• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

SERIKALI KUMALIZA KERO YA MAJI NYASA..

Posted on: October 25th, 2018

WAZIRI wa maji Profesa Makame Mbarawa amesema Serikali itahakikisha miradi yote ya maji vijijini na mijini inakamilika kwa wakati ili kuwaondolea kero ya maji Safi na Salama wananchi  ili waweze kufanya kazi kwa bidii za kujiletea maendeleo.

Aliyasema hayo jana (24/10/2018) alipofanya ziara ya siku mbili ya kukagua miradi ya maji katika  katika kijiji cha Ukuli Kata ya kingerikiti na kata ya Tingi.

Profesa Mbarawa alifafanua kuwa aliamua kufanya ziara ya kukagua miradi hiyo ya maji ili aione kwa macho na siyo kusubiri kuletewa kwa maandishi ili azijue  changamoto gani zilizopo katika miradi hiyo ili aweze kuitatua na kuhakikisha Wananchi wanapata maji safi na Salama ikiwa ndilo lengo kuu la Serikali.

Aliongeza kuwa kwa muda mrefu alisikia kuna tatizo la maji katika kata ya Tingi na Kingerikiti hivyo akaamua aje aone,na kutolea ufafanuzi wa kuwa katika mradi wa Ukuli  kuna tatizo la kupasuka kwa viungio vya kwenye bomba kutokana na bomba kupita kwenye miteremko mikali ikitokea kijiji cha burma na kuvuka hadi kijiji cha Ukuli na akasema ameona na ameliona tatizo ambalo atatuma wataalam kutoka Wizara yake ili waweze kutatua tatizo hilo na maji yaweze kutoka na wananchi wafurahie huduma ya maji safi na salama  kwa kuwa  serikali ilishatoa tsh 1,129,433,944.00.kwa ajili ya kutekeleza mradi wa Ukuli-Kingerikiti.

“nimefanya ziara ya siku mbili kuja katika kijiji hiki kwa lengo la kutatua tatizo lilopo katika eneo hili badala ya kukaa ofisini na kusubiri kuletewa tatizo kwa maandishi lakini leo nimefurahi nimekagua na niko huku kwenye hii miteremko ambayo nimefanikiwa kuona tatizo lililopo na nitatuma wataalam kuja kurekebisha bomba viungio hivi ambavyo vinapasuka tujue tatizo kubwa ni nini kwa kutumia fedha kidogo na kwa haraka tuweze kutatua tatizo lililopo na hatimaye wanachi waweze kupata maji safi na salama kwa kuwa mapendekezo niliyopata awali ni kupitisha mabomba haya sehemu nyingine”

Wakazi wa kijiji cha Ukuli kata yakingerikiti wakiongelea tatizo la maji katika kijiji hicho wanatumia umbali mrefu wa kilomita tatu hadi tano kutafuta huduma  ya maji hivyo serikali ikifaulu kukamilisha mradi huo itakuwa imewapunguzia kero nzito ya upatikanaji wa maji katika eneo hilo.

Awali akitoa taarifa ya kero ya maji katika eneo hilo kwa Waziri wa maji  kwa niaba ya wananchi wa kata ya Kingerikiti Diwani wa kata ya Kingerikiti Alto Komba ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa alisema Tatizo hilo ni kubwa linalowafanya wananchi kutembea umbali mrefu kutafuta huduma ya maji safi na salama.

Aidha alitumia fursa hiyo kuziagiza Halmashauri Nchini  kusimamia vizuri miradi ya maji kuanzia kutangaza zabuni na kuwateua wakandarasi wenye sifa na uwezo wa kifedha ili waweze kukamilisha miradi kwa wakati na kutanguliza maslahi ya wananchi bila kujali maslahi yao binafsi.

Katika kijiji cha Tingi alikagua mradi wa maji wenye thamani ya tsh 361,233,107/= na kuwataka wananchi kuwa na subira wakati mradi huo unakamilishwa na kuwaahidi Serikali itahakikisha inachukua hatua ya kuwaleta wataalam na kuongeza chanzo kingine cha maji ili upatikanaji wa maji safi na salama uwe asilimia 85 kwa vijijini na mjini iwe aslimia 90 ifikapo mwaka 2020.

Aidha Waziri Mbarawa alitoa wito kwa jamii ya watanzania kuvilinda na kuvitunza vyanzo vya maji kwa kuacha kulima kwenye vyanzo vya maji na kuacha kukata miti hovyo ili maliasili iliyopo kwenye vyanzo vya maji viendelee kutoa maji kwa wakazi wa maeneo yote nchini.

Miradi hiyo ya maji itahudumia watu 6286 kwa kata ya kingerikiti na watu 7326 kwa kata ya tingi kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012.

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • Jela maisha Kwa Ubakaji

    May 27, 2025
  • Msigwa aipongeza Tamisemi kikao maafisa habari

    May 24, 2025
  • SERIKALI ilivyodhamiria kuboresha Barabara na madaraja

    May 23, 2025
  • Mwenge wa Uhuru wapitia miradi 76 mkoa wa Ruvuma

    May 17, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.