• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

DC MAGIRI AZINDUA RASMI BODI YA MAJI WILAYA YA NYASA

Posted on: July 12th, 2025
  • ASISITIZA UTENDAJI WENYE TIJA

Na Byarugaba Innocent, Nyasa DC

Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Mhe. Peres Magiri amezindua rasmi bodi ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Wilaya ya Nyasa -MBAUWASA sambamba na kugawa vitendea kazi  ikiwemo Sheria ya Maji Na.5 ya Mwaka 2019 na kanuni zake huku akisistiza  weledi na uzalendo kwa watumishi wa bodi hiyo ili kufanikisha adhima ya kuwahudumia Wananchi.

Mhe. Magiri ametoa rai hiyo kwa wajumbe wa bodi ya MBAUWASA waliochaguliwa kujipanga vizuri na kufanyakazi kwa bidii, ubunifu, weledi na ushirikiano ili kuifanya mamlaka  kujiendesha  kwani bila kufanya hivyo itafutwa na yeye kama kiongozi wa Wilaya tena mteule  wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  hayupo tayari kuona ikifutwa mikononi mwake

Mkurugenzi mtendaji wa MBAUWASA Mhandisi John Guseseka amesema kuwa mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Mbamba-Bay ilianzishwa rasmi mwaka 2018 ikiwa daraja C na kutangazwa  kwenye gazeti la Serikali la tarehe 2 Machi, 2018 No.67 huku eneo la huduma  likibainishwa kuwa ni Kata tatu za Mbamba-Bay, Kilosa na Mtipwili  na gharama za uendeshaji ikiwa ni makusanyo yake ya maduhuli ya maji na uwekezaji mkubwa wa miundombinu kutoka Serikali Kuu.

Mhandisi Guseseka ameongeza kuwa tayari Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Hamidu Aweso ameteu bodi ya MBAUWASA tangu tarehe 12 Februari, 2025 itakayohudumu kwa kipindi cha  miaka mitatu mpaka tarehe 11 Februari, 2028 kwa kuhakikisha hudma ya Maji  inapatikana muda wote na inakuwa endelevu.

Wajumbe walioteuliwa  ni Stanley Vumu ambaye ni Mwenyekiti, Asifiwe Salum anayewakilisha kundi la watumia Maji, Dkt. John Papalika anayewakilisha kundi la wafanyabiashara, Veronica Simba mwakilishi kundi la wanawake na Leslie Kadambe anayewakilisha kundi la watumia maji wakubwa  huku Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa na Mkurugenzi Mtendaji wa MBAUWASA wakiingia kwa nyadhida zao.

Katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Nyasa Acheni Mwinshehe ametoa rai kwa wenyeviti wa vijiji  na vitongoji kusimamia utaratibu na kutoa elimu kwa wananchi ya ulipiaji huduma ya Maji ili kuiwezesha Mamlaka Kujiendesha huku akiwaasa kamwe kutokuwa sehemu ya kukwamisha juhudi za Serikali za kufikisha huduma za Maji kwa Wananchi.

Mwenyekiti wa MBAUWASA Stanley Vumu amejinasibu mbele ya Mkuu wa Wilaya kuwa wajumbe walioteuliwa wapo kikazi zaidi na kuahidi kuwa watafanyakazi ya kuisimamia  mamlaka kwa weledi, Ushirikiano kwa kuzingatia Sheria, Kanuni, taratibu na miongozo iliyopo na kwamba ameyapokea maelekezo yote ikiwemo kuongeza na kutanua mtandao wa Maji kutoka kata tatu zilizoanishwa sasa na kupandisha upatikanaji wa maji kutoka asilimia 68 mpaka 85

Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Mhe. Peres Magiri ametumia fursa hiyo kuwakumbusha Wananchi kushiriki kikamilifu kwenye uchaguzi Mkuu, 2025 unaotarajia kufanyika Mwezi Oktoba huku akiwataka Wananchi wa Wilaya ya Nyasa kumchagua kwa kumpa kura za kishindo Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa utendaji wake bora ikiwemo kuleta miradi mingi ya maendeleo Wilaya ya Nyasa

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • UTEKELEZAJI KAMPENI YA CHANJO YA MIFUGO YAANZA NYASA

    July 12, 2025
  • MAKUNDI SOGOZI YA WHATSAAP YAPASWA KUJADILI MAENDELEO

    July 12, 2025
  • DC MAGIRI AZINDUA RASMI BODI YA MAJI WILAYA YA NYASA

    July 12, 2025
  • DKT.SAMIA AMWAGA TENA MAMILIONI YA MIRADI NYASA

    July 10, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.