• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

VIJANA 100 WILAYANI NYASA WAPATIWA MAFUNZO YA UZALISHAJI WA MAZAO

Posted on: June 12th, 2019


Jumla ya Vijana 100 kutoka kata zote za Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa, wamepatiwa mafunzo ya siku 12 ya Kujenga kitalu nyumba na miundombinu yake na uzalishaji wa mazao ya Bustani ili waweze kulima eneo dogo na kuvuna mavuno ya kutosha.

Mafunzo hayo yamefanyika hivi karibuni kuanzia mei 20 – 31 mwaka huu katika Kijiji cha Ukuli Kata ya Kingerikiti wilayani Nyasa, na kutolewa na Kampuni ya SUGECO (Umoja wa Wajasiliamali Waliohitimu Chuo Kikuu cha Sokoine – SUA), ikiwa ni Utekelezaji wa Mradi wa Kitalu Nyumba unaogharamiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu (OWM)

Afisa Kilimo wa Kampuni ya SUGECO, na Kiongozi wa timu ya mafunzo Baraka Paul, alisema mafunzo hayo yatawanufaisha wakulima kutengeneza Kitalu nyumba na miundombinu yake ya umwagiliaji na kuweza kuzalisha mazao mengi kwa kwa kutumia sehemu ndogo ya uzalishaji mazao mbalimbali na kumudu umwagiliaji kwa kipindi chote kwa mwaka mzima kwa kuwa miundombinu iliyopo kwenye kitalu hicho ambayo haitegemei mvua.

Aliongeza kuwa wakulima hao wamepewa mafunzo ili wakawafundishe wakulima wengine waliopo katika Kata zao ili waweze kuzalisha mazao mbalimbali ili kuongeza kipato kwa wakulima ikiwa ni kusaidia juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano ya kuhakikisha kuwa wakulima wananufaika na kilimo chao. “Mafunzo haya ni muhimu sana kwa kuwa yatakuwezesha mkulima kujenga Kitalu Nyumba na Miundombinu yake ya umwagiliaji na kukuwezesha kumudu na kutunza kitalu hicho wakati wote kwa kipindi cha mwaka mzima”, alisema Baraka.

Mmoja wa Wahitimu wa mafunzo hayo, Alfred Mapunda, ameipongeza Serikali kwa kuwapa mafunzo hayo na kuahidi kuyatumia vema mafunzo hayo kwa yeye binafsi na kwa Kata yake ya Kingerikiti kwa kuwafundisha wakulima wengine ili wanufaike na kilimo hicho cha kitalu nyumba.

Naye Joyce Mtundu ambaye ni mhitimu wa mafunzo hayo alisema mafunzo hayo yamemsaidia sana kwa kuwa alikuwa akilima tu kilimo cha mazoea ambacho kilikuwa kinampa mavuno kidogo.

Afisa kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa, Rashidi A. Rashidi, aliwapongeza wakulima hao kwa kuhudhuria mafunzo hayo ya siku sita na kuwataka kuwa Mabalozi wazuri kwa wakulima wengine kwa kutumia mafunzo waliyo yapata na kuisaidia jamii kwa kuwa Halmashauri ya Nyasa ilikuwa ikihitaji mafunzo hayo kwa muda mrefu hivyo wahitimu wajione kuwa wamebahatika kupata mafunzo hayo ya kitalu nyumba.

IMEANDALIWA NA

KITENGO CHA TEHAMA

WILAYA YA NYASA

12/06/2019

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • Jela maisha Kwa Ubakaji

    May 27, 2025
  • Msigwa aipongeza Tamisemi kikao maafisa habari

    May 24, 2025
  • SERIKALI ilivyodhamiria kuboresha Barabara na madaraja

    May 23, 2025
  • Mwenge wa Uhuru wapitia miradi 76 mkoa wa Ruvuma

    May 17, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.