• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

WAFANYAKAZI Ruvuma waiomba Serikali kutatua changamoto zinazowakabili.

Posted on: May 1st, 2022

WAFANYAKAZI wa Mkoa wa Ruvuma wameiomba Serikali kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu changamoto zao za kiutumishi.

Ombi hilo llimetolewa katika risala ya watumishi hao iliyosomwa na Mratibu wa Chama cha TUCTA Ashirafu Chussi katika maadhimisho ya Mei Mosi yaliyofanyika kimkoa Wilaya ya Namtumbo.

Risala hiyo imezitaja baadhi ya changamoto zinazowakabili watumishi kuwa ni mishahara ya watumishi bado ni midogo ukilinganisha na gharama za maisha hivyo wameiomba Serikali kuongeza mishahara na kuboresha maslai ya watumishi.

‘’Tunaiomba Serikali kupitia Mei Mosi hii kwa jicho la pekee kabisa iongoze mishahara na kuboresha maslahi kwa wafanyakazi kwa muda mrefu  mishahara haijaongozwa takribani miaka sita sasa’’, imeeleza risala hiyo.

Watumishi hao wamesema kutoongeza mishahara kwa muda mrefu kunashusha morali ya utendaji kazi kwa wafanyakazi na kusababisha kutoa huduma duni kwa jamii.

Kulingana na risala hiyo changamoto nyingine zinazowakabili watumishi wa Mkoa wa Ruvuma ni baadhi ya watumishi kutolipwa madeni kwa wakati na baadhi ya waajiri kutolipa nauli za watumishi na mizigo yao pindi wanapostaafu.

Changamoto nyingine wamezitaja kuwa ni baadhi ya waajiri  kuendelea kufanya kikao kimoja tu cha Baraza la wafanyakazi ili kupitisha bajeti na wengi wao kutolipa stahiki sahihi za wajumbe kwa mujibu wa muongozo kwa mfano 2022 kati ya Halmashauri nane za Mkoa wa Ruvuma ni Halmashauri moja tu ya Manispaa ndio imelipa.

Kwa mujibu wa risala hiyo baadhi ya waajiri kutopeleka michango kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii kwa wakati na kusababisha baadhi ya watumishi kutolipwa stahiki zao za mafao kwa wakati na baadhi ya watumishi kufanyishwa kazi siku za mapumziko bila kulipwa stahiki zao za saa za ziada.

Hata hivyo uwepo muongozo mpya kandamizi wa upandishaji wa madaraja ya mishahara unaotaka mtumishi wa ajira mpya kukaa miaka mitano na miaka minne kwa aliyopo kazini ili kupata sifa ya kupandishwa daraja ni changamoto kubwa kwa wafanyakazi wetu.

Licha ya changamoto hizo wafanyakazi wa Mkoa wa Ruvuma wameahidi  kuendelea kufanya kazi kwa bidii na weledi kwa maslahi mapana ya Nchi yetu na Mkoa huku wakiamini Serikali itachukua hatua kwa wakati kutatua changamoto hizo.

Akijibu risala hiyo mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge ambaye aliwakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Dkt Julius Ningu ameahidi Serikali kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu changamoto hizo.

Hata hivyo RC Ibuge ametoa rai kwa waajiri kuhakikisha wanajitahidi kuzingatia maslahi kwa watumishi na kulipa madeni kwa wakati sanjari na kuandaa nauli za watumishi na mizigo yao kuandaliwa kwa wakati.

‘’Natoa maelekeza kwa waajiri wote kuhakikisha wanazingatia muongozo uliowekwa na Serikali katika kushughulikia stahiki za watumishi na kupeleka michango kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii’’, amesema RC Ibuge.

Kauli mbiu ya maadhimisho ya Mei Mosi 2022 ni mishahara na maslaHi bora kwa wafanyakazi ndio kilio chetu.

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • Karibu Mwenge wa Uhuru Wilayani Nyasa

    May 11, 2025
  • Mwenyekiti wa Tume huru ya Uchaguzi Tanzania akagua vituo vya kujiandikisha Nyasa.

    May 04, 2025
  • Dc Nyasa awataka madiwani na watendaji kubuni vyanzo vipya vya mapato

    April 30, 2025
  • DC Nyasa azindua Kituo kipya cha Mafuta

    April 26, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.