• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

WILAYA ya Nyasa yakaribisha wawekezaji wa Zao la Kahawa

Posted on: September 15th, 2021

Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa kwa kushirikiana na Bodi ya Kahawa Tanzania, Tarehe 14.08.2021 imeadhimisha siku ya Wakulima wa kahawa maadhimisho yenye lengo la kutoa Elimu kwa wakulima wa kahawa, na kuhamasisha wakulima kulima zao hilo kitaalamu.

Maadhimisho hayo yamefanyika katika shamba darasa la Kahawa la Kikundi cha Pisi, Katika Kijiji cha Kingerikiti Kata ya Kingerikiti Wilayani Nyasa, na Mgeni Rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Nyasa  Kanali Laban Thomas aliyewakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Mhe Aziza Ally Mangosongo .

Akifungua Maadhimisho ya siku ya Kahawa, Mkuu wa Wilaya ya  Nyasa amewataka wakulima kuongeza ukubwa wa mashamba yao na kupanda mbegu aina ya Compact, ambayo ni mpya inavumilia ukame na inatoa mavuno bora na kuongeza kipato kwa wakulima,  na  Halmashauri kwa ujumla.

Ameongeza kuwa, kahawa ni zao la biashara la  kimkakati la Serikali ambalo linatakiwa uzalishaji wake uhamasishwe na wakulima wote waweze kuhamasika na kulima kulima kwa kufuata kanuni bora za kilimo cha zao la kahawa, kuanzia upandaji hadi uvunaji wake ili uweze kuongeza tija, na uzalishaji wa kahawa bora.

Ametoa wito kwa wawekezaji, kuja kuwekeza kilimo cha kahawa katika Wilaya ya Nyasa kwa kuwa kuna eneo kubwa la uwekezaji wa kilimo cha kahawa katika Tarafa ya mpepo, ambapo kuna Hekta 2169, ambazo hazijawahi kulimwa hivyo ni fursa kwa wawekezaji kuwekeza Wilayani hapa.

Awali akitoa taarifa fupi ya lengo la siku ya Kilimo cha kahawa, Kaimu Meneja wa Bodi ya Kahawa Mkoa wa Ruvuma Bw Rashid Rashid amesema Lengo la siku hiyo ni wakulima wapate elimu, jinsi ya uzalishaji bora wa zao la kahawa ambapo wakulima waliofundishwa kwa vitendo toka kuandaa shamba, kupanda, kutunza mpaka kuvuna wanatoa elimu kwa wakulima wenzao ambao hawajawahi kushiriki.

Aidha ameongeza kuwa wataalamu wa Zao la kahawa wamepata ufumbuzi wa zao la kahawa kwa kupanda mbegu mpya aina ya compact ambayo inavumilia ukame, inatoa mavuno bora,na haipatwi na magonjwa ya mara kwa mara.

Ameyataja mafanikio yaliyopatikana katika kilimo cha kahawa Wilaya ya Nyasa ni pamoja na kuongezeka kwa wakulima wa kahawa,upandaji wa mbegu bora aina ya Compact ambayo imeongeza uzalishaji  wa zao la kahawa, na hivi sasa Chama cha Msingi Kingerikiti Amcos kimeanza kukaanga na kuuza kahawa yake,hivyo ni mafanikio makubwa yaliyopatikana.

Kwa upande wao wakulima wa zao hilo wamesema zao la kahawa inawasaidia kupambana na umaskin,i kwa kuwa huwapa mavuno bora na fedha ambazo zinatatua changamoto zinazowakabili na kupata nyumba bora na kusomesha watoto wao.

Wilaya ya Nyasa ni mzalishaji mkubwa wa zao la kahawa na zao hili huchangia kwa asilimi 80 ya mapato ya ndani ya Halmashauri hivyo huhamasisha wananchi wa Tarafa ya Mpepo kuongeza uzalishaji wa zao hilo kwa kutoa elimu kwa wananchi juu ya upandaji ulimaji,uchakataji, na  mpaka kufikisha zao hilo sokoni na kwa sasa wakulima wamehamasika na kuongeza kilimo cha zao la kahawa.

Imeandaliwa na Netho Sichali

Afisa habari Nyasa dc

0767417597

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • Karibu Mwenge wa Uhuru Wilayani Nyasa

    May 11, 2025
  • Mwenyekiti wa Tume huru ya Uchaguzi Tanzania akagua vituo vya kujiandikisha Nyasa.

    May 04, 2025
  • Dc Nyasa awataka madiwani na watendaji kubuni vyanzo vipya vya mapato

    April 30, 2025
  • DC Nyasa azindua Kituo kipya cha Mafuta

    April 26, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.