• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

Waingereza walivyozamisha meli yaMjerumani bandari ya Liuli mwaka 1914

Posted on: September 4th, 2024

WAINGEREZA WALIVYOIZAMISHA MELI YA WAJERUMANI BANDARI  YA LIULI MWAKA 1914

Na Netho sichali NDC 


Bandari ndogo ya Liuli mwambao wa ziwa Nyasa wilayani Nyasa mkoa wa Ruvuma, inajulikana hasa kutokana hospitali ya Mtakatifu Anna ya kanisa Anglikana inayohudumia wagonjwa wengi katika wilaya   Nyasa.


Katika sekta ya utalii bandari ya Liuli ni eneo lenye utajiri wa vivutio vya utalii wa aina mbalimbali. Jina Liuli lina maana ya 'jiwe lile'. Wakati wa ukoloni wa Kijerumani Liuli iliitwa "SPHINXHAFEN" yaani bandari ya SFINKSI kwa sababu ya kuwepo utajiri wa miamba mikubwa inayofanana na sanamu mashuhuri kwenye Piramidi za giza kama nchini Misri.


Tarehe 13/8/1914 mwanzoni mwa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia Waingereza walishambulia katika eneo la Liuli meli ya pekee ya Wajerumani kwenye ziwa Nyasa ambapo katika Jiwe kubwa la Pomonda lililopo meta 300 ndani ya ziwa Nyasa lilitumika kama maficho ya askari wakati wa vita.


Kwa mujibu wa habari katika gazeti la Times iliyochapishwa mwaka 1914, Uingereza iliwahi kuingia katika vita ya kwanza ya Dunia Agosti 4,1914 na kwamba Siku chache baadaye Nahodha Mwingereza Edmund Rhoades katika kisiwa cha Nkhata Bay nchini Malawi alipokea amri ya kuzamisha meli Hermann von Wissmann iliyokuwa meli  pekee ya Wajerumani kwenye ziwa   Nyasa.


Meli hii ilikuwa chini ya Nahodha wa kijerumani aliyeitwa Berndt ambapo baada ya kupata amri, Rhoades aliendesha meli yake HMS Gwendolyn kuelekea Sphinxhafen (Liuli) kwa sababu alijua meli ilikuwa wapi. Manahodha wote wawili walikuwa marafiki waliowahi kutembeleana mara kwa mara na kukaa pamoja.


HMS Gwendolyn ilipokaribia bandari ya Liuli, Mpiganaji mzinga wa pekee wa meli na mfanyabiashara mmoja Mskoti alikuwa mtu wa pekee mwenye kujua  matumizi ya mzinga hivyo alianza kufyatulia risasi dhidi ya Hermann von Wissmann.


Dakika chache baadaye boti ndogo ilikaribia haraka HMS Gwendolyn. Nahodha Berndt akapanda meli na kumwuliza mwenzake kwa hasira, kwa nini amelewa wakati wa mchana.


Hakujua kuwa vita ilianza tayari katika  bara la Ulaya hivyo  Rhoades  alimtangaza Nahodha wa kijerumani kuwa mfungwa wa vita.


Habari ya ushindi huo ilipelekwa London kwa simu na tarehe 16 Agosti mwaka 1914,gazeti la Times lilichapisha na kutangaza ushindi wa Uingereza katika bandari ya Liuli ziwa Nyasa "Naval victory on Lake Nyasa".


Wakati ule Waingereza waliondoa mzinga mdogo wa meli na vipuli kadhaa ili meli isitumike tena bila kuiharibu. Mwaka 1915 Wajerumani walikuwa wameleta tena vipuli na kutengeneza meli ambapo  Waingereza walirudi Liuli na kuzamisha meli ya Hermann von Wissmann katika bandari ya Liuli.


Baada ya vita meli ilifufuliwa tena na kufanya kazi kwa Waingereza ambapo hadi sasa  maboya yamewekwa katika eneo la Liuli kuonesha mahali  meli hiyo ilipozamishwa.

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • Jela maisha Kwa Ubakaji

    May 27, 2025
  • Msigwa aipongeza Tamisemi kikao maafisa habari

    May 24, 2025
  • SERIKALI ilivyodhamiria kuboresha Barabara na madaraja

    May 23, 2025
  • Mwenge wa Uhuru wapitia miradi 76 mkoa wa Ruvuma

    May 17, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.