• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

WANANCHI Wilayani Nyasa Waipongeza TARURA

Posted on: January 21st, 2025

BAADHI ya wakazi wa wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma,wameipongeza Serikali kupitia Wakala wa Barabara za vijijini na mijini(TARURA) kwa kuboresha miundombinu na kujenga barabara za mitaa katika mji mdogo wa Mbambabay kwa kiwango cha lami.

Wamesema,ujenzi wa Barabara hizo umesaidia kurahisisha huduma ya usafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine, kuondoa adha ya vumbi kipindi cha kiangazi na matope kila inapofika msimu wa mvua pamoja na maeneo yao kupanda thamani ikilinganishwa na siku za nyuma.

Petro Zambala mkazi wa Mbambabay alisema,uamuzi wa Serikali ya awamu ya sita kujenga barabara kwa kiwango cha lami katika mji huo utaharakisha maendeleo na kuchochea kukua kwa uchumi wa mtu mmoja mmoja na wilaya ya Nyasa.

Alisema,kabla ya barabara za lami baadhi ya huduma za kijamii zilipatikana kwa shida kwa sababu walishindwa kufika maeneo ya kutolea huduma hizo kwa wakati, jambo lililosababisha kuwa na maisha magumu.

Mkazi mwingine wa Mbambabay Nikaya Mbalale alisema,tangu Serikali ya awamu ya sita ilipoingia madarakani kuna mabadiliko makubwa katika mji huo hasa baada ya TARURA kupatiwa fedha nyingi ambazo zimewezesha kuboresha miundombinu ya barabara zake kwa lami, tofauti na siku za nyuma ambapo barabara nyingi za mitaa zilikuwa za vumbi.

Alisema,kuimarisha na kuboreshwa kwa barabara hizo zimehamasisha na kuwavutia watu wengi kwenda kuwekeza katika Mji wa Mbambabay ambao wananchi wake wanategemea shughuli za uvuvi na kilimo ili kuendesha maisha yao.

“ni jambo la faraja kwetu sisi wananchi Serikali yetu ya awamu ya sita kutujengea barabara za lami kwenye mitaa yetu,siku za nyuma tulipata shida kubwa kupitia kwenye maeneo haya kwenda kutafuta huduma za kijamii kwenye maeneo mengine”alisema Mbalale.

Aidha Mbalale,amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha zilizowezesha kukamilisha ujenzi wa mradi wa barabara ya Mbambabay- Mbinga yenye urefu wa kilometa 66 kwa kiwango cha lami.

Alisema,kukamilika kwa barabara hiyo kumesaidia kupunguza gharama za maisha na usafiri kwani hapo awali walikuwa wanalipa Sh.15,000 nauli ya kutoka Mbambabay hadi Mbinga lakini kwa sasa wanalipa Sh.9,000 hadi 10,000.

“kabla ya barabara ya lami ya Mbambabay-Mbinga,wilaya yetu ya Nyasa ilikuwa kama kisiwa kila inapofika msimu wa masika,barabara zilijifunga hivyo kuathiri shughuli za usafiri na usafirishaji wa mazao na bidhaa mbalimbali”alisema.

Alisema,Rais Samia Suluhu Hassan na Serikali yake imemaliza kero hiyo,sasa magari yanafika na kuondoka kwenye mji wa Mbambabay muda wowote na wananchi wanafanya shughuli zao za uzalishaji mali.

“awali kila inapofika kipindi cha masika tulikuwa kwenye mateso makubwa sana kwani barabara zote zilijifunga kutokana na ubovu wa barabara,magari pekee yaliyoweza kufika katika wilaya ya Nyasa ni LandRover tu,hali hii ilipelekea tuwe na maisha magumu sana”alisema Mbalale.

Jackob Madondola alisema,miaka ya nyuma kila inapofika msimu wa masika wananchi wa Mji wa Mbambabay walikuwa kwenye mateso makubwa kutokana na nyumba zao kuzingirwa na maji kutokana na kukosekana kwa mitaro ya kutiririsha maji kwenda Ziwa Nyasa.

Alisema,tangu TARURA ilipoboresha miundombinu kwa kujenga barabara za lami na mifereji ya kupitisha maji wananchi wanaishi kwa amani na wanapata muda wa kufanya shughuli za kuwaingizia kipato bila hofu badala ya kubaki nyumbani pindi mvua zinaponyesha ili kuokoa mali zao zisisombwe na maji.

Alitolea mfano katika mlango wa kuingia kituo cha afya Mbambambay, kulikuwa na miundombinu mibovu ya barabara iliyokwamisha kuwahisha wagonjwa hasa akina mama wajawazito na watoto kupata huduma za haraka ili kuokoa maisha yao.

“kwa hiyo uletaji wa fedha katika wilaya yetu umesaidia sana kumaliza kero ya usafiri na usafirishaji kwa kiwango kikubwa na sasa wananchi wanaishi vizuri na kwa amani wakati wote,tunaishukuru Serikali kupitia TARURA kwa kazi nzuri iliyofanya”alisema.

Kaimu meneja wa TARURA Wilaya ya Nyasa Derick Theonest alisema,TARURA inaendelea kufanya jitihada mbalimbali kwa kujenga barabara za lami ili kuboresha mazingira na maisha ya wananchi wa mji wa utalii wa Mbambabay na wilaya ya Nyasa kwa ujumla.

Alisema,hadi sasa wamebakisha kilometa1 ili kukamilisha barabara za lami katika mji wote wa Mbambabay na kuishukuru Serikali kwa kuendelea kuipatia TARURA fedha kwa kujenga miundombinu ikiwemo barabara za lami ambazo zina mchango mkubwa katika kuchochea na kuharakisha maendeleo.

Amewataka wananchi kuhakikisha wanatunza na kulinda miundombinu ya barabara hizo ili ziweze kudumu kwa muda mrefu kwani zinatumia fedha nyingi kuzitekeleza.

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • Mwenyekiti wa Tume huru ya Uchaguzi Tanzania akagua vituo vya kujiandikisha Nyasa.

    May 04, 2025
  • Dc Nyasa awataka madiwani na watendaji kubuni vyanzo vipya vya mapato

    April 30, 2025
  • DC Nyasa azindua Kituo kipya cha Mafuta

    April 26, 2025
  • Wilaya ya Nyasa yaadhimisha miaka 61 ya Muungano kwa Kufanya Usafi

    April 26, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.