• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

WILAYA YA NYASA YAWAAPISHA NA KUWAPA MAFUNZO VIONGOZI WAPYA WA SERIKALI ZA MITAA

Posted on: November 26th, 2019


Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma imeanza kuwaapisha na kuwapa mafunzo, viongozi wa Serikali za mitaa waliochaguliwa katika uchaguzi uliofanyika novemba 24 mwaka huu.

Zoezi la Viongozi hao kula kiapo na mafunzo ,  yanafanyika katika kila Makao makuu ya Kata husika, na wakili Loveness gwimile anawaapisha  kiapo cha utii na kutunza siri.

Kaimu Afisa uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Onesmo Mkandawile amesema kuwa kula kiapo kwa viongozi hao wa Serikali za Mitaa, ni Matakwa ya kisheria za uchaguzi wa Serikali za mitaa,ya mwaka 2019.  viongozi hao ili waweze kuanza kufanya kazi,  ni lazima waape ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa kufuata taratibu, kanuni, na sheria.

“Ndugu viongozi zoezi hili la kuwaapisha na matakwa ya kisheria ,hivyo kila kiongozi aliyechaguliwa anatakiwa aape kabla ya kuanza kutekeleza majukumu yake .Kiongozi yeyote asiyeapa hataruhusiwa kufanya kazi au kutekeleza majukumu yake”.alisema Mkandawile.

Aliongeza kuwa pamoja na kuapa wameona kama Halmashauri watoe pia  mafunzo, yatakayowawezesha kutekekeleza majukumu yao ipasavyo. Lengo kuu la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo  viongozi hao ili waweze kutatua changamoto mbalimbali za wananchi na kuwaunganisha ili waweze kutekeleza miradi ya maendeleo katika vijiji vyao.

Viongozi  wa vijiji wameipongeza Halmashauri ya Nyasa kwa kuwapa mafunzo elekezi na kuahidi kuwa watayatumia vizuri na watashirikiana na Halmashauri katika kuwahudumia wananchi wa Wilaya ya Nyasa.

Zoezi la kuwaapisha na Mafunzo,  yamefanyika,  katika kata ya Mbamba-bay, Kilosa, Mtipwili, Chiwanda, Lipingo, Liuli, na Kihagara.Kesho  zoezi hili litaendelea katika Kata ya Liwundi, Ngumbo,Mbaha na Lituhi.

Aidha kwa mujibu wa Kaimu Afisa uchaguzi  Bw. Mkandawile amesema mpaka jumamosi Halmashauri itakuwa imewaapisha Viongozi wote  wa vijiji waliochaguliwa Katika wilaya ya Nyasa.

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • Jela maisha Kwa Ubakaji

    May 27, 2025
  • Msigwa aipongeza Tamisemi kikao maafisa habari

    May 24, 2025
  • SERIKALI ilivyodhamiria kuboresha Barabara na madaraja

    May 23, 2025
  • Mwenge wa Uhuru wapitia miradi 76 mkoa wa Ruvuma

    May 17, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.