• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

MAKUNDI SOGOZI YA WHATSAAP YAPASWA KUJADILI MAENDELEO

Posted on: July 12th, 2025
  • JUBILEI YA MIAKA 50 SHULE YA MSINGI NGINGAMA YALETA NEEMA
  • ‘WAJUBILANT’ WATOA FADHILA KWA KUKARABATI MADARASA CHAKAVU

Na Byarugaba Innocent, Nyasa DC

Watanzania wameaswa kuyatumia makundi ya WhatSaap kujadili mambo ya maendeleo kuanzia ngazi ya kaya, Jamii na Taifa tofauti na uhalisia uliopo hivi sasa ambapo makundi mengi yamekuwa yakitumia muda mwingi kujadili mambo yasiyokuwa na tija pengine kuwa sehemu ya kuchochea tabia na mienendo isiyofaa katika jamii.

Rai hiyo imetolewa na Aidani Ndomba mwenyekiti wa kamati  iliyokarabati jengo moja la shule ya Msingi Ngingama lenye vyumba viwili vya madarasa na ofisi ya walimu kupitia  kundi la WhatSaap lililotumika kuwaunganisha wanafunzi waliosoma shule hiyo miaka 50 iliyopita  tangu kuanzishwa kwake mwaka 1975-2025

“…kupitia kundi la WhatSaap tuliona kuna haja ya kuleta fadhila, tukahamasishana kuchangia kidogo kidogo kila mtu alichoweza na kupata shilingi milioni 7.5 iliyotumika kununua vifaa na wengine wakachangia ufundi, tumefanikiwa. Suala la elimu si jukumu la serikali pekee, tunaona serikali imekuwa ikifanya pakubwa nasi kama jamii inatupasa kuongeza nguvu kwa kuunga mkono juhudi za Serikali yetu”… amesema Ndomba

Jubilei ya miaka 50 (1975-20250 shule ya msingi Ngingama ikiitikiwa na Elimu ni ufunguo wa Maisha ni kauli mbiu yenye lengo la  kuwakumbusha wananchi wa  Vijiji vya Lukali, Kiogo na Ngingama kuendelea kuikumbatia elimu na kamwe kutokubali kuwaozesha mabinti ama kuwapeleka machungani vijana wa kiume kwani kupitia elimu tunapata wataalam wanaolitumikia taifa lao.

Makamu mkuu wa chuo kikuu cha Jordani kilichopo Mkoani Morogoro Profesa Betram Mapunda  ni miongoni mwa wazawa walioshiriki Jubilei hiyo ambapo ametoa wito kwa wazazi, walezi na jamii nzima kuendelea kuhamasika na kuwekeza kwenye elimu kwani jamii ama taifa lisilokuwa na wataalam halina uhai kimaendeleo

Thadei Chale Mwalimu Mkuu na Christoms Mahundi kiranja mkuu wa shule ya msingi Ngingama wameiomba serikali kuwaongezea walimu, kujenga jengo la kujisitiri watoto wa kike pamoja na kuwaongezea vifaa vya kujifunza na kujifunzia hususan wa Ki-TEHAMA kwani dunia ya leo inajifunza kwa vitendo zaidi.

Kwa upande wake kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Hamis Mkele aliyekuwa mgeni rasmi amewapongeza sana wananchi wa Ngingama, Lukali na Kiogo waliosoma shule hiyo hasa wanaoishi nje ya Wilaya ya Nyasa, Mkoa wa Ruvuma kwa ushirikiano, Upendo na utashi wa kukumbuka walikotoka na kuamua kurudi nyumbani kutoa fadhila kwenye kumbukizi ya Jubilei ya dhahabu ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwake.

Aidha, amesema serikali inatambua na kuthamini mchango wao na kwamba katika bajeti ya 2026/2027 watawajengea miundombinu waliyoomba sanjali na kuongeza walimu kwa mujibu  wa ikama.

Sherehe hii ya maadhimisho ya miaka 50 ya Jubilei ya dhahabu iliadhimishwa kwa wananchi wote kula, kunywa huku ikipambwa kwa ngoma maarufu za asili kama  Muganda, Kioda na Mahalamisi.

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • UTEKELEZAJI KAMPENI YA CHANJO YA MIFUGO YAANZA NYASA

    July 12, 2025
  • MAKUNDI SOGOZI YA WHATSAAP YAPASWA KUJADILI MAENDELEO

    July 12, 2025
  • DC MAGIRI AZINDUA RASMI BODI YA MAJI WILAYA YA NYASA

    July 12, 2025
  • DKT.SAMIA AMWAGA TENA MAMILIONI YA MIRADI NYASA

    July 10, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.