• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

Usafiri wa meli ziwa Nyasa unavyofungua fursa za uwekezaji Ruvuma

Posted on: April 4th, 2023

Pichani ni meli ya MV Mbeya II ikiwa imetia nanga katika bandari ya Mbambabay wilayani Nyasa

SERIKALI imenunua meli tatu zinazotoa huduma za abiria na mizigo katika mikoa ya Ruvuma,Mbeya na Njombe kupitia ziwa Nyasa.

 Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) inahudumia jumla ya bandari 15 katika ziwa Nyasa ambapo katika Mkoa wa Ruvuma,TPA inahudumia bandari sita ambazo  ni  Mbambabay,Liuli,Njambe,Lundu,Mkili na Ndumbi,katika Mkoa wa Njombe TPA pia inahudumia bandari sita ambazo ni  Lumbila, Ifungu, Nsisi, Makonde,Lupingu na Manda na  katika Mkoa wa Mbeya TPA inahudumia bandari tatu ambazo ni Itungi,Kiwira na Matema.

Baadhi ya bandari TPA imeweka miundombinu ya kisasa,pia kuna bandari ambazo zinaendelea kuwekwa miundombinu kwa ajili ya utoaji huduma bora na za kisasa.

Kila bandari inahitaji kuwa na magati,maghala,yadi za kutunzia mitambo na mizigo na uwepo wa nyumba za kuishi wafanyakazi,sanjari na kuweka mifumo ya  zimamoto,majisafi,maji taka na mifumo ya TEHAMA ili kufanyakazi kwa ufanisi na tija kulingana na maelekezo ya serikali.

Ili kuboresha huduma katika bandari zote za ziwa Nyasa,TPA inatekeleza mpango kabambe unaoanza mwaka 2021/2022 na unaotarajia kukamilika katika kipindi cha mwaka 2028/2029.

Mpango huo kabambe utaongeza shehena ya mizigo katika ziwa Nyasa kutoka tani zaidi ya 11,000 hadi kufikia shehena ya mizigo zaidi ya tani 100,000,lengo hili linachochewa na mipango mizuri ya serikali ikiwemo kukamilika kwa ujenzi wa barabara ya lami toka Mbinga hadi Mbambabay.

kutokana na kukamilika kwa lami ya Mbinga hadi Mbambabay na kuanza kutoa huduma za meli katika ziwa Nyasa kunafufua uchumi wa mji wa Mbambabay wilaya ya Nyasa  hivyo kuunganisha Tanzania kupitia ushoroba wa Mtwara na nchi za Malawi,Msumbiji , Zimbabwe na Zambia.

Hakuna ubishi Mji wa Mbambabay utafufuka kwa kasi kutokana na kukamilika kwa mtandao wa barabara ya lami kutoka Mbinga hadi Mbambabay na serikali kununua meli tatu mpya  kati ya hizo meli mbili za MV Njombe na MV Ruvuma ni za mizigo na meli moja ya MV Mbeya II ni ya abiria.

Kulingana na TPA meli zote tatu zimegharimu zaidi ya shilingi bilioni 20.1  ambazo zimetolewa na serikali kujenga meli kwa kutumia  kampuni ya Songoro Marine inayomilikiwa na Mtanzania.

Meli mbili za mizigo MV Njombe na MV Ruvuma kila moja ina uwezo wa kubeba tani 1000 na kwamba kila meli imegharimu shilingi bilioni 5.5 na meli ya abiria ya MV Mbeya II ina uwezo wa kubeba abiria 300 na mizigo tani 200, imegharimu shilingi bilioni 9.1.

Kwa mujibu wa taarifa ya TPA meli ya abiria ya MV Mbeya II  imerithi jina la meli ya MV Mbeya I iliyozama eneo la Makonde ziwa Nyasa mwaka 1977.

Hata hivyo  meli ya MV Mbeya II baada ya kujengwa iliingizwa majini Septemba 2019

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas anasema  wilaya ya Nyasa sasa imefunguka kutokana na kukamilika kwa ujenzi wa barabara ya lami toka Mbinga hadi Mbambabay na kuanza rasmi kwa huduma za meli tatu ndani ya ziwa Nyasa.

Amesema huduma za meli zinaimarishaji bandari katika ziwa Nyasa na kuchochea shughuli za kiuchumi hususani biashara na uwekezaji  na sekta ya utalii.

Mkuu wa Mkoa  anatoa rai kwa watanzania waliopo ndani na nje ya nchi kufika kuwekeza katika wilaya ya Nyasa  ambayo miundombinu yake imeboreshwa ikiwemo barabara ya lami,umeme na usafiri wa majini.

Mhandisi Stella Manyanya ni Mbunge wa Jimbo la Nyasa anasema kuboreshwa kwa barabara na uwepo wa meli mpya kutaongeza idadi ya wageni wanaotembelea wilaya Nyasa ambayo ni kitovu cha utalii katika Mkoa wa Ruvuma.

Imeandikwa na Netho Sichali wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wilaya ya Nyasa

Aprili 4,2023


Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • Karibu Mwenge wa Uhuru Wilayani Nyasa

    May 11, 2025
  • Mwenyekiti wa Tume huru ya Uchaguzi Tanzania akagua vituo vya kujiandikisha Nyasa.

    May 04, 2025
  • Dc Nyasa awataka madiwani na watendaji kubuni vyanzo vipya vya mapato

    April 30, 2025
  • DC Nyasa azindua Kituo kipya cha Mafuta

    April 26, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.