• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

WANANCHI Kata ya Ngumbo na Liwundi Waridhishwa na Utendaji kazi wa Wakala wa Maji RUWASA Nyasa.

Posted on: July 8th, 2022

Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira (RUWASA) Wilaya ya Nyasa, imemtambulisha Mkandarasi atakayejenga Mradi wa maji wenye thamani ya zaidi ya  Tsh,Bilioni 2.5, Utakaotatua tatizo la Maji katika Kata ya Ngumbo na Liwundi, na kufanya makubaliano na Utiaji sahihi wa Miradi ya Maji ya Puulu Songambele, katika Kata ya Kihagara na Malungu Kata ya Tingi Taerehe 08.07.2022.

Ruwasa Nyasa imemtambulisha Mkandarasi NIPO Africa Eng ltd katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Hinga Kata ya Ngumbo tarehe 09.07.2022 na kuhudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Kanali Laban Thomas,Mbunge wa Jimbo la Nyasa Mhandisi Stella Manyanya na Viongozi wa Chama  Na Serikali pamoja na Wananchi.

Lengo la kutambulisha Mradi huo ni kuwataarifu wananchi ili washiriki kikamilifu katika mradi huo na kuwashirikisha kabla ya kuanza mradi.

Akizungumza katika Mkutano huo Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Kanali Laban Thomas, Amemtaka Mkandarasi, kufanya kazi kwa bidi na kuhakikisha mradi huo unatoa maji ya kutosha, naye atafuatilia kwa ukaribu ili wananchi wapate huduma ya maji safi na salama katika Kata ya Ngumbo na Liwundi.

Mbunge wa Jimbo la Nyasa Mhandisi Stella Manyanya, amesema anayafurahia maendeleo yanayofanyika katika Kata za Mwambao hasa katika Sekta ya Maji,amempongeza Wziri wa Maji na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kutatua kero mbalimbali katika Wilaya ya Nyasa.

Ameongeza kuwa kama Mbunge wa Jimbo la Nyasa ataendelea kulipigania Jimbo la Nyasa kwa kuleta maendeleo katika Sekta Mbalimbali na kuwataka wananchi kushiriki kikamilifu shughuli za ujenzi wa Taifa.

Awali akitoa Taarifa ya Mradi Kaimu Meneja wa Ruwasa Wilaya ya Nyasa Mhandisi Jeremi Maduhu amesema Mradi Serikali imetoa Tsh,Bilioni 2.56 kwa ajili ya kutekeleza Mradi huu na unategemea kuwanufaisha wakazi 11,764 wa kata Mbili za Ngumbo na Liwundi,na Vituo 12 vinatarajiwa kujengwa na matank 2 makubwa.

Wananchi wa Kata ya Ngumbo wameipongeza Serikali kwa kutatua changamoto ya Ukosefu wa Maji safi na salama wamekubali kushirikiana na Mkandarasi huyo, ili kujenga miundimbinu na kuhakikisha hakuna Ubadhirifu unafanyika na kuwazawadia RUWASA zawadi ya Mbuzi.

Wakati huohuo Ruwasa wilaya ya Nyasa watiliana sahihi na wakandarasi wa wili watakaotekeleza miradi ya Malungu kata ya Tingi Mradi wenye thamani ya tsh Milioni 471,734,245 ambao utatatua kero ya maji katika Kata Tingi Tarafa ya Mpepo naMkandarasi ni PEACE CONSTRUCTION L.TD.

Mradi mwingine ni Puulu Songambele wenye thamani ya Tsh 819,156,220 utakaotekelezwa bkatika Kata ya Kihagara Wilayani Nyasa na Mkandarasi akiwa ni Palemon Construction L.t.d

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • Jela maisha Kwa Ubakaji

    May 27, 2025
  • Msigwa aipongeza Tamisemi kikao maafisa habari

    May 24, 2025
  • SERIKALI ilivyodhamiria kuboresha Barabara na madaraja

    May 23, 2025
  • Mwenge wa Uhuru wapitia miradi 76 mkoa wa Ruvuma

    May 17, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.