• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

VIKAO VYOTE VYA WAKUU WA IDARA KUFANYIKA ENEO LA UJENZI WA HOSPITALI NYASA

Posted on: May 31st, 2019


Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Nyasa Jimson Mhagama amebadilisha eneo la kufanyia mikutano ya wakuu wa idara inayofanyika Ofisini kwake kila ijumaa na Jumatatu asubuhi na kufanyia eneo la ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Nyasa inayojengwa katika Kijiji cha Nangombo Kata ya Kilosa Wilayani hapa ili kuhakikisha ujenzi huo unakamilika kabla ya juni 30 mwaka huu.

Ameyasema hayo leo wakati akiongea na mwandishi wa habari hizi Ofisini kwake kuhusu maendeleo ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya inayoendelea kujengwa katika Kijiji cha Nangombo.

Mhagama alifafanua kuwa amelazimika kubadili eneo la kufanyia vikao vya wakuu wa Idara Wilayani hapa  kutoka Ofisini kwake  hadi kufanyia eneo la Ujenzi wa Hospitali katika kijiji cha Nangombo kwa lengo la kuongeza ufanisi wa kazi ili kila mkuu wa idara aone kwa macho maendeleo ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya mpaka itakapokamilika yenye lengo la kutatua kero za wananchi wa Wilaya ya Nyasa waliokuwa wakitembeai umbali wa kilomita 66 kufuata Huduma za Matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya mbinga.

Aliongeza kuwa vikao vyote vya wakuu wa idara alivyokuwa akivifanya Ofisini kwake sasa amevihamishia katika eneo la ujenzi na kila mkuu wa idara na Vitengo wanatakiwa kushiriki bila kukosa mpaka juni 30 tutakapokuwa tumeshakamilisha ujenzi huu wa Hospitali ya Wilaya ya Nyasa.

“kuanzia leo vikao vyote vya kiutawala vinavyojumisha Wakuu wa idara na Vitengo vitakuwa vinafanyika katika eneo la Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Nyasa katika Kijiji cha Nangombo kata ya kilosa na kila Mkuu wa idara na Vitengo wanatakiwa kufika bila kukosa wala kuchelewa. Mheshimiwa Rais amezitoa fedha hizi kwa ajili ya kukamilisha ujenzi huu kwa wakati tuna kila sababu ya kusimamia ujenzi huu kwa nguvu zote” alisema Mhagama.

Aidha katika hatua nyingine amempongeza sana Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli kwa kuwajali wananchi wa Wilaya ya Nyasa kwa kuwapa fedha ya kujengea Hospitali ya Wilaya ya Nyasa kwa kuwa walikuwa wakitembea umbali mrefu kufuata huduma za matibabu.

Aidha bwana Jimson Mhagama alitoa wito kwa wananchi wa Wilaya ya Nyasa kutembelea na kuona jinsi ujenzi unavyoendelea na kutoa maoni na ushauri kwa kuwa Hospitali hii ni mali ya wana Nyasa.

Imeandaliwa na 

Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano

Wilaya ya Nyasa.

31/05/2019

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • Jela maisha Kwa Ubakaji

    May 27, 2025
  • Msigwa aipongeza Tamisemi kikao maafisa habari

    May 24, 2025
  • SERIKALI ilivyodhamiria kuboresha Barabara na madaraja

    May 23, 2025
  • Mwenge wa Uhuru wapitia miradi 76 mkoa wa Ruvuma

    May 17, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.