• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

WILAYA YA NYASA YAJIPANGA KUKABILIANA NA CORONA

Posted on: March 18th, 2020

Wilaya ya Nyasa imejipanga kukabiliana na ugonjwa wa Corona kwa kutoa Elimu kwa Maafisa Watendaji Kata, na waganga wakuu wa Vituo vya afya na Zahanati zote za Wilaya ya Nyasa, ili wakatoe maelekezo kwa jamii inayo wazunguka ili, wajihadhari na ugonjwa wa corona.

Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Bi Isabela Chilumba, akiwa ameongozana na kamati ya Ulinzi na Usalama, Kaimu Mganga mkuu wa Wilaya ya Nyasa, Bi Engtrauda Ngondola pamoja na Afisa afya wa bandari ya Mbamba-bay, bw Antony Misana  walitoa mafunzo ya kukabiliana na Virusi vya Corona, Hivi karibuni katika Ukumbi wa Kepten John Komba.

Bi Chilumba alifafanua kuwa , amelazimika kutoa mafunzo  kwa viongozi wa Kata na Waganga wakuu wa zahanati na Vituo vya Afya kwa kuwa ni wataalam, wanaokutana moja kwa moja na jamii, hivyo wana nafasi kubwa ya kuwaelekeza wanajamii ili waweze kufahamu ugonjwa huu, na kutowatisha wananchi au kuzua tafrani miongoni mwa jamii kwa ujumla.

Aliongeza kuwa, Maelelekezo zaidi yanaendelea kutolewa na Viongozi wa Kitaifa, hivyo wananchi wanatakiwa kuyafuata kwa umakini, na sisi kama Wilaya ya Nyasa, tumepakana na Nchi mbili ya Malawi na Tanzania,hivyo tunatakiwa kuwa makini kwa kuwa hatujui ugojwa huu utaanzia wapi, hivyo Viongozi wote wa vijiji, Kata , na watoa huduma za afya na Wilaya kwa ujumla tunatakiwa kuwa makini na Ugojwa wa Corona.

“Ndugu Waganga wakuu wa Zahanati, Vituo vya Afya na Watendaji wa Kata zote katika Wilaya ya Nyasa nimelazimika kutoa mafunzo haya kwa kuwa Nchi yetu  na Dunia kwa ujumla imekumbwa na Ugonjwa  hatari wa Corona,  kwa sasa Tayari umeshaingia nchini kwetu kama Taarifa toka kwa Waziri Mkuu Mh Cassim Majaliwa pamoja na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu  Inavyosema, kwa hiyo sisi kama Viongozi tunatakiwa kuchukua hatua Kwanza ya kuutaarifu umma  lakini kutozua tafrani. Tunatakiwa kuwaelekeza kwa umakini jinsi unavyoambukizwa, Dalili, na nini kifanyike baada ya kuona dalili za Ugonjwa huu na kwa kuwa Mganga mkuu wa Wilaya yupo Atatelekeza namna ya kujikinga na Ugonjwa huu kwa kuwa Kinga ni bora kuliko kinga.”

Aidha alisema wageni wote kutoka Nchi ya Msumbiji na Malawi wanaotibiwa Zahanati za hapa Nyasa wachukuliwe kwa Tahadhari, kwa kuwa bado hakuna agizo lolote linalowahusu. Aidha kama Wilaya ya Nyasa tayari wamejipanga na alisema wametenga jengo moja lililopo Hospitali ya Wilaya ya Nyasa, kwa ajili ya kuwahifadhi wagonjwa wa Corona kama watatokea mkwa kuwa kinga ni bora kuliko Tiba.

Kaimu Mganga mkuu wa Wilaya Englitrauda Ngondola alisema Dalili kuu za ugonjwa wa Corona ni pamoja na Homa kali, Uchovu na Kikohozi kikavu na zinatokea taratibu. Dalili kubwa na inayoweza kutia hofu, ni mtu kukosa pumzi,aliongeza kama wahudumu wa afya watamkuta mtu akiwa na dalili hizo wanatakiwa kutoa taarifa haraka kwa Mganga mkuu  wa Wilaya na aliongeza kuwa tunatakiwa kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima na knawa mikono na sabuni kwa maji yanayotiririka.

Aidha aliwaomba waganga wakuu na maafisa watendaji Kata kutoa mafunzo kwa wananchi  juu ya ugonjwa huu wa Corona bila kuzua hofu kwa jamii kwa ujumla.

Naye afisa Bandari wa Mbamba-bay  bw. Misana alisema atahakikisha wageni wote watakaoingia kupitia Bandari ya Mbamba-bay , atahakikisha wanakuwa na tahadhari kuhakikisha mtu mwenye dalili za ugonjwa huu anaripotiwa kwa haraka.

Kwa upande wao Maafisa Watendaji wa kata na Waganga wakuu wa vituo vya Afya na Zahanati wamesema wamepokea mafunzo hayo na watatoa elimu kwa wananchi wote wa Wilaya ya Nyasa na kutoa Taarifa Mara moja Kama kutatokea kesi ya aina hiyo.

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • Jela maisha Kwa Ubakaji

    May 27, 2025
  • Msigwa aipongeza Tamisemi kikao maafisa habari

    May 24, 2025
  • SERIKALI ilivyodhamiria kuboresha Barabara na madaraja

    May 23, 2025
  • Mwenge wa Uhuru wapitia miradi 76 mkoa wa Ruvuma

    May 17, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.