• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

Serikali kujenga Miradi 3 ya TSH Bilion 6.4 Nyasa

Posted on: December 3rd, 2024

Mhe. Peres Magiri na Mhe Stella Manyanya Washuhudia Utiaji Saini Mikakati ya Miradi ya Maji Wilaya ya Nyasa


Mkuu wa Wilaya ya Nyasa, Mheshimiwa Peres Magili, pamoja na Mbunge wa Jimbo la Nyasa, Mheshimiwa Stella Manyanya, washuhudia zoezi la utiaji saini mikataba ya miradi mikubwa ya maji inayotekelezwa katika wilaya hiyo. Miradi hii inatarajiwa kufanywa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA), ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali kuboresha huduma za maji vijijini.


Mikataba hiyo imesainiwa na Kaimu Meneja wa RUWASA Mkoa wa Ruvuma, Mhandisi Bartholomew Matwiga, na wakandarasi wa miradi mbalimbali ya maji katika wilaya ya Nyasa. Wakandarasi waliosaini mikataba ni: Rj Mussa Construction, kwa mradi wa Maji wa Nangombo-Kilosa; Consel Construction Ltd, kwa mradi wa Maji wa Mbanga; na Namis Corporate Construction kwa mradi wa Maji wa Ndengele.


Akizungumza katika hafla hiyo, Mheshimiwa Magiri aliwaasa wakandarasi kuhakikisha wanakamilisha miradi hiyo kwa wakati na kulingana na masharti ya mikataba. Alisisitiza kuwa, jamii ya wilaya ya Nyasa inahitaji huduma ya maji kwa haraka, na Serikali ina dhamira ya kufikia lengo la kutoa huduma ya maji kwa asilimia 85 ya wananchi vijijini.


Meneja wa RUWASA Wilaya ya Nyasa, Mhandisi Masoud Samila, alieleza takwimu za wananchi watakaonufaika na miradi hiyo, pamoja na gharama za jumla za miradi. Alisema mradi wa Maji Nangombo-Kilosa, wenye gharama ya shilingi bilioni 3.7, utawanufaisha wananchi wapatao 13,500 kutoka vijiji vya Nangombo, Kilosa, Luhekei, na Likwilu.

Mradi wa Maji wa Ndengele/Mbuyula, wenye gharama ya shilingi bilioni 1.8, utawanufaisha wananchi 10,072 wa vijiji vya Ndengele na Mbuyula.

 Mradi wa Maji wa Mbanga, wenye gharama ya shilingi milioni 900,000, utawanufaisha wananchi 4,900 wa vijiji vya Mbanga na Kigongo.


Baada ya kusainiwa kwa mikataba hiyo mitatu, yenye gharama jumla ya shilingi bilioni 6.4, Mheshimiwa Mbunge wa Nyasa, Eng. Stella Manyanya, alimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa dhamira yake ya dhati ya kumtua Mama Ndoo kichwani. Alisema kuwa, kwa mara Kwa mara wilaya ya Nyasa imepokea fedha za ujenzi wa miradi ya maji zikiwa mabilioni kwa bilioni.


Aidha, Mheshimiwa Manyanya alishukuru Wizara ya Maji, chini ya uongozi wa Mheshimiwa Jumaa H. Aweso, Naibu Waziri Mheshimiwa Eng. Kundo A. Mathew, pamoja na Katibu Mkuu, Eng. Mwajuma Waziri, kwa usimamizi na ufuatiliaji mzuri wa miradi ya maji. Mbunge huyo pia alishukuru RUWASA Makao Makuu, Mkoa na Wilaya kwa kusimamia miradi hiyo kwa ufanisi na viwango vya juu kama ilivyobainishwa kwenye mikataba.

Mheshimiwa Manyanya alisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa pamoja kati ya Serikali, wakandarasi, na wananchi ili kuhakikisha miradi hii inatekelezwa kwa ufanisi, na kwamba huduma ya maji inapatikana kwa wananchi wa Nyasa kwa haraka na kwa ubora wa hali ya juu.

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • Jela maisha Kwa Ubakaji

    May 27, 2025
  • Msigwa aipongeza Tamisemi kikao maafisa habari

    May 24, 2025
  • SERIKALI ilivyodhamiria kuboresha Barabara na madaraja

    May 23, 2025
  • Mwenge wa Uhuru wapitia miradi 76 mkoa wa Ruvuma

    May 17, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.