• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

WAKULIMA SONGEA WAGOMEA BEI MNADAWA SOYA,WAINGIZA MILIONI 400 KATIKA UFUTA

Posted on: June 17th, 2020


MNADA wa nane wa mazao ya ufuta na soya ulioshirikisha Halmashauri tano za Mkoa wa Ruvuma na vyama vya msingi vya ushirika 11 umewawezesha wakulima kuuza kilo zaidi ya 264,000 za ufuta na kuwaingizia zaidi ya milioni 400.

Akizungumza mara baada ya kufanyika mnada huo katika soko la mazao la Lilambo,Meneja Operesheni wa Chama Kikuu cha Ushirika wa mazao ya kilimo Songea na Namtumbo (SONAMCU) Zamakanary Komba amezitaja Halmashauri tano zilizoshiriki katika mnada wa zao la ufuta kuwa ni Halmashauri ya Mbinga, Halmashauri ya Songea,Madaba na Nyasa.

Amevitaja vyama 11 vilivyoshiriki katika mnada huo kuwa ni Kingambi,Tingi,Kilumba,Mpiki,Lina,MugisoNalisi,Songea West, Amkeni, Muungano na Tama na kwamba katika kilo za ufuta zilizouzwa katika mnada huo,bei ya juu iliyokubalika na wakulima ilikuwa ni sh.1930 na baada ya kutoa tozo mkulima anauza kwa  sh.1759.

“Pesa ambayo imekwenda moja kwa moja kwa wakulima katika mnada wa leo ni  shilingi milioni 465,250,223,lakini kabla ya makato  kwenda kwa wakulima,fedha ilikuwa ni zaidi ya  milioni  510’’,alisisitiza Komba.

Komba amesema kupitia mnada huo, tozo ya mfuko wa maendeleo katika Halmashauri imepatikana shilingi milioni 7.9 na kwamba ushuru wa Halmashauri  ni zaidi ya sh. Milioni 20.6.

Hata hivyo katika mnada wa zao la soya ambao umeshirikisha Halmashauri mbili   wakulima wamegomea bei ya zao hilo ambayo bei ya juu ilikuwa ni  680 kwa kilo ambapo ukitoa tozo mkulima alikuwa anabakiwa na sh.558.

“Wakulima wa soya wamegomea bei hiyo kwa hiyo tumeusogeza mbele mnada huo hadi Jumatatu ijayo,leo tuliangalia asubuhi bei ya Dar es salaam ilikuwa kilo ni sh.800,Morogoro sh.850 kwa hiyo tunawashauri wenye Kampuni wanunue bei nzuri kutoka kwa wakulima’’,alisisitiza Komba.

Wakulima wa zao la ufuta katika Wilaya za Namtumbo,Songea na Tunduru mkoani Ruvuma wameanza kunufaika na zao hilo baada ya kupokea shilingi bilioni 16.8 tangu kuanza kuuza zao hilo kwa mfumo wa stakabadhi ghalani Apirili 30 mwaka huu

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari wa Mkoa wa Ruvuma

Juni 15,2020

Announcements

  • Tangazo la nafasi za kazi Halmashauri ya wilaya ya Nyasa December 01, 2025
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • TANGAZO la nafasi ya kazi February 03, 2023
  • View All

Latest News

  • Balozi wa Tanzania nchini Malawi atembelea Wilaya ya Nyasa

    December 06, 2025
  • Maonesho ya Nane Nane Kanda za Nyanda za juu kusini , Mguu sawa Kuanza leo

    August 01, 2025
  • UTEKELEZAJI KAMPENI YA CHANJO YA MIFUGO YAANZA NYASA

    July 12, 2025
  • MAKUNDI SOGOZI YA WHATSAAP YAPASWA KUJADILI MAENDELEO

    July 12, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.