKALI ilivyodhamiria kuboresha Barabara na madaraja

    May 23, 2025
  • Mwenge wa Uhuru wapitia miradi 76 mkoa wa Ruvuma

    May 17, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.