• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

yaliyojiri Ziara ya Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma Wilayani Nyasa

Posted on: November 6th, 2024

Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma, Mary Makondo, akiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, amefanya ziara ya kikazi wilayani Nyasa. Lengo la ziara ni kutembelea miradi ya maendeleo na kutoa miongozo ya kuimarisha ulinzi na usalama, na kuhamasisha, uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

 Akiwa Hospitali ya Wilaya ya Nyasa,  ametembelea jengo la wagonjwa wa nje, ambalo limejengwa kwa lengo la kutoa huduma bora kwa wananchi  jengo la dharura (emergency), ambalo linahusisha huduma za haraka kwa wagonjwa wanaohitaji matibabu ya Dharula.

Pia ametembelea jengo la oksijeni ambalo linahudumia wilaya za Mbinga, Ludewa, pamoja na wilaya ya Nyasa. Jengo hili limekuwa na mchango mkubwa katika kutoa huduma ya oksijeni kwa wagonjwa wanaohitaji matibabu ya papo kwa papo, yanayohitaji hewa ya Oksijeni

Akiwa katika Kata ya Mpepo, ametembelea  mpaka wa Tanzania na Msumbiji, eneo ambalo limekuwa na umuhimu mkubwa katika masuala ya usalama na ushirikiano wa kikanda. Akizungumza na wananchi  amewataka wananchi kuwa macho na kuhakikisha wanatambua na kutoa taarifa mapema kuhusu mgeni yeyote wasiyemfahamu, hasa wale wanaoingia au kutoka kupitia mpaka huo.

"Usalama wa mipaka yetu ni jukumu la kila mmoja wetu. Tunahitaji ushirikiano wa karibu kati ya wananchi na vyombo vya usalama ili kudumisha amani na kuzuia uhalifu katika maeneo yetu," amesisitiza Katibu Tawala huyo.

Amehitimisha Ziara yake kwa kutembelea na kukagua ujenzi wa Kituo cha Polisi cha Mpepo, ambacho kinatarajiwa kuwa na mchango mkubwa katika kuboresha usalama katika wilaya ya Nyasa na maeneo ya jirani na kuridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho na kuwahimiza wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa kuchangia ujenzi huo.

"Miradi ya usalama kama hii ni muhimu katika kujenga jamii salama na yenye utulivu. Kituo hiki cha polisi kitaongeza ufanisi wa kudhibiti uhalifu na kutoa huduma za haraka kwa wananchi," amesema Katibu Tawala, akiwataka wananchi wa Kata ya Mpepo na maeneo ya jirani kuwa mstari wa mbele katika kutoa taarifa za usalama.

 Amehamasisha uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kuwataka wananchi wote waliojiorodhesha kwenye Orodha ya wapiga kura wahakikishe wanapiga kura tarehe 27.11.2024.

“Uchaguzi ni haki yetu, lakini ni jukumu letu pia kuhakikisha kuwa unafanyika kwa amani na kwa kufuata sheria. Tunahitaji ushirikiano wa kila mmoja ili uchaguzi wa Serikali za Mitaa ufanikiwe kwa amani na utulivu,”

Ziara ya  Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma, imelenga kuhamasisha wananchi kuhusu umuhimu wa ushirikiano katika miradi ya maendeleo na kuimarisha ulinzi na usalama katika wilaya ya Nyasa. Alimshukuru Kamati ya Ulinzi na Usalama kwa ushirikiano wao, huku akiwataka wananchi kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha mafanikio ya miradi ya maendeleo na usalama.

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • Jela maisha Kwa Ubakaji

    May 27, 2025
  • Msigwa aipongeza Tamisemi kikao maafisa habari

    May 24, 2025
  • SERIKALI ilivyodhamiria kuboresha Barabara na madaraja

    May 23, 2025
  • Mwenge wa Uhuru wapitia miradi 76 mkoa wa Ruvuma

    May 17, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.