• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

WAZIRI MWAKYEMBE. Uandishi wa habari sio kimbilio la waliofeli

Posted on: August 17th, 2020

WAZIRI wa Habari, Sanaa,Utamaduni na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe hivi karibuni amefanya ziara ya kikazi mkoani Ruvuma na kuzungumza na wadau wa Habari katika ukumbi wa Mipango uliopo ofisi ya Mkuu wa Mkoa mjini Songea.

Katika ziara yake Waziri Mwakyembe ametembelea maeneo ya kihistoria yakiwemo Makumbusho ya Taifa ya Majimaji  kutembelea mitambo ya  TBC  Kanda ya ziwa Nyasa,vituo viwili vya redio binafsi vya Jogoo na Key FM na hatimaye kuzungumza na wadau wa habari.

Akizungumza na wadau wa habari,Waziri Mwakyembe amesema kwa muda mrefu wanahabari hapa nchini wamedharauliwa na kukosa haki zao za msingi wanazostahili kupata kama wanahabari.

“Mimi ni mwanahabari mwenzenu, nimekulia humo potelea mbali anayeficha kidonda haponi,Hii tasinia inawezesha nchi na Demokrasia kufanya kazi,imekuwa ni kimbilio la mtu anayefeli duniani,uandishi wa habari siyo wa kupokea makapi’’,amesisitiza Mwakyembe.

Waziri wa Habari ameongeza kuwa Mwandishi ni mwalimu,ni mkalimani,ni mfasili na  mchambuzi wa masuala mbalimbali na kwamba mtu yeyote  ambaye hakidhi vigezo siyo mwandishi wa habari.

Hata hivyo amekiri kuwa hapo awali makosa yalifanyika kwa kuichukulia fani ya uandishi wa habari ni kama makapi ya wanaofeli ambapo mwaka 2016 iliundwa sheria  na kwamba katiba inatambua uandishi wa habari ni taaluma,na kazi ya uandishi wa habari ni hatari na inampasa mwanahabari  kuwekewa Bima,pia aingizwe kwenye mifuko ya hifadhi ya mifuko ya Taifa.

“Sheria ya habari imeundwa  baraza Huru la Habari tulejee kwenye Misimamo tumeunda kamati ya Baraza itakuwa na mamlaka kama mahakama tumegundua bila serikali kuingiza pesa kwenye mifuko yao wengi watashindwa kusoma na kilele chake  mwaka 2021 wanahabari tutakao anza nao kazi 2022 watakuwa wana elimu kuanzia Diploma na Degree’’,alisema.

“Siyo kwamba sina huruma, nina huruma sana,kuna watu wana uzoefu mkubwa lakini hawana Elimu inayotakiwa vijana wote wadogo hakikisheni mnakimbia kwenda kusoma”,alisisitiza Waziri wa Habari.

Katika hatua nyingine Waziri Mwakyembe amekoshwa    shule ya Ruhuwiko Sekondari  iliyopo Songea Mjini kwa kufanya vizuri katika michezo ya UMISETA kitaifa iliyofanyika mwaka 2019 mkoani Mtwara.

Kaimu Afisa Michezo Mkoa wa Ruvuma Anzawe Chaula amesema  mafanikio waliyopata  Kuimarisha Michezo kwa Shule za Msingi na Sekondari  ngazi ya mkoa, ambapo katika mashidano ya UMISETA taifa mwaka 2019  timu ya mpira wa miguu ya mkoa wa Ruvuma iliibuka kinara kitaifa  na kuchangia golikipa bora ambaye aliweza kwenda kushiriki mashindano ya  Afrika Mashariki yaliyofanyika nchini Kenya.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Ufundi TBC Mhandisi Upendo Mbele amesema usikivu wa  TBC Taifa KATIKA Mkoa wa Ruvuma kwa sasa ni mzuri tukilinganisha na miaka ya 80 ambapo mitambo yake ilichakaa  na usikivu ulikuwa ni hafifu.

Amesema Serikali  kupitia shirika lake la utangazaji  ilimeamua kuweka mitambo mingine mipya ya FM ambapo hadi sasa katika nchi nzima kuna mitambo 67.

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • Jela maisha Kwa Ubakaji

    May 27, 2025
  • Msigwa aipongeza Tamisemi kikao maafisa habari

    May 24, 2025
  • SERIKALI ilivyodhamiria kuboresha Barabara na madaraja

    May 23, 2025
  • Mwenge wa Uhuru wapitia miradi 76 mkoa wa Ruvuma

    May 17, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.