• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

Wahandisi ujenzi msikae ofisini nendeni mkasimamie miradi-mhe. Magiri

Posted on: March 20th, 2025


Albano Midelo na Netho Sichali,Mbambabay 

Wataalamu wa ujenzi kutoka Halmashauri zote nane za Mkoa wa Ruvuma wameanza kikao kazi  cha kuwajengea uwezo  kuhusu usimamizi na ufuatiliaji katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili kuhakikisha miradi yote  mwaka 2024/2025  inakamilika kabla ya Mei 30 mwaka huu.


Kikao kazi hicho kimefanyika kwenye ukumbi wa St.Vinsenti mjini Mbambabay wilayani Nyasana mgeni Rasmi  ni  Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma aliyewakilishwa na Mheshimiwa Peres Magiri ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Nyasa.

Akizungumza kabla ya kufungua kikao kazi hicho Mheshmiwa Magiri amewataka watalaamu  hao wa ujenzi kuacha kukaa ofisini badala yake waende kusimamia miradi katika kila hatua ya utekelezaji ili iweze kukamilika kikamlifu na kwa wakati.

‘’Unakuta mradi unajengwa mtaalam wa ujenzi hajawahi Kwenda kukagua,wananchi wanaendelea na ujenzi ,hivyo mradi kupoteza ubora unaotakiwa,nawaomba baada ya kikao kazi hiki mbadilike’’,alisisitiza.

Amesema baada ya kukamilika kwa kikao kazi hicho anaamini kwamba miongoni mwa malengo yaliyokwekwa likiwemo la kumaliza  ujenzi wa miradi ifikapo Mei 30 mwaka huu litafikiwa kwa kuhakikisha miradi  yote wanayosimamia  iwe imekamilika kulingana na maelekezo.

Awali akitoa taarifa kwenye kikao kazi hicho Katibu Tawala Msaidizi Miundombinu Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Girbert Simiya amekitaja kikao kazi hicho kinawahusisha watalaam wa ujenzi,wabunifu majengo na wakadiriaji majengo wa Mkoa wa Ruvuma  waliopo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na katika Halmashauri zote  nane.

Simiya amesema hadi sasa Mkoa wa Ruvuma una watalaamu 64 wa ujenzi kati yao wahandisi 20,wabunifu majengo watano,wakadiriaji majengo 11 na mafundi sanifu 28.

Ameitaja miradi inayoendelea kutekelezwa katika Mkoa wa Ruvuma kuwa ni Pamoja miradi ya barabara yenye thamani ya shilingi bilioni 70 na mradi wa  ujenzi wa bandari ya Mbambabay wenye thamani ya shilingi bilioni 80.

Miradi mingine ameitaja kuwa ni miradi ya miundombinu ya elimu kupitia program ya BOOST yenye thamani ya shilingi bilioni 3.5 na program ya SEQUIP yenye thamani ya shilingi bilioni 14.6 na miradi ya program ya SWASH yenye thamani ya Zaidi ya shilingi bilioni moja.

Katika kikao kazi hicho mada mbalimbali zitafundishwa zikiwemo utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Halmashauri zote na usimamizi na ufuatiliaji wa miradi.

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • Jela maisha Kwa Ubakaji

    May 27, 2025
  • Msigwa aipongeza Tamisemi kikao maafisa habari

    May 24, 2025
  • SERIKALI ilivyodhamiria kuboresha Barabara na madaraja

    May 23, 2025
  • Mwenge wa Uhuru wapitia miradi 76 mkoa wa Ruvuma

    May 17, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.