• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

WAZAZI NYASA WATAKIWA KUCHANGIA CHAKULA MASHULENI

Posted on: July 6th, 2020

Katibu wa  jumuiya ya wazazi CCM, Wilaya ya Nyasa  Abdul Sikitiko amewataka wazazi  wa Wilaya ya Nyasa, kuchangia chakula na kuhakikisha wanafunzi wote wananakula shuleni  ili waweze kusoma kwa bidii.

Ameyasema hayo hivi karibuni, wakati akikagua maendeleo ya elimu toka shule zifunguliwe na kuona ni namna gani wanafunzi wanafundishwa ili kujihadhari na ugonjwa wa Corona, pamoja na kukagua  miradi ya elimu katika shule za Sekondari Limbo, lundo na shule za msingi Likwilu na Mwongozo  Wilayani hapa, ili kubaini changamoto zinazowakabili walimu na wanafunzi na jamii inatatuaje changamoto hizo.

Bw,Sikitiko alifafanua kuwa hajaridhishwa na wanafunzi kutokula shuleni, kwa kuwa kila shule aliyopita wanafunzi walikuwa hawana utaratibu wa kula shuleni, hali inayosababisha wanafunzi wengi kukaa na njaa shuleni, na wengine kuletewa chakula shuleni na wazazi wao, na wasioletewa wanakaa bila kula tangu asubuhi mpaka jioni hali ambayo inawafanya kutoweza kuhimili masomo.

Aliongeza kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imewapunguzia mzigo wa hali ya juu wazazi , kwa kutoa elimu bila malipo kuanzia darasa la awali hadi kidato cha nne. Wazazi majukumu waliyonayo ni kuhakikisha watoto wanakuwa na sare za shule, na kuhakikisha wanapata chakula cha mchana ili waweze kusoma kwa bidiii.

“Kwa kweli sijaridhishwa na vitendo vya  wazazi kutochangia chakula na wanafunzi wengi wanasoma bila ya kupata chakula kama nilivyozungumza nao hivyo naagiza wazazi wote wilayani Nyasa kuhakikisha wanashirikiana kuhakikisha watoto wanapata chakula cha mchana mashuleni, kwa kuwa watoto hawa hata wakikaa majumbani mwetu si wanakula? Kwa nini wasichangie na kula mashuleni na hii ni mbinu nyingine ya kupunguza utoro na kuhamasisha wanafunzi kuja mashuleni.Watoto wakiona chakula kinatolewa shuleni watakuwa na ari ya kuja shuleni. Kwa hiyo kuanzia leo hakikisheni watoto wanakula mashuleni.” Alisema Sikitiko.

Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Nyasa ambaye pia ni Ofisa Elimu Msingi, Bw Said Kalima alisema utaratibu wa wanafunzi kula mashuleni unatekelezwa vizuri katika Tarafa ya Mpepo na kuleta changamoto katika Tarafa za Ruhekei na Ruhuhu Wilayani Nyasa. Na alimpongeza Katibu huyo kwa kuiona changamoto hiyo na kumueleza iwapo wazazi watatatua changamoto hiyo itaongeza ari ya kujifunza na kupandisha ufaulu kwa wanafunzi wa Wilaya ya Nyasa.

Ziara hii ni ya kikazi ya siku moja ambayo alikagua shule za sekondari ya Limbo, lundo na shule za msingi Likwilu na Mwongozo  pia alipata kuongea na kamati za shule hizo na kukubaliana na kamati hizo changamoto walizozikuta watazitatua haraka iwezekanavyo.

Aidha aliwapongeza wazazi hao kwa kushirikiana na Serkali kutekeleza miradi ya maendeleo katika maeneo yao hasa katika shule za mwongozo na Likwilu ambapo walikuwa wkijenga miradi ya vyoo vya wanafunzi na kuona wanafunzi wameelekezwa namna ya unawaji mikono mara wanapoingia eneo la shule.

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • Jela maisha Kwa Ubakaji

    May 27, 2025
  • Msigwa aipongeza Tamisemi kikao maafisa habari

    May 24, 2025
  • SERIKALI ilivyodhamiria kuboresha Barabara na madaraja

    May 23, 2025
  • Mwenge wa Uhuru wapitia miradi 76 mkoa wa Ruvuma

    May 17, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.