• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

Livestock and Fisheries


Mr.Madondola-Head of livestock and Fisheries

Idara ya Mifugo na Uvuvi katika Halmashauri inajishughulisha na usimamizi wa wanyama wote wafugwao wakiwemo jamii za ndege na samaki.

Idadi ya Watumishi

Idara hii ina jumla ya watumishi 19 kati yao 5 wapo makao makuu ngazi ya Wilaya akiwemo Afisa uvuvi 1. Maafisa Mifugo 13 na Afisa uvuvi msaidizi 1 wapo ngazi ya Kata na hakuna watumishi ngazi ya Vijiji. Aidha kata 6 hazina maafisa Mifugo.

Idadi ya Mifugo

Aidha, Kufikia Juni, 2016 Wilaya ilikuwa na Mifugo ya aina mbalimbali ikiwemo Ng’ombe 22, 283 kati ya hao ng’ombe wa kienyeji ni 21,984 na wa maziwa 299, Nguruwe 41,653 Mbuzi 39,585 kati ya hawa Mbuzi wa asili ni 39,560 na Mbuzi wa maziwa 25, Kondoo 4,911 na, kuku 160,771 kati ya hao Kuku wa asili wa kienyeji ni 160,324na kuku wa kisasa ni 447 bata 3,986 punda 9 mbwa 6,257 Paka 1,367 Kanga 92, Sungura 1,601 na njiwa 329.

Eneo la Malisho

Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa kutokana na idadi ya mifugo iliyopo inahitaji kuwa na jumla ya eneo la malisho lipatalo hekta 16,089.625, kwa sasa inakadiriwa kuwa na jumla ya Ha. 748 zinazofaa kwa malisho lakini eneo na linalotumika ni Hekta. 733 ambapo hekta 15 ni eneo lenye mbung’o na halitumiki kwa malisho.

Kutokana uwiano huo inamaanisha kwamba yapo maeneo yanayotumika kwa ufugaji ambayo si rasmi kwa shughuli hiyo. Aidha kuhusu mpango wa matumizi bora ya ardhi katika Wilaya ni vijiji 6 tu vimetenga maeneo ya malisho (grazing blocks) ambayo hayaja rasmishwa na hakuna ranchi ndogo ndogo zilizoanzishwa hadi sasa.

Vitengo vya Idara ya Mifugo na Uvuvi

Idara ina vitengo vikuu 2

  • Kitengo cha Mifugo

1. Kitengo cha Tiba na Kinga ya magonjwa ya Mifugo.

2. Kitengo cha Uendelezaji wa nyanda za malisho ya Mifugo.

3. Kitengo cha Uzalishaji Uboreshaji wa Mifugo na mazao yake.

4.  Kitengo cha ushauri na uelimishaji.

  • Kitengo cha Uvuvi.

Doria, uokoaji, uhamasishaji na ukusanyaji wa maduhuli ya serikali

SHUGHULI ZA VITENGO IDARA YA MIFUGO NA UVUVI. 

  • Kitengo cha Mifugo
  1. Kitengo cha Tiba na Kinga ya magonjwa ya Mifugo

Majukumu

  1. Kusimamia tiba ya ya magonjwa ya Mifugo.
  2. Kusimamia kinga ya magonjwa ya mifugo kama vile chanjo dhidi ya Ugonjwa wa Homa wa Kichaa cha Mbwa, Mdondo (New Castle Disease (NCD)) Ugonjwa wa ndui ya kuku n.k
  3. Kusimamia afya ya mifugo inayotoka na kuingia Wilayani.
  4. Kusimamia ukaguzi wa usafi na usalama wa nyama na maeneo ambayo nyama inazalishwa.
  5. Kusimamia ukusanyaji wa maduhuli ya serikali yanayotokana na mifugo
  6. Kuandaa ripoti mbalimbali za magonjwa na kuziwasilisha kwenye Kituo cha Utafiti wa Magonjwa ya Mifugo Iringa.
  1. Kitengo cha Uendelezaji wa nyanda za malisho ya Mifugo 

Majukumu

  • Kutoa ushauri wa kitaalamu juu ya matumizi na uboreshaji wa nyanda za malisho
  • Kutoa ushauri kwa Serikali ya Vijiji kuainisha maeneo yanayofaa kwa ufugaji wakati wa kuandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi vijijini.
  • Kusimamia na kuendeleza miundombinu ya mifugo.
  1. Kitengo cha Uzalishaji na Uboreshaji wa Mifugo na mazao yake.

Majukumu

  • Kusimamia uboreshaji wa mifugo ya asili ili kuleta tija kwa mfugaji.Hasa kuku wa asili, mpaka sasa idara imeshasambaza jumla ya kuku bora wa kienyeji aina ya sasso 2,550 wanaokua haraka ukilinganisha na kuku wetu wa asili.
  • Kusimamia sheria ya utambuzi, usajili na ufwatiliaji wa Mifugo na wafugaji ambapo zoezi la uhamasishaji jamii linaendelea.
  • Kusimamia sheria ya ubora na usalama wa maziwa katika wilaya ili kuhakikisha mlaji anapata maziwa safi na salama.
  • Kusimamia utekelezaji wa Sheria na Sera mbalimbali zinazotolewa na Serikali katika sekta za Mifugo na Uvuvi.
  1. Kitengo cha ushauri na uelimishaji
  • Kuandaa mafunzo yote yanayohusina na mifugo na wafugaji katika Halmashauri.
  • Kutoa elimu na ushauri wa kitaalam kwa wafugaji ikiwemo kuhimiza mbinu bora za ufugaji kwa lengo la kuhifadhi mazingira.
  • Kutoa taarifa za matokeo ya tafiti mbalimbali za mifugo na hatua za kuchukua ili kuwa na uzalishaji wenye tija katika sekta ya mifugo na uvuvi.

Kitengo cha Uvuvi.

Majukumu:

  • Kutoa elimu ya utunzaji wa fukwe za ziwa kwa kuanzisha vikundi shirikishi vya kulinda fukwe yaani “Beach management Units” (BMU).
  • Kutoa elimu ya Uvuvi endelevu katika Ziwa huku tukiweka mkazo kulinda na kutunza mazalia ya samaki ili kuwa na uvuvi endelevu.
  • Kufanya doria za mara kwa mara ili kupunguza tatizo la uvuvi haramu katika Ziwa Nyasa.
  • Kufanya shughuli za Uokoaji wakati wa dhoruba katika ziwa.
  • Kutoa elimu ya usalama wa usafiri ndani ya maji huku tukisisitiza matumizi ya vifaa vya uokoaji kama “LIFE JACKETS” Na Maboya.
  • Kuhamasisha wananchi kuchimba mabwawa na kufuga samaki.
  • Kutoa elimu na ushauri wa kitaalamu juu ya uzalishaji samaki kwenye mabwawa.


Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • Karibu Mwenge wa Uhuru Wilayani Nyasa

    May 11, 2025
  • Mwenyekiti wa Tume huru ya Uchaguzi Tanzania akagua vituo vya kujiandikisha Nyasa.

    May 04, 2025
  • Dc Nyasa awataka madiwani na watendaji kubuni vyanzo vipya vya mapato

    April 30, 2025
  • DC Nyasa azindua Kituo kipya cha Mafuta

    April 26, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.