• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

URASIMISHAJI WA MAKAZI YA WANANCHI WASHIKA KASI NYASA

Posted on: November 12th, 2020

Halmashauri ya wilaya ya Nyasa imeanza zoezi la Urasimishaji wa makazi holela  ili wananchi waweze kumilikishwa kwa  kupatiwa hati miliki ya Viwanja vyao.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Nyasa Bw Jimson Mhagama , wakati akiongea na Mwandishi wa Habari hizi Ofisini kwake leo, wakati akiongelea zoezi la Urasimishaji ambalo linaendelea katika Kijiji cha Likwilu Kata ya Kilosa Wilayani hapa.

Bw Mhagama amefafanua kuwa, Lengo la Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa ni  kupima maeneo yote Wilayani hapa lakini kwa sasa wataalamu wa upimaji wa ardhi , wanaendelea na Upimaji anaofanyika katika Kijiji cha Likwilu, na Lengo ni kupima Viwanja 1500.

Ameongeza kuwa Upimaji huu ni shirikishi ambao unawashirikisha kikamilifu wananchi,  na tayari Mkutano wa hadhara ulishafanyika wa kuwajengea uelewa wananchi juu ya Upimaji wa Maeneo yao, na wananchi wanachangia Tsh 50,000 tu kiasi ambacho ni rafiki kwa wananchi wetu wa Wilaya ya Nyasa.

“Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa tayari imeanza Zoezi la urasimishaji Makazi ya Wananzhi wetu na zoezi limeanza katika kijiji cha Likwilu Kata ya Kilosa na Tunatarajia Zoezi hili lifanyike Halmashauri nzima ili Wananchi wetu waweze kupata faida nyingi za Urasimishaji wa Makazi yao”

Amezitaja faida za Urasimishaji kuwa ni Kutatua Migogoro ya Ardhi, kupata hati Miliki ambazo zitawasaidia kuweka rehani katika Taasisi za Kifedha, kupangwa kwa eneo kimipango miji, Kufikiwa na Huduma muhimu kwa Urahisi kama Umeme,maji na  barabara.

Aidha ametoa wito kwa wananchi wa Wilaya ya Nyasa kushirikiana na wataalamu wa mipango miji wilayani hapa, kuhakikisha wanapima maeneo yao ili waweze kupata maendeleo na kuishi katika eneo ambalo limepimwa na lenye Miundombinu ya kutosha.

Kwa upande  wao wananchi wa kijiji cha Likwilu wakiongelea upimaji huo wamesema wanaipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa, kwa Kuanza zoezi la Urasimishaji wa makazi yao kwa kuwa awali walikuwa wanaishi kwenye makazi holela ambayo ilikuwa haina miundombinu kama barabara, maji, umeme hali iliyokuwa inawalazimu hata kuuza kwa bei rahisi na kukosa dhamana wanapokuwa na uhitaji wa kukopa Benki.

Mara baada ya Upimaji wanategemea kuuza kwa bei ya juu Viwanja vyao na maeneo yatapanda thamani kubwa,” Kwa kweli tunaipongeza sana Halmashauri ya Nyasa kwa Kurasimisha makazi yetu ,tumepatiwa elimu ya kutosha katika mikutano ya Hadhara na wananchi wamepokea elimu hii vizuri na wamefarijika sana hasa kwa fedha ambayo tutachangia ambayo ni sh 50,000 ambayo wananchi wote wanaouwezo wa kuchangia “ alisema Bwana  Omary Mkachaga ambaye ni mkazi wa kijiji cha Likwilu.

Ameiomba Serikali kuhakikisha mpango huu unawafikia wananchi wote wa Wilaya ya Nyasa kwa kuwa unalengo la kutatua changamoto iliyowakumba wananchi hao kwa muda mrefu kwa kuwa walikuwa hawajui kama kiwango cha kupima kimepungua mpaka kufikia elfu hamsini kwa Kiwanja kimoja. Kwa kuwa awali walishindwa kutokana na bei kubwa ya kupimia kiwanja kimoja kuwa juu.

Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa habari hizi umebaini wananchi wengi wameufurahia mpango huu na washirikiana na wataalamu kikamilifu na kuhamasishana wao kwa wao ili kutekeleza mpango huu wa urasimishaji.


Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • Jela maisha Kwa Ubakaji

    May 27, 2025
  • Msigwa aipongeza Tamisemi kikao maafisa habari

    May 24, 2025
  • SERIKALI ilivyodhamiria kuboresha Barabara na madaraja

    May 23, 2025
  • Mwenge wa Uhuru wapitia miradi 76 mkoa wa Ruvuma

    May 17, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.