• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

yafahamu Malikale na Ujio wa Dini Wilaya ya Nyasa

Posted on: August 12th, 2024

vivutio vya mambokale  vinapaswa kupewa kipaumbele kwa sababu vinachangia katika kukuza historia na kuendeleza utalii.Wilaya ya Nyasa imebarikiwa pia na utalii wa mambokale ambao unavutia wengi kujua masuala mbalimbali ya kihistoria katika wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma.

Vivutio vya mambokale katika wilaya ya Nyasa vimegawanyika katika sehemu ambazo ni historia za mambokale zilizofanywa na viongozi wa nchi  katika maeneo mbalimbali na kuingia kwa dini na madhehebu ambayo yameacha alama kubwa. 

Baadhi ya vivutio vya mambokale katika wilaya ya Nyasa  ni kile kilichopo  Katika  eneo la  Mbamba bay ambapo  Rais Mstaafu wa Awamu ya Kwanza Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Oscar Kambona katika harakati za kudai Uhuru walilala hapo miaka ya 1956 nyumbani kwa dada wa Oscar Kambona ambapo palikuwa na ofisi ya chama cha TANU.

 Magavana wa Shirikisho wa Rodesia na Nyasaland walikutana katika (Rest House) eneo la Mbamba bay jengo ambalo kwa sasa ni ofisi ya Afisa Mtendaji wa Kata ya Mbambabay wakiwa na lengo la kuagana kutokana na vuguvugu la waafrika kudai Uhuru 1959 kushika kasi. Jengo hilo lilijengwa kwa miti.

Kivutio kingine cha utalii wa mambokale ni Kuingia kwa dini  na madhehebu mbalimbali pia  sehemu kubwa ya utalii wa nyasa unaobeba historia.

Mwaka 1981 wananchi wa Lituhi waliahamishwa kwa ajili ya kupisha mafuriko yaliyosababishwa na kufungwa kwa Mto Shire nchini Malawi na baadaye mwaka 1987 Mwalimu Nyerere akiwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi alifika kwa ajili ya kutoa maamuzi magumu ya kuwarudisha katika makazi yao ya awali na baada ya kuongea na wananchi hao kwenye mti mtebhele (muyombo) ambao upo katika kijiji cha Mwera mpya kata ya Lituhi na baadae alipiga picha na mkewe katika eneo hilo kabla ya kuondoka. 

Dini iliyoanza kuingia katika wilaya ya Nyasa ni dini ya Kikristo,Mwinjilisti wa kwanza wa Anglikana William Parcival Johnson alianza kuhubiri Februari 9,1881 na akahamia rasmi Liuli mwaka 1906, alifariki Oktoba 11,1928 na kuzikwa Liuli.

Wakati huo ilitambulika kwa jina la DayosisI ya Nyasaland, ikafuata Dayosisi ya Southwest Tanganyika mwaka 1952 na baadaye kuitwa Dayosisi ya Ruvuma  mwaka 1971.

Mwinjilisti William Parcival Johnson awali wakati anaingia Nyasa alikuwa na lengo la kujenga kanisa Kijiji cha Hongi ambapo wenyeji hawakutaka na alifukuzwa ndipo akakilaani kijiji cha Hongi kiwe na sisimizi wengi, pia kiote majani yaitwayo mapelele ambayo kabla yake hayakuwapo. Historia na simulizi za wahenga zinatoa simulizi hizo za kusisimua.

Historia inaonesha kuwa Kanisa Katoliki wilayani Nyasa liliingia mwaka 1912 huko Nkaya na kuanzisha Parokia na baadae kujenga kanisa kubwa la Lituhi mwaka 1939. Mwanzilishi akiwa ni Padre Henrich Kunster.

 Uislamu uliingia Nyasa mnamo mwaka 1928, Sheikh wa kwanza aliitwa Mzee Bin Amanzi, Ilipofika mwaka 1932 Waasisi walijenga msikiti ambao miongoni mwao ni Twaib Abdallah, Akida Wabu, Mdoka, Ajali Hassan, Mfaume Bolin na Issa Kimambe.

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • Karibu Mwenge wa Uhuru Wilayani Nyasa

    May 11, 2025
  • Mwenyekiti wa Tume huru ya Uchaguzi Tanzania akagua vituo vya kujiandikisha Nyasa.

    May 04, 2025
  • Dc Nyasa awataka madiwani na watendaji kubuni vyanzo vipya vya mapato

    April 30, 2025
  • DC Nyasa azindua Kituo kipya cha Mafuta

    April 26, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.