• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

TAMASHA LA UTALII NYASA NI LA KIPEKEE

Posted on: December 21st, 2020


Mkuu wa wa Wilaya ya Nyasa Isabela Chilumba mbaye amemwakilisha Mkuu wa Mkoa Ruvuma, amewataka wawekezaji wa Utalii , kuwekeza Wilaya ya Nyasa kwa kuwa Wilaya ya Nyasa ina Vivutio Vingi vya Utalii ambavyo, ni Vya kipekee ambavyo Vinapatikana Wilaya ya Nyasa pekee .

Ameyasema hayo jana, Akiwa Mgeni rasmi wakati akihutubia wananchi na wageni Mbalimbali , katika Kilele cha  Tamasha la Utalii 2020, lililofanyika katika Viwanja vya fisheries, Mbamba bay Wilayani Nyasa.

Mkuu huyo alifafanua kuwa Wilaya ya Nyasa ni Wilaya, ya  kipekee katika Mkoa wa Ruvuma, ambayo ukishindanisha na Wilaya zingine za Mkoa wa Ruvuma, ina Vivutio vingi vizuri vinavyowavutia wageni wengi, hasa Ziwa Nyasa na Fukwe zake za Asili ambazo zimeifanya Wilaya, hii kuwa ni ya kipekee, na kuwataka wawekezaji kuja kuwekeza Wilaya ya Nyasa.

Aliongeza kuwa Wilaya ya Nyasa pia ina miundombinu rafiki, ya kuwavutia watalii na Wawekezaji ukizingatia kuwa Barabara ya Mbinga hadi Mbamba bay, Tayari imekamilika na Hospitali ya Wilaya ya Nyasa imeanza Kazi na kutoa huduma kwa,  wananchi na kuwawafanya hata watalii na wawekezaji hata wakiumwa watatibiwa na kupata huduma bora za kiafya.

Aidha kwa upande wa usafiri wa Maji, amewatangazia wananchi kuwa Usafiri wa Meli ya Kisasa ya Mizigo ya Mv Mbeya 11 inaanza rasmi kazi na jumanne wiki hii itatia Nanga katika Bandari ya Mbamba bay, na Meli ya Mv Njombe nayo inafanya kazi.

Aidha amempongeza Rais John Pombe Magufuli kwa Juhudi zake za kuiboresha Wilaya ya Nyasa, hasa kwa miundombinu Wilaya ya Nyasa, na sasa Hakika ni Wilaya ya Kitalii.

“Nichukue Fursa hii kumpongeza sana Mh Rais, kwa Juhudi zake alizozifanya hasa kwa upande wa miundombinu, ametujengea barabara ya Lami na kwa kwa sasa inapitika mwa haraka na muda wote tofauti na ilivyokuwa mwanzo. Upande wa Usafiri wa majini Meli kubwa mbili zinafanya kazi na Mv Mbeya imeanza kazi rasmi na Jumanne itawasili Mbamba bay hivyo, Mbamba bay imefunguka nawakaribisha sana wawekezaji”.

Kwa Upande wake  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Ambaye pia ni Kamishna wa Uhifadhi Tanzania National parks TANAPA, Mh. Allan Kijazi amewapongeza wananchi wa Wilaya ya Nyasa kwa kuandaa Tamasha la Utalii kwa miaka mine mfululizo, na kuwashauri kuwa wanatakiwa kuwa na Siku maalum na  Tarehe maalumu ya kutangaza Vivutio vyot, na Wizara ya Maliasili na Utalii imeyapokea maombi ya kuchangia na kuandaa Tamasha lenye Hadhi ya Kimataifa.

Naye Mbunge Wa Jimbo la Nyasa Mhandisi Stella Manyanya, ameliomba Shirika la Utangazaji Tanzania TBC, kupitia Safari Channel Kuja kutengeneza makala na Vipindi mbalimbali vya Vivutio vya Wilaya ya Nyasa, ambavyo ni vya aina yake kwa kuwa vivutio vingi vya wanyama watanzania wanavifahamu sasa ni zamu ya kutangaza Ziwa Nyasa na Fukwe zake.

Tamasha hili limepambwa na Ngoma za Asili za Chioda, Muhambo na Lingoga, mashindano ya kuogelea, kupiga kasia na Utalii wa Kisiwa Cha Lundo pamoja na Utali wa Nyama choma.


Announcements

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI WILAYA YA NYASA April 18, 2023
  • Tangazo la kujiunga na jeshi la kujenga Taifa, (JKT) August 29, 2023
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • Wilaya ya Nyasa yaadhimisha sikukuu ya Uhuru Kwa kufanya Kongamano

    December 09, 2023
  • Dc Nyasa, na Mbunge Manyanya, waongoza Usafi wa mazingira Hospitali ya Wilaya ya Nyasa.

    December 08, 2023
  • Wilaya ya Nyasa inaadhimisha juma la uhuru wa Tanzania bara kwa kufanya shughuli mbalimbali

    December 07, 2023
  • Nyasa kuadhimisha Siku ya Ukimwi Duniani Kwa kupima V. V.U na kutoa Elimu ya ukatili wa kijinsia

    November 30, 2023
  • View All

Video

HAFLA YA UTIAJI SAINI MRADI WA UJENZI NA USANIFU BANDARI YA MBAMBA BAY
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.