• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

Wananchi Nyasa waishukuru Serikali Kwa kufungua Barabara

Posted on: March 17th, 2023

BAADHI ya wananchi wa kata ya Ngumbo wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma wameishukuru serikali kwa kuifungua barabara ya Hinga-Litolomelo na Ngumbo-Litoho zinazounganisha wilaya ya Mbinga na Nyasa na maeneo mengine mkoani humo ambazo awali zilikuwa hazipitiki kirahisi.

Wamesema,kufunguka kwa barabara hizo  katika kipindi cha miaka miwili ya uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kumerahisisha usafiri na usafirishaji wa bidhaa mbalimbali za kilimo na  samaki na kumaliza  kero ya usafiri iliyokuwepo kwa muda mrefu.

Wamesema,changamoto kubwa  kwa wananchi wa kata ya Ngumbo ilikuwa barabara za kuunganisha kata hiyo na maeneo mengine,lakini sasa kero hiyo haipo baada serikali  ya awamu  ya sita  kupitia wakala wa barabara za vijijini na mijini(Tarura) kutoboa na kufanya matengenezo ya  makubwa ya barabara hizo kwa kiwango cha changarawe.

John Mkomola mkazi wa kijiji cha Ngumbo amesema,serikali  ya awamu ya sita imewatendea haki kwa kuboresha huduma za kijamii ikiwemo  barabara zinazokwenda kuchochea na kuharakisha shughuli mbalimbali za kiuchumi.

Alisema,baadhi ya maeneo katika wilaya ya Nyasa hayakuweza kufikiwa na baadhi ya huduma  za kijamii kwa kukosa barabara, hivyo kusababisha maisha ya wananchi kuwa magumu licha ya wilaya hiyo kuwa na rasimilia kubwa ya ardhi na ziwa Nyasa lenye samaki wengi.

Adolat Kapinga mkazi wa kijiji cha Lugali amesema,awali barabara ya Ngumbo-Litoho inayounganisha wilaya ya Nyasa na Mbinga haikuweza kupitika kwa urahisi kutokana na ubovu hasa mashimo makubwa na wakati wa masika kuwa na utelezi na hivyo kusababisha magari kukwama na hata kulala barabarani.

Aidha ameeleza kuwa,katika kipindi cha miaka miwili ya utawala wa Rais Samia barabara hiyo imeimarika na kurahisisha shughuli za kiuchumi kwa wananchi wa wilaya hizo mbili ambao sasa wanatembea kifua mbele na kufaidi matunda ya serikali yao.


Kapinga ameipongeza wakala wa barabara za vijijini na mijini Tarura wilayani Nyasa kufanya matengenezo ya barabara na kurudisha mawasiliano katika maeneo mengi ya wilaya hiyo ambayo hapo awali hayakufikika kwa urahisi.

“miaka miwili ya Rais Dkt Samia  tunaona mabadiliko mengi na makubwa katika wilaya yetu,barabara hii haikuweza kupitika kirahisi, lakini sasa serikali imefanikiwa kuunganisha mawasiliano kati ya wilaya ya Mbinga na Nyasa”amesema Kapinga.

Kwa upande wake meneja wa Tarura wilaya ya Nyasa Thomas Kitusi alisema,barabara ya Hinga-Litolomelo ni moja ya barabara saba zilizotengenezwa kwa fedha za tozo kwa mwaka wa fedha 2022/2023 yenye urefu kilomita 11.7 kwa gharama ya shilingi milioni 174 kwa kiwango cha changarawe.

Kitusi alitaja barabara nyingine ni Ngumbo –Litoho yenye urefu wa km 6.59 ambayo ilitengewa jumla ya shilingi milioni 84 kwa ajili ya kufanya matengenezo kwa kiwango cha chanagarawe.

Alisema,katika kipindi cha miaka miwili ya utawala wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kumekuwa na mabadiliko makubwa kwenye sekta ya barabara ikilinganisha na miaka ya nyuma. na ameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kutenga fedha nyingi ambazo zimewezesha Tarura kufanya matengenezo ya barabara nyingi za vijijini zilizoleta mabadiliko makubwa.


Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • RAIS SAMIA AMWAGA MAMILIONI YA EDHA KUIMARISHA SEKTA YA AFYA NYASA DC

    June 28, 2025
  • RAIS SAMIA AMWAGA MAMILIONI YA EDHA KUIMARISHA SEKTA YA AFYA NYASA DC

    June 28, 2025
  • TAARIFA YA MAENDELEO YA JAMII

    June 26, 2025
  • KICHEKO CHATAWALA TAFRIJA YA KUWAAGA MADIWANI

    June 19, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.