• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

ZAIDI YA ASILIMI 60 YA MAGONJWA YA BINADAMU YANATOKANA NA WANYAMA

Posted on: October 5th, 2020

MTAALAM kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dr. Justine Assenga  amesema  zaidi ya asilimia 60 ya magonjwa anayougua binadamu yanasababishwa na wanyama.

Dr.Assenga ameyasema hayo kwenye mafunzo ya utayari wa kukabili magonjwa ambukizi kwa timu za dharura za kukabili magonjwa kutoka mikoa hatarishi ya Ruvuma na Mtwara ambayo yanafanyika kwa siku tano kwenye ukumbi wa Hoteli ya Tiffany mjini Mtwara.

Kwa mujibu wa Mtaalam huyo kati ya asilimia hizo,asilimia 75 ya magonjwa hayo yanaambukizwa na wanyamapori na asilimia 20 kutoka wanyama wanaofugwa.

Ameyataja magonjwa sita hatarishi  ya milipuko kuwa ni kimeta,kichaa mbwa,bonde la ufa,mafua makali ya ndege,kutupa mimba na ebola na amewataja baadhi ya wanyama ambao ni hatarishi katika kusambaza magonjwa hayo kuwa ni popo na panya.

Akifungua mafunzo hayo,Mkurugenzi wa  Maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Kanali  Jimmy Matamwe ameitaja dhana ya afya moja kuwa inawakutanisha wataalam na wadau kutoka sekta mbalimbali hususani sekta ya afya,mazingira,maliasili,mifugo na wanahabari kutekeleza agenda ya usalama wa afya duniani.

“Dhana ya afya moja inatumika zaidi kwa kuzingatia kuwa vimelea vingi vinavyosababisha magonjwa ya binadamu,asilimia 60 vinatoka kwa wanyamapori na mifugo,maambukizi yanatokea pale binadamu anapoingilia masikani ya wanyama hao bila tahadhari”,alisema.

Hata hivyo amesema kwa nchi za Afrika hali ni hatarishi zaidi kwa kuzingatia kuwa bara hili hususani sehemu ambazo zinakaribia mapori makubwa ya wanyama ikiwemo Kongo Basin ni kitovu cha magonjwa ya milipuko kama vile ebola na homa ya bonde la ufa na hivi sasa ni virusi vya corona.

Kanali Matamwe amesema imedhirika kuwa ushirikiano wa watalaam katika mifumo ya afya moja  hivi sasa ni agenda ya dunia nzima kwa sababu inapunguza gharama katika kushughulikia tishio la magonjwa yanayotokana na vimelea vyenye uwezo wa kutoka kwa wanyama kwenda binadamu.

Amesema Tanzania sio kisiwa hivyo kutokana na ongezeko la watu duniani,mabadiliko ya tabianchi na utandawazi umekuwa na mwingiliano mkubwa baina ya watu na wanyama katika mazingira yao na kusababisha kueneo kwa vimelea kwa haraka zaidi na kusababisha magonjwa kwa binadamu,wanyama na mimea.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani (FAO) Niwael Mtui ameyataja malengo ya kutoa mafunzo kwa timu ya afya moja ni  kuwajengea uwezo washiriki ili waweze kuzuia na kukabiliana na magonjwa ya mlipuko kabla hayajatokea.

Mafunzo ya utayari wa kukabili magonjwa ambukizi ya mlipuko kwa timu za dharura yanafadhiliwa na FAO kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu ambayo yalianza kutolewa mwaka 2018.

Imeandikwa na Netho Sichali, Mtwara.

Oktoba 5,2020

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • UTEKELEZAJI KAMPENI YA CHANJO YA MIFUGO YAANZA NYASA

    July 12, 2025
  • MAKUNDI SOGOZI YA WHATSAAP YAPASWA KUJADILI MAENDELEO

    July 12, 2025
  • DC MAGIRI AZINDUA RASMI BODI YA MAJI WILAYA YA NYASA

    July 12, 2025
  • DKT.SAMIA AMWAGA TENA MAMILIONI YA MIRADI NYASA

    July 10, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.