• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

YALIYOJIRI KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI HALMASHAURI YA WILAYA YA NYASA KUJADILI TAARIFA ZA ROBO YA PILI OCTOBA-DESEMBA 2024/2025

Posted on: February 24th, 2025

YALIYOJIRI MKUTANO WA BARAZA LA MADIWANI HALMASHAURI YA WILAYA YA NYASA, KUJADILI TAARIFA ZA ROBO YA PILI OKTOBA-DESEMBA 2024/2025

HALMASHAURI ya Wilaya ya Nyasa imefanya kikao cha Baraza la madiwani kujadili taarifa za robo ya pili (Oktoba-Desemba), kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Nyasa tarehe 24/02/2025.

Mkuu wa wilaya ya Nyasa Mhe. Peres magiri ametoa salamu za Serikali wilaya ya Nyasa, amesema Hali ya usalama iko vizuri licha ya kuwa na Tishio la mamba ambao hukamata wananchi wanaoenda kuoga na kuvua. Ametoa wito kwa wananchi kuchukua Tahadhari wanapoenda kuoga na kuvua. Aidha amesema wananchi wanaendelea vizuri na majukumu yao na kuwataka kuendelea kuchapa kazi kwa juhudi na maarifa ili kuiendeleza Wilaya ya Nyasa.

Amesema ameridhishwa na kasi ya ukusanyaji wa mapato kwa kuwa kila mwaka wa fedha kasi inaendelea kupanda kutoka Bilioni 1.2 mwaka 2021/2022 hadi kukukusanya bilioni 2.9 mwaka 2025/2026. Amempongeza Mkurugenzi Mtendaji na watumishi wote wanaohakikisha wilaya ya Nyasa inakua. Aidha ametoa wito kwa watumishi hao kuendelea kukusanya na kuvuka malengo ya ukusanyaji ili kutoa Huduma bora kwa wananchi na kuiendeleza Halmashauri yetu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa amewataka madiwani kuishi vizuri na watumishi wa Serikali wanaofanya kazi katika maeneo yao ya Utawala kwa kuwa wameletwa na Serikali ili kuinua ustawi wa jamii, hivyo mnatakiwa kuhakikisha watumishi hawa wanastawi na kuwapa ushirikiano sio kuungana na wananchi na kuwasema vibaya watumishi.

Mbunge wa Jimbo la Nyasa Mhandisi Stella Manyanya amesema Halmashauri ya wilaya ya Nyasa imeendelea kutatua kero za wananchi kwa kuwapa huduma bora za Afya na Elimu pamoja na miundombinu, hivyo amewataka wananchi kutumia vituo vya afya ili kupata huduma bora za afya na kuacha tabia ya kuchelewa kwenda Hospitali mara unapokuwa unaumwa hasa akina mama wajawazito, wanaotarajia kujifungua, wanatakiwa kuwahi vituo vya afya ili kupata huduma bora kwa vituo vya afya vipo, na vinaendelea kutoa huduma bora kwa wananchi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa bw. Khalid Khalif amesewataka madiwani kuendelea kuhamasisha ukusanyaji wa mapato na utekelezaji miradi ya maendeleo, inayotekelezwa katika maeneo yao na kuwataka wanapokutana na changamoto wasisite kumtaarifu ili aweze  kutatua changamoto kwa haraka.

Aidha Baraza hilo limepitisha Bajeti ya Tsh bilioni 29.9 kwa bajeti yote kwa mchanganuo ufuatao, bilioni 17.1 malipo ya mishahara bilioni 4.4 matumizi mengineyo bilioni 8.3 kwa ajili ya miradi ya maendeleo na kwa mapato ya ndani tunatarajia kukusanya bilioni 2.9.

Bw. Ngonyani ambaye ni Mkuu wa Divisheni ya Mipango na Uratibu, amevitaja vipaumbele vya bajeti ni kuboresha miundombinu ya elimu, Afya na kuongeza uzalishaji wa mazao ya Kimkakati kahawa, kokoa, michikichi kwa kutenga milioni 60 ili kununua mbegu na kuwagawia wananchi bure ili kuongeza uzalishaji wa mazao mbalimbali na kukamilisha ujenzi wa Ofisi za kata na vijiji.

Kwa upande wake waheshimiwa madiwani wamepongeza mikakati ya kuongeza uzalishaji wa mazao na utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa kusema kuwa watakuwa bega kwa bega kushirikiana na kuhakikisha Halmashauri ya Nyasa inasonga mbele kwa maendeleo.

Imeandaliwa na Netho Sichali

Afisa Habari

Kitengo cha mawasiliano Serikalini Wilaya ya Nyasa.

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • Jela maisha Kwa Ubakaji

    May 27, 2025
  • Msigwa aipongeza Tamisemi kikao maafisa habari

    May 24, 2025
  • SERIKALI ilivyodhamiria kuboresha Barabara na madaraja

    May 23, 2025
  • Mwenge wa Uhuru wapitia miradi 76 mkoa wa Ruvuma

    May 17, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.