• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

WAZIRI WA UJENZI ARIDHISHWA NA UJENZI WA BARABARA YA MBAMBA-BAY- MBINGA.

Posted on: October 9th, 2018

Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Izack Kamwele ameridhishwa na maendeleo ya Mradi wa ujenzi wa barabara ya Mbinga –Mbamba-bay (Kilomita 67 kiwango cha Lami) unaoendelea na hajaridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa daraja la mto Ruhuhu unaounganisha mkoa wa Ruvuma na Njombe.

Aliyasema hayo jana wakati akiongea na waandishi wa habari  katika eneo la chunya Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma, kwenye kiwanda cha kusaga mawe kwa ajili ya kokoto wakati akikagua ujenzi wa barabara ya Mbinga-Mbamba-bay (kiwango cha Lami) yenye urefu wa kilomita 67 .

Mh. Kamwele alifafanua kuwa ameridhishwa na ujenzi wa barabara hiyo jinsi unavyoendelea na maandalizi yake na kumtaka mkandarasi afanye kazi kwa juhudi kubwa na maarifa ili kazi iendelee kwa nguvu zote ili kuwapa wananchi fursa ya kuwa na barabara nzuri watakayoitumia katika shughuli zao za kiuchumi.

Aliongeza kuwa tangu asubuhi alikuwa akitembelea miradi inayotekelezwa katika mkoa wa Ruvuma hususani alikagua barabara ya Likuyufusi –mkenda ambayo alisema upembuzi yakinifu ulishafanyika lakini kutokana na ugunduzi wa makaa ya mawe katika eneo la Muhukuru wamelazimika kufanya tena upembuzi huo kwa kuwa magari mengi yenye uzito mkubwa yatapita katika barabara hiyo na barabara ya kitai-lituhi na lituhi-mbamba-bay pamoja na kukagua daraja la mto Ruhuhu linalounganisha mkoa wa Ruvuma na Njombe.

“Ndugu wanahabari nimekuwepo tangu asubuhi nikiwa nakagua miradi ya maendeleo na hii leo nimekagua barabara ya Likuyufusi –Mkenda ,kitai-Lituhi na Lituhi-Mbamba-bay na Mbamba-bay-mbinga kwa kifupi na ujenzi wa barabara ya Mbinga-Mbamba-bay kwa kuwa maandalizi yake ni mazuri na hata kasi ya ujenzi ni nzuri na inaendelea vizuri Lakini Sijaridhika na ujenzi wa Daraja la mto Ruhuhu kwa kuwa Mkandarasi huyo ni Mtanzania lakini hana uwezo wa kujenga lile Daraja. Nimeongea nae mkandarasi anayejenga daraja na sijataka nitoe amri ya kumwachisha kazi lakini nimemshauri aonane na wakala wa barabara Tanroad Mkoa wa Ruvuma ili akabidhi yeye mwenyewe ile kazi ili iweze kukamilika kwa muda wa miezi miwili kwa kuwa kazi iliyobaki siyo kubwa sana.”

Nae Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Isabela Chilumba alimpongeza waziri huyo kwa mikakati ya ujenzi wa barabara hizo na kusema kuwa kwa niaba ya wananchi wa Wilaya ya Nyasa anaishukuru sana Serikali ya awamu ya tano kwa kujenga Barabara za huku mpakani mwa Tanzania kwa kuwa barabara ya Lituhi Mbamba-bay iko karibbu mpakani mwa Tanzania na Malawi upande wa Tanzania hivyo itasaidia sana katika ukuaji wa uchumi kwa wakazi wa Wilaya ya Nyasa.

Katika hatua nyingine Mhandisi Kamwele amefurahi kuona rasilimali ya makaa ya mawe iliyopo katika mkoa wa Ruvuma, Muhukuru Wilayani Songea pamoja na Ruanda Wilayani Mbinga kwa kuwa ni vichocheo vya ukuaji wa sekta ya Viwanda kwa kuwa Viwanda vingi vinatumia makaa ya mawe na akavitaja viwanda hivyo kuwa ni cha Dangote cha Mtwara na viwanda vya siment cha Tanga na Dar es salaam na viwanda vingine vya nchi jirani za Rwanda na Kenya.

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • RAIS SAMIA AMWAGA MAMILIONI YA EDHA KUIMARISHA SEKTA YA AFYA NYASA DC

    June 28, 2025
  • RAIS SAMIA AMWAGA MAMILIONI YA EDHA KUIMARISHA SEKTA YA AFYA NYASA DC

    June 28, 2025
  • TAARIFA YA MAENDELEO YA JAMII

    June 26, 2025
  • KICHEKO CHATAWALA TAFRIJA YA KUWAAGA MADIWANI

    June 19, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.