• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

WILAYA YA NYASA YAPOKEA MBEGU ZA MICHIKICHI

Posted on: March 31st, 2021

Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa imepokea Mbegu Elfu Arobaini (40,000) za Michikichi kutoka Taasisi ya Utafiti TARI iliyopo Kihinga Mkoani Kigoma, ili kuanzisha kitalu cha miche na kusambaza kwa Wakulima wa Wilayani hapa.

Lengo la Uanzishaji wa kitalu hiki ni kuboresha na utekelezaji wa kilimo cha Mazao ya kimkakati likiwemo zao la michikichi. Halmashauri inalenga kupanda Hekta 240 katika Kata kumi na moja (11) zilizopo mwambao wa Ziwa Nyasa, ili kukabiliana na uhaba wa mafuta na kuwaongezea kipato wananchi.

Akipokea mbegu hizo kwa niaba ya wananchi, Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Mh.Isabela O. Chilumba amesema “Mbegu hizo ni Ukombozi mkubwa kwa wakulima kwa kuwa mbegu hii ni ya kisasa na inachukua miaka mitatu kuanza kuvuna”. Awali kulikuwa na Mbegu ya kienyeji ambayo ilikuwa ikichukua miaka zaidi ya mitano na kuendelea mpaka  kufikia kuvuna.

Mh. Chilumba ameongeza kuwa kwa Ukanda wa mwambao wa Ziwa Nyasa kuna Kata 11 ambazo zina uwezo mkubwa wa kustawisha zao hili la biashara kwa kuwa awali walikuwa wakitegemea Uvuvi pekee, sasa zao hili limekuja kuwakomboa wakulima ili waongeze kipato na  kupata mafuta ya kupikia ya Mawese kutokana na zao hili la Mchikichi.

Aidha ametoa wito kwa wakazi wa Wilaya ya Nyasa kuchangamkia fursa ya Kilimo cha Michikichi ili wakuze kipato cha kaya na kutatua tatizo la mafuta ya kupikia Nchini.

Awali Akikabidhi mbegu hizo Mkurugenzi wa kituo cha Utafiti cha TARI Kihinga, Dkt Filson Kagimbo amesema amefika kukabidhi na kuotesha mbegu hizo kama wakulima wa Nyasa walivyoomba na Wilaya ya Nyasa ni moja kati ya Wilaya ambazo zina udongo na hali ya hewa inayofaa kuotesha  zao la Mchikichi, Ikiwa ni Utekelezaji wa Agizo la Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Mh. Kasim Majaliwa kwa kuitaka TARI kuzalisha na kusambaza Michikichi nchi nzima.

Ametoa wito kwa wananchi wa Wilaya ya Nyasa kuchangamkia fursa ya kilimo cha Michikichi kwa kuwa Mbegu hii ni ya kisasa na inazalisha mazao mara tano ya michikichi ya kienyeji ambapo kwa hekta inazalisha Tani 4 hadi 5 za Mafuta, ukilinganisha na miche ya kienyeji inayotoa Tani 1.6 ya Mafuta ya kwa hekta pia.

Naye Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Nyasa Bw Jimson Mhagama amesema atahakikisha anawasimamia wataalamu wa kilimo ili waweze kuwahamasisha wananchi wazalishe kwa wingi zao la Michikichi.

Baadhi ya Wananchi wa kikundi cha Nuru kutoka Nanungu kijiji cha Likwilu ambao wana Shamba Darasa la mfano kwa ajili ya kuwafundisha wakulima wa zao la Michikichi Wilaya ya Nyasa wameipongeza Serikali Wilayani Hapa kwa juhudi za kuwaletea mbegu hizo na kuwapa mahitaji wanayotaka na Kuboresha Zao la Michikichi.

Announcements

  • Tangazo la nafasi za kazi Halmashauri ya wilaya ya Nyasa December 01, 2025
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • TANGAZO la nafasi ya kazi February 03, 2023
  • View All

Latest News

  • Balozi wa Tanzania nchini Malawi atembelea Wilaya ya Nyasa

    December 06, 2025
  • Maonesho ya Nane Nane Kanda za Nyanda za juu kusini , Mguu sawa Kuanza leo

    August 01, 2025
  • UTEKELEZAJI KAMPENI YA CHANJO YA MIFUGO YAANZA NYASA

    July 12, 2025
  • MAKUNDI SOGOZI YA WHATSAAP YAPASWA KUJADILI MAENDELEO

    July 12, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.