• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

TAARIFA YA MAENDELEO YA JAMII

Posted on: June 26th, 2025

TAARIFA YA DIVISHENI YA MAENDELEO YA JAMII WILAYA YA NYASA KUHUSU MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA TAREHE 16 JUNI, 2025.

 

UTANGULIZI 

Mnamo Mwaka 1990, uliokuwa Umoja wa Nchi Huru za Kiafrika (OAU) ulipitisha Azimio la nchi 51 wanachama wa Umoja huo, kukumbuka watoto wa kitongoji cha Soweto kilichopo Afrika ya Kusini ambao waliuawa kinyama na iliyokuwa Serikali ya Makaburu ya nchi hiyo tarehe 16 Juni, 1976. Watoto hao Wakiafrika walikuwa wakidai haki ya kutobaguliwa kwa msingi wa Rangi pamoja na haki nyingine za kibinadamu.

 

MADHUMUNI: 

Pamoja na kukumbuka mauaji hayo ya kinyama, madhumuni mengine ya kuadhimisha siku hii ni kuwa na fursa ya kusisitiza wajibu wa Serikali za Afrika kwa Watoto; kuziwezesha Serikali hizo kuandaa na kutekeleza mipango ya taifa ya kuwaendeleza Watoto na kuinua kiwango cha uelewa na ufahamu wa matatizo yanayowakabili Watoto wa Afrika.

Tanzania ikiwa ni nchi mojawapo mwanachama wa Umoja wa Afrika, imekuwa ikishiriki kikamilifu katika kuadhimisha siku hii kwa miaka ishirini na moja (21) mfululizo, tangu mwaka 1991.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania imekuwa ikitumia siku hii kutafakari kwa kina matatizo yanayowakabili Watoto na vile vile kutafuta namna ya kuyapatia ufumbuzi matatizo hayo. Serikali inapata pia wakati mzuri wa kutangaza sera, programu na mipango mbalimbali inayohusu masuala ya Watoto na kuhamasisha jamii kuchangia kuondoa matatizo ya Watoto nchini.

Kwa upande mwingine, maadhimisho haya ni sehemu ya utekelezaji wa sera na sheria zetu zinazohusu kuwaendeleza Watoto, ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa mikataba mbalimbali ya Kimataifa inayohusu haki na Ustawi wa Watoto.

KAULI MBIU: 

Kaulimbiu ya mwaka 2025 inasema “MAENDELEO ENDELEVU 2030: IMARISHA ULINZI NA FURSA SAWA KWA WATOTO.” Lengo mahususi la maadhimisho haya ni kuona nini kifanyike katika kutoa haki za msingi za Mtoto. Ni ukweli usiopingika kuwa kauli mbiu hii ina lengo la kukuza na kuthamini utu wa Mtoto katika nyanja zote za Kijamii, Kisiasa, Kiuchumi na Kiutamaduni.

Ndugu mgeni rasmi; Halmashauri ya wilaya ya Nyasa kupitia kitengo cha Ustawi wa jamii imefanikiwa kushughulikia matatizo mbalimbali ya watoto yanayohusu ukatili na unyanyasaji wa Watoto kama ifatavyo;                                          

TAKWIMU ZINAZOONYESHA VITENDO VYA UKATILI DHIDI YA WATOTO WILAYA YA NYASA KWA KIPINDI CHA JULAI 2024 HADI JUNE 2025.

NAMBA
AINA YA KOSA
IDADI YA KOSA
HALI KESI
ADHABU 
1
ULAWITI
 01
HUKUMU IMESHATOLEWA
KIFUNGO CHA MAISHA JELA PAMOJA FAINI YA 2,000,000/=
2
UBAKAJI
05
KESI MOJA  IMESHATOLEWA HUKUMU NA ZINGINE NNE BADO ZIPO MAHAKAMANI
KIFUNGO CHA MAISHA JELA PAMOJA NA FAINI YA 2,000,000/=

JUMLA YA  MAKOSA
06


                Chanzo cha takwimu ni Ofisi ya Ustawi wa jamii Wilaya.

Adha, Halmashauri ya wilaya ya Nyasa kupitia Divisheni ya Maendeleo ya Jamii katika Dawati la Msaada wa Kisheria imefanikiwa kutoa elimu dhidi ya Ukatili wa Kijinsia kwa wanafunzi wa shule 30 zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa, lengo la kutoa elimu hizo ni kumlinda Mtoto dhidi ya Ukatili na Unyanyasaji unaofanywa na jamii dhidi ya Watoto, ili kuimarisha ulinzi na fursa sawa kwa Watoto.

Aidha, Halmashauri ya wilaya ya Nyasa kupitia divisheni ya Elimu Msingi na Sekondari zimefanikiwa kusajili wanafunzi wapya kwa mwaka huu 2025 kama ifuatavyo;

 TAKWIMU ZA UANDIKISHAJI WANAFUNZI WA DARASA LA AWALI KATIKA SHULE ZA MSINGI WILAYA YA NYASA JANUARI 2025.

MALENGO YA UANDIKISHAJI
UANDIKISHAJI HALISI
WAV
WAS
JUMLA
WAV
WAS
JUMLA
%
2951
2790
5741
2952
2791
5743
99.9%

                Chanzo cha takwimu ni Idara ya Elimu Msingi Wilaya.

TAKWIMU ZA UANDIKISHAJI WANAFUNZI WA DARASA LA KWANZA KATIKA SHULE ZA MSINGI WILAYA YA NYASA JANUARI 2025.

MALENGO YA UANDIKISHAJI
UANDIKISHAJI HALISI
 
WAV
WAS
JUMLA
WAV
WAS
JUMLA
%
2840
2815
5655
2842
2815
5657
99.9%








                Chanzo cha takwimu ni Idara ya Elimu Msingi Wilaya.

TAKWIMU ZA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA KATIKA SHULE ZA MSINGI WILAYA YA NYASA JANUARI 2025.

WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA
WANAFUNZI WALIORIPOTI SHULE.
 
WAV
WAS
JUMLA
WAV
WAS
JUMLA
%
1405
1618
3023
1186
1431
2617
87%








                Chanzo cha takwimu ni Idara ya Elimu Sekondari Wilaya.

  Halmashauri ya wilaya ya Nyasa kwa kushirikana  na wadau wa shirika la PADI kwa ufadhili wa Social Action Trust Fund (SATF), linatekeleza mradi uitwao SATF-MVC care and support program” unaojishughulisha na kusaidia watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi. Shirika limefanikiwa kununua vifaa vya shule na sare kama (kaptura, sketi, shati, suruali, soksi, sweta, daftari, vitabu vya kujifunzia na viatu) kwa wanafunzi wa 93 wasekondari na wanafunzi 13 wa shule ya Msingi. Lakini pia wamegawa lishe (maziwa, uga wa lishe, sukari, pamoja na fedha ya matunda na mboga za majani) kwa watoto wanaoishi na VVU na pamoja na taulo za kike. Ugawaji huu umefanyika katika kata 07 amabazo ni kata ya Kilosa, Mbamba bay, Lumeme, Tingi, Mpepo, Lituhi na Liuli.

MWISHO: 

Ni matarajio ya Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa kuwa kila mmoja wetu atatoa ushirikiano wa hali ya juu katika kuhamasisha jamii yetu juu ya umuhimu wa siku hii pamoja na maudhui yake. 

Mwisho, ninapenda kuchukua tena fursa hii kuwakumbusha Watanzania wote na viongozi wetu hapa nchini kuwa tuna wajibu wa kuhakikisha kuwa Watoto wote wanapewa haki zao za msingi pasipo kujali Rangi, Dini,Jinsi, Ulemavu na hata Kabila.

Nawatakia kila la kheri katika kufanikisha maadhimisho haya.

 

WATOTO NI TAIFA LA LEO NA KESHO.

SHANEL M. MBUNDA

KAIMU AFISA MAENDELEO YA JAMII WILAYA

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • RAIS SAMIA AMWAGA MAMILIONI YA EDHA KUIMARISHA SEKTA YA AFYA NYASA DC

    June 28, 2025
  • RAIS SAMIA AMWAGA MAMILIONI YA EDHA KUIMARISHA SEKTA YA AFYA NYASA DC

    June 28, 2025
  • TAARIFA YA MAENDELEO YA JAMII

    June 26, 2025
  • KICHEKO CHATAWALA TAFRIJA YA KUWAAGA MADIWANI

    June 19, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.