• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

Balozi wa Tanzania nchini Malawi atembelea Wilaya ya Nyasa

Posted on: December 6th, 2025

*BALOZI WA TANZANIA NCHINI MALAWI AFANYA ZIARA RASMI YA KIKAZI WILAYANI NYASA*


 _Na Byarugaba Innocent, Nyasa_


Balozi wa Tanzania nchini Malawi Mhe.Agnes Richard Kayola amefanya ziara rasmi ya Kikazi Wilayani Nyasa kwa lengo la kuona fursa za uwekezaji,raslimali zilizopo na kukiri kuwa iwapo zitatumiwa vyema zinaweza kuchechemua uchumi kuanzia ngazi ya Kaya.

Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Mhe.Peres Boniphace Magiri akiwasilisha taarifa kwa Mhe.Balozi Kayola amesema uchumi wa Nyasa kwa 75% unatokana na Kilimo cha  mazao ya chakula kama Mahindi,maharage,Karanga na Mazao ya biashara ikiwemo Kahawa na Korosho kwa uchache


Mhe.Magiri ameongeza kuwa sehemu ya uchumi inatokana na Uvuvi kutokana na uwepo wa Ziwa Nyasa,uchimbaji wa madini,Utalii wa kisiwa cha Lundo huku akibainisha fursa mpya za uchumi kama usafiri na usafirishaji,usindikaji wa Mazao ya ziwani, uwekezaji wa hoteli kutokana na uwepo wa fukwe kando ya ziwa Nyasa,usambazaji na uuzaji wa bidhaa za viwandani,usindikaji wa Matunda na usindikaji wa Mazao ya Kilimo.


Akiongea na wafanyabiashara Mhe.Balozi Kayola amewataka kuwa wazalendo kwa kuzitangaza na kutumia fursa zilizopo nchini, kuangalia hali ya ulinzi na Usalama ili kufanyabiashara zao bila Vikwazo na kulinda mitaji yao,kuzitumia fursa za Mazao kwa kufuata Sheria na taratibu zilizopo na fursa za usafiri na usafirishaji


Aidha,Mhe.Balozi Kayola ametoa rai kwa Watanzania kuendelea kuchapa kazi kuiunga mkono Serikali iliyopo Madarakani kwa vitendo kwa uthubutu wa Kujenga Bandari kubwa inayogharimu kiasi cha fedha zaidi ya  Shilingi bilioni 80 kwani inakwenda kuchagiza Sekta ya  usafiri na usafirishaji wa bidhaa mbalimbali kwa mataifa ya Malawi, Msumbiji, Zambia na Tanzania na kuimarisha zaidi maeneo ya Kimkakati ikiwemo Viwanda, Bandari,bidhaa za Mazao na bidhaa za usindikaji.


Wakiongea kwa niaba ya wafanyabiashara Vincent Muli na Gabliel Mathius wamemwomba Mhe.Balozi kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Malawi kuboresha Mazingira ya Kibiashara ili kuwarahisishia wafanyabiashara ikiwemo Kujenga Soko la Kimataifa Wilayani Nyasa ili nchi jirani za Msumbiji,Malawi na Zambia kuja kuchukua na kuleta bidhaa.


Afisa Uhamiaji Wilaya ya Nyasa Albert Masao ametoa wito kwa wafanyabiashara kufanyabiashara halali ikiwemo kuingia kwenye mipaka ya mataifa mengine kisheria wakiwa na hati za Kimataifa za Kusafiria badala ya kutumia hati za dharula.


Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Nyasa Khalid A.Khalif amewataka wafanyabiashara kushirikiana na mamlaka zinazowahudumia ikiwemo Ofisi za biashara za Wilaya na Mamlaka ya Mapato ili kupata Suluhu ya Mambo yao.


Mhe.Balozi Kayola akiwa  Wilayani Nyasa ametembelea fukwe zilizopo kandakando ya ziwa Nyasa,Kisiwa cha Lundo,eneo la uwekezaji la Bio Camp,Ujenzi wa Bandari kubwa inayogharimu fedha za kitanzania zaidi ya Bilioni 80,Ofisi za Uhamiaji pamoja na kuongea na wafanyabiashara.

Announcements

  • Tangazo la nafasi za kazi Halmashauri ya wilaya ya Nyasa December 01, 2025
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • TANGAZO la nafasi ya kazi February 03, 2023
  • View All

Latest News

  • Balozi wa Tanzania nchini Malawi atembelea Wilaya ya Nyasa

    December 06, 2025
  • Maonesho ya Nane Nane Kanda za Nyanda za juu kusini , Mguu sawa Kuanza leo

    August 01, 2025
  • UTEKELEZAJI KAMPENI YA CHANJO YA MIFUGO YAANZA NYASA

    July 12, 2025
  • MAKUNDI SOGOZI YA WHATSAAP YAPASWA KUJADILI MAENDELEO

    July 12, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.