• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

WATAALAMU WASHAURIWA KUSHIRIKIANA KUKABILIANA KUDHIBITI MAGONJWA YA MLIPUKO

Posted on: October 6th, 2020

MTAALAMU wa Epidemiolojia na Udhibiti wa  Magonjwa wa Wizara ya Afya na Maendeleo ya Jamii ,Jinsia,Wazee na Watoto Dr.Azma Simba, ametoa rai kwa wataalam kuungana na kushirikiana  ili  kukabiliana na magonjwa ya milipuko na kuimarisha usalama wa afya duniani.

Dr.Simba ametoa rai hiyo wakati anawasilisha mada ya agenda ya kukabiliana na matukio muhimu ya kiafya ya kimataifa, kwenye mafunzo ya utayari wa kukabiliana na magonjwa mlipuko kwa timu za dharura kwa wataalam kutoka mikoa ya Ruvuma na Mtwara.

Akizungumza katika mafunzo hayo ambayo yamefanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Tiffany mjini Mtwara, Dr.Simba amesema dunia imeathirika zaidi na magonjwa ya milipuko yakiwemo ebola na COVID 19 na kwamba mwaka 2014 Agenda ya Afya Duniani ilianzishwa kwa lengo la kuhakikisha Dunia inakuwa salama kutokana na milipuko ya magonjwa hayo.

“Nchi nyingi duniani zimeweka jitihada kubwa katika kujilinda na magonjwa ya mlipuko,hata hivyo ni vema watalaam kufanya kazi kwa ushirikiano ili pawepo na usalama wa afya duniani’’,alisema.

Mtaalam huyo wa kudhibiti magonjwa amesema, kupitia agenda ya afya duniani,imetolewa miongozo na kanuni za kimataifa zinazoongoza kukabiliana na magonjwa ya milipuko.

Ameyataja madhumuni ya Agenda ya afya ya dunia kuwa ni  kuwepo kwa mifumo ya afya ambayo imejikita kuzuia,kutambua mapema na kukabiliana na ugonjwa unapotokea na kwamba milipuko mingi ya magonjwa inayotokea inaweza kuzuilika kwa njia ya chanjo.

Hata hivyo ametoa rai kwa  timu za dharura za kukabili magonjwa ya mlipuko katika ngazi za Halmashauri na Mkoa  kufanya ufuatiliaji wa magonjwa kwa wakati na kutoa taarifa mapema katika ngazi husika.

Kwa upande wake Daktari wa mifugo  Dr.Moses Ole Neselle kutoka Shirika la Chakula na Kilimo Duniani(FAO) akitoa mada kwenye mafunzo hayo,ameyataja magonjwa sita ya kipambele ambayo yanaambukiza kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu kuwa ni Kichaa cha mbwa  ambacho kinatarajiwa kutokemezwa mwaka 2030.

Ameyataja magonjwa mengine kuwa ni homa ya bonde la ufa,kutupa mimba kwa wanyama,mafua ya ndege,kimeta na ugonjwa wa ebola na amesisitiza kuwa magonjwa hayatambui mipaka ya nchi hivyo ni vema wataalam wote kushirikiana kukabiliana na magonjwa hayo.

Amesema asilimia 50 ya magonjwa yote yanaambukizwa kupitia virusi na kwamba asilimia 60 ya magonjwa ya binadamu yanasababishwa na wanyamapori hivyo ameshauri kuwepo mpango mkakati wa kukabiliana na magonjwa hayo.

Naye Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Profesa Rudovick Kazwala imesisitiza kuwa katika kutokomeza magonjwa ya mlipuko ni lazima wataalamu wafanye kazi kwa kushirikiana ili kutoa matokeo chanya.

Imeandikwa na Albano Midelo na Netho Credo

Maafisa serikalini

Mtwara

Oktoba 6,2020

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • Jela maisha Kwa Ubakaji

    May 27, 2025
  • Msigwa aipongeza Tamisemi kikao maafisa habari

    May 24, 2025
  • SERIKALI ilivyodhamiria kuboresha Barabara na madaraja

    May 23, 2025
  • Mwenge wa Uhuru wapitia miradi 76 mkoa wa Ruvuma

    May 17, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.