• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

Simba adimu auawa Kijiji Cha Mitomoni Nyasa

Posted on: April 16th, 2025

SIMBA ADIMU DUNIANI AANGAMIA LIPARAMBA

Katika kijiji kidogo cha Mipotopoto, pembezoni mwa Pori la Akiba la Liparamba wilayani Nyasa mkoani Ruvuma, simulizi ya nadra na ya kusikitisha imetokea simba mwenye rangi ya kahawia na nyeupe, kiumbe adimu anayepatikana katika maeneo machache duniani, ameuawa baada ya kuingia kwenye makazi ya watu na kusababisha taharuki kubwa.

Kwa muda mrefu, wakazi wa kijiji hicho wameishi kwa amani, wakifahamu kuwa hifadhi ya Liparamba ni jirani yao, lakini si hatari kwao. Lakini siku nne zilizopita, hali hiyo ilibadilika ghafla.

Diwani wa Kata ya Mipotopoto Mheshimiwa Said Mahamud, anasimulia tukio la mwananchi mmoja aliyenusurika kifo baada ya kukutana uso kwa uso na simba huyo porini.

 “Alikuwa njiani kutoka shambani, alipokutana na simba huyo. Aliweza kujiokoa kwa kupanda mti na kutumia matawi kujilinda, kabla ya simba huyo kuondoka,” anasema Mahamud.

Lakini kama tukio hilo halikutosha kuibua hofu, usiku wa kuamkia Aprili 15, simba huyo alifanya kile kinachoonekana kama shambulizi la kipekee, alipanda paa la nyumba, akashika mbwa, kubomoa dirisha, na hata kuchukua nguo kabla ya kutoweka gizani.

Kulingana na Diwani huyo Usiku uliofuata, simba huyo akaingia zizini na kuua kondoo watano na mbuzi mmoja wa mwananchi Said Njete.

Kilichofuata ni hatua ya haraka ya Serikali kupitia askari wa wanyamapori wa Pori la Akiba Liparamba waliowasili kutoka Mbinga.Baada ya ufuatiliaji, waliweza kumuua simba huyo na kuchukua ngozi yake.

Kwa mujibu wa diwani huyo, simba huyo alikuwa ni dume mwenye rangi ya kahawia na nyeupe,maelezo yanayowiana na tabia ya simba weupe adimu duniani wanaopatikana tu katika Pori la Akiba la Liparamba.

 Inasemekana kuwa simba huyo alikuwa dhaifu na mwenye dalili za ugonjwa, jambo ambalo huenda lilimfanya kuvuka mipaka ya pori na kuingia kwenye makazi ya binadamu.

“Kwa miaka mingi hatujawahi kushuhudia simba wakiingia hadi nyumbani kwa watu. Hili ni tukio la kwanza la aina yake,” alisema Mheshimiwa Mahamud.

Wananchi wa Mipotopoto wameipongeza Serikali kwa hatua ya haraka iliyochukuliwa, wakisema kuwa simba huyo angeweza kuleta maafa makubwa iwapo asingedhibitiwa.

Askari wa wanyamapori wamewataka wananchi kutoa taarifa mapema kila wanapoona wanyama hatari ili kuzuia majanga makubwa.

Pori la Liparamba, ambalo linapakana na nchi ya Msumbiji, ni moja ya hazina za kipekee za taifa, likiwa na mandhari ya kuvutia na wanyama adimu kama tembo na simba weupe wa ajabu, pori hili linatajwa kuwa na uwezo wa kugeuka kuwa moja ya vivutio vikuu vya utalii wa kipekee barani Afrika.

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • Jela maisha Kwa Ubakaji

    May 27, 2025
  • Msigwa aipongeza Tamisemi kikao maafisa habari

    May 24, 2025
  • SERIKALI ilivyodhamiria kuboresha Barabara na madaraja

    May 23, 2025
  • Mwenge wa Uhuru wapitia miradi 76 mkoa wa Ruvuma

    May 17, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.