• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

DKT.SAMIA AMWAGA TENA MAMILIONI YA MIRADI NYASA

Posted on: July 10th, 2025

-Aridhia milioni 748.1 kujenga miundombinu ya elimu msingi na awali 

-Milioni 314 kujenga shule mpya ya msingi Limbo

Na Byarugaba Innocent, Nyasa DC

Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Julai 1, 2025 imepokea fedha za Miradi zaidi ya shilingi za kitanzania Milioni 748.1 kutoka serikali kuu kupitia mradi wa kuboresha upatikanaji wa fursa  sawa katika ujifunzaji bora wa elimu awali na msingi Tanzania (BOOST)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameridhia fedha hiyo kiasi cha shilingi 748,158,910 zitumike kwenye ujenzi wa miundombinu ya shule za msingi na awali Wilaya ya Nyasa ili kuimarisha zaidi ujifunzaji kwa kuweka mazingira wezeshi

Kaimu mkuu wa divisheni ya Mipango na Uratibu Aliko Anthony Mwabukusi ameeleza kuwa fedha hiyo itatumika kukarabati majengo chakavu, kujenga shule mpya, Kujenga nyumba  ya Mwalimu, kujenga madarasa  na kujenga Matundu ya Vyoo kwenye maeneo husika

Aidha, Mwabukusi amezitaja kata zilizopokea fedha kuwa ni Kilosa kwa ajili ya ukarabati wa shule ya Msingi Kilosa shilingi 153,458,910 pamoja na ujenzi wa shule mpya ya Msingi Limbo ambapo kiasi cha shilingi 314,000,000 kimetolewa

Kata nyingine ni Chimate iliyopokea shilingi 154,200,000 kujenga vyumba 2 vya Madarasa, Matundu 6 ya vyoo pamoja na nyumba ya mtumishi ya familia mbili.

Mwabukusi ameongeza kuwa Kata ya Kingerikiti  imepokea shilingi 59,200,000 kujenga vyumba 2 vya madarasa na Matundu 6 ya vyoo shule ya msingi Ukuli. Aidha, Kata ya Lipingo imepokea shilingi 67,300,000 kujenga Madarasa 2 na Matundu 6 shule ya Msingi Lipingo.

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Khalid A. Khalif amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuiheshimisha Nyasa kwa kutoa fedha hiyo kuimarisha zaidi miundombinu ya Elimu na kuahidi kuisimamia kwa weledi mkubwa, ikamilike kwa wakati kwa viwango bora vinavyolingana na thamani ya fedha  iliyotumika  ili ianze  kutoa huduma bila kuathiri mipango na malengo ya serikali

Khalid ametoa rai kwa wkandarasi, Wazabuni na wananchi kufanyakazi kwa ushirikiano ili kukamilisha miradi kwa manufaa ya jamii yetu kwani uwekezaji mkubwa unaofanywa na serikali yetu katika sekta ya elimu tunapaswa kuunga mkono kwa vitendo

Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa ina jumla ya shule za Msingi 117 za Serikali na kukamilika kwa shule ya Msingi Limbo kutaongeza idadi na kufikia 117.

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • UTEKELEZAJI KAMPENI YA CHANJO YA MIFUGO YAANZA NYASA

    July 12, 2025
  • MAKUNDI SOGOZI YA WHATSAAP YAPASWA KUJADILI MAENDELEO

    July 12, 2025
  • DC MAGIRI AZINDUA RASMI BODI YA MAJI WILAYA YA NYASA

    July 12, 2025
  • DKT.SAMIA AMWAGA TENA MAMILIONI YA MIRADI NYASA

    July 10, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.