• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

WILAYA YA NYASA YABORESHA HUDUMA ZA AFYA.

Posted on: January 17th, 2019

Wilaya ya nyasa imefanikiwa kuongeza idadi ya vituo vya  kutolea huduma za afya kutoka 29 mwaka 2016/2017 hadi kufikia 35 mwaka wa fedha 2018/2019 na kuboresha afya za wananchi ili wapate maendeleo. Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Nyasa  Dkt Oscar  Mbyuzi alisema Wilaya imeendea kuboresha vituo vya kutolea huduma hivi karibuni wakati akiongea na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake.

Dkt mbyuzi alifafanua kuwa Wilaya ina jumla ya vituo vya kutolea huduma 35, ambavyo kati ya hivyo Hospitali ni 2, Vituo vya Afya ni 5, na Zahanati ni 28, ambapo Hospitali  zote 2 zinamilikiwa na mashirika ya Dini, Vituo vya Afya 4 vinamilikiwa na Serikali na kituo cha afya kimoja kinamilikiwa na shirika la dini.

Dkt Mbyuzi aliongeza kuwa zahanati 6 zinamilikiwa na Mashirika ya dini na 1 inamilikiwa na mtu binafsi, na Zahanati  21 zinamilikiwa na Serikali.   Wilaya imeendelea kutekeleza  ujenzi wa Miradi mbalimbali katika sekta ya Afya, hususani ujenzi wa Vituo vya Afya ambapo kwa sasa kuna ujenzi wa  Vituo vitatu.

Alivitaja vituo hivyo kuwa ni kituo cha Afya Kihagara ujenzi huu unahusisha jengo la upasuaji, jengo la wagonjwa wa nje (OPD), jengo la matibabu, jengo la kutunza na kugawia Dawa pamoja na jengo la Ushauri, mradi huu unajengwa na Wakala Wa Majengo Tanzania (TBA). Mradi huu ulianza kutekelezwa tarehe 4 April 2017 na sasa upo katika hatua za ukamilishaji ambapo mpaka sasa Jumla ya Tsh. 493,363,294.89 zimetumika.

Mradi huu hadi kukamilika kwake utagharimu jumla ya Tsh. 585,505,575.00 ambazo ni fedha za Ruzuku ya Miradi ya Maendeleo ya Serikali za Mitaa (LGCDG).

Mkurugenzi huyo alizidi kutaja kituo kingine kuwa ni Kituo cha Afya Mbamba Bay, ambacho ujenzi wa wodi daraja la kwanza umeanza kwa nguvu za Wananchi, Watumishi wa ngazi zote, na Mhe. Mbunge wa Jimbo la nyasa Stela Manyanya Hadi kufikia sasa Watumishi wamechangia jumla ya Tshs. 650,000, Mhe. Mbunge kupitia mfuko wa jimbo amechangia jumla ya Tshs. 5,000,000 na Halmashauri imechangia Tshs. 15,000,000 kutoka mapato ya ndani, Ewura TSH. 5,000,000.00 NSSF Tshs. 5,000,000.00 SUMATRA Tsh. 5,000,000.00, BRELLA Tsh. 3,000,000, Mdaka Five Tsh. 1,000,000.00, mapato ya Vituo Tsh. 300,000. 

Aidha katika kuhamasisha Wadau  mbalimbali wa maendeleo wamechangia michango yao Tshs. 460,000 na kufanya jumla Tshs. 40,410,000 zilizopokelewa. Hata hivyo mradi huu hadi kukamilika kwake utagharimu jumla ya Tshs. 190,000,000.00,na aliongeza kuwa kwa sasa kuna ujenzi wa 

Kituo cha Afya Mkili ujenzi huu unahusisha jengo la upasuaji, jengo la wagonjwa wa nje (OPD), jengo la matibabu, jengo la kutunza na kugawia dawa pamoja na jengo la maabara. Mradi huu unagharimu jumla ya Tshs. 400,000,000.00 hadi kukamilika kwake na ujenzi unaendelea kwa sasa ujenzi ambao ni wa majengo ya kisasa yaliyojengwa kwa uimara wa hali ya juu. Aidha baraza la madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa lmeridhia kuongeza kiasi cha tsh. 94,000,000.00 kutoka mapato ya ndani ili kuwezesha kituo hicho kukamiika kwa ufasaha

 Lakini pia Tshs. 300,000,000.00 kwa ajili ya vifaa vya kituo hicho pindi kitakapokamilika. Fedha hizi Tshs. 300,000,000.00 hazitakuwa taslimu vitakuwa ni vifaa vya thamani ya fedha hizo Serikali Kuu italipa Bohari Kuu ya Dawa na Kituo kitapokea vifaa hivyo vya thamani hiyo (Receipt inkind) kutoka Bohari Kuu ya Dawa.

Hata hivyo alibainisha kuwa Wilaya imeendelea kuhakikisha upatikanaji wa chanjo mbali mbali za watoto na mama wajawazito kama vile chanjo za kukinga kifua kikuu, ugonjwa wa kupooza, kukinga magojwa ya pepopunda, donda koo, homa ya ini na kifaduro. Vichomi, uti wa mgongo, na Surua.

Kaimu mganga mkuu wa Wilaya ya Nyasa Dkt Aaron Hyera wakati akiwa katika ufunguzi na uhamasishaji wa kampeni ya upimaji wa virusi vya ukimwi kwa wanaume ya Pima Ishi Jitambue katia kijiji cha litumba kuhamba katika kata ya Linga aliwathibitishia wananchi kuwa Kuanzia mwanzoni mwa mwezi Januari 2018 hadi sasa hatuna upungufu wa chanjo kwa Wilaya ya Nyasa. Malengo nikufikia asilimia 95% ya watoto wote kuwa wamepata chanjo kwa sasa tupo 92%.

Naye Mbunge wa Jimbo la Nyasa ambaye pia ni Naibu Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Stella Manyanya ameipongeza Serikali kwa kuleta fedha za ujenzi wa miundombinu pamoja na madawa katika Wilaya ya Nyasa hivyo kuwapunguzia kero wananchi wa Wilaya ya Nyasa ambao walikuwa wanapata huduma za afya kwa shida kwa kipindi cha Nyuma lakini kwa sasa zimeboreshwa na hakuna shida kwa wakazi wa Jimbo la Nyasa japo bado kuna uhaba wa kituo cha afya kimoja katika kata ya Kingerikiti Tarafa ya Mpepo Wilayani Nyasa.

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • UTEKELEZAJI KAMPENI YA CHANJO YA MIFUGO YAANZA NYASA

    July 12, 2025
  • MAKUNDI SOGOZI YA WHATSAAP YAPASWA KUJADILI MAENDELEO

    July 12, 2025
  • DC MAGIRI AZINDUA RASMI BODI YA MAJI WILAYA YA NYASA

    July 12, 2025
  • DKT.SAMIA AMWAGA TENA MAMILIONI YA MIRADI NYASA

    July 10, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.