• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

SERIKALI ilivyodhamiria kuboresha Barabara na madaraja

Posted on: May 23rd, 2025

SERIKALI ILIVYODHAMIRIA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA NA MADARAJA

SERIKALI kupitia Wakala wa Barabara (TANROADS) inaendelea na juhudi za kuboresha miundombinu ya barabara na madaraja mkoani Ruvuma.

Lengo kuu ni kurahisisha usafiri na usafirishaji wa bidhaa, hivyo kuchochea uchumi na kupunguza umaskini.


TANROADS Mkoa wa Ruvuma inasimamia mtandao wa barabara wa kilomita 2,166.62, zikiwemo barabara kuu na barabara za mkoa.


BAJETI NA UTEKELEZAJI WA MIRADI


Meneja wa TANROADS Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Salehe Juma Mkwama anasema Katika kutekeleza majukumu yake, TANROADS inasimamia miradi mikubwa ya maendeleo, miradi midogo ya maendeleo, pamoja na matengenezo ya barabara na madaraja.


Miradi hii inatekelezwa kwa bajeti inayosimamiwa kupitia Makao Makuu ya TANROADS kwa kushirikiana na serikali na wadau wa maendeleo.


MIRADI MIKUBWA YA MAENDELEO


 UJENZI WA BARABARA YA MBINGA – MBAMBA BAY


Barabara hii ya kilomita 66 ilijengwa na kampuni ya China Henan International Cooperation Group Co. Ltd (CHICO) kwa gharama ya Tsh. 129.36 bilioni. Mradi huu ulizinduliwa tarehe 24 Septemba 2024 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. Samia Suluhu Hassan.


 UJENZI WA DARAJA LA RUHUHU


Daraja  la Ruhuhu lililopo katika Mto Ruhuhu unaomwaga maji yake ziwa Nyasa\, lina urefu wa mita 98.01 linaunganisha Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma na Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe. Ujenzi  wa daraja hilo ulikamilika tarehe 15 Oktoba 2021 kwa gharama ya Tsh. 8.976 bilioni.


UKARABATI WA UWANJA WA NDEGE SONGEA


Ukarabati wa uwanja huu ulianza Aprili 2019 na kukamilika Machi 2023 kwa gharama ya Tsh. 37.09 bilioni. Mradi huu ulikuwa kwenye kipindi cha uangalizi hadi Septemba 2024.


UJENZI WA BARABARA YA KITAI - LITUHI - NDUMBI


Mradi huu wa kilomita 95.3 unatekelezwa kwa awamu tatu kwa kiwango cha lami:


• Kitai – Amani Makoro (Km 5): Ulianza Juni 2019 na kukamilika Agosti 2020 kwa Tsh. 6.957 bilioni.


• Amani Makoro – Ruanda (Km 35): Ujenzi ulianza Juni 2022 na unatarajiwa kukamilika Aprili 2024 kwa Tsh. 60.481 bilioni.


• Ruanda – Lituhi – Ndumbi (Km 50): Ujenzi unaendelea kwa Tsh. 95.76 bilioni na unatarajiwa kukamilika Juni 2026.


 UJENZI WA BARABARA YA LIKUYUFUSI – MKENDA


Barabara hii ya kilomita 124 ipo kwenye hatua za mwisho za kusainiwa kwa mkataba wa ujenzi. Fidia ya Tsh. 5.19 bilioni imeshatathminiwa na kusubiri malipo kutoka Wizara ya Fedha.


 UJENZI WA BARABARA YA LUMECHA–LONDO-MALINYI – LUPIRO


Mradi wa ujenzi wa barabara hii ya kilomita 512 inaunganisha

mikoa ya Ruvuma na Morogoro.


 Serikali imesaini mkataba na kampuni ya China Civil Engineering ConstructionCorporation Ltd (CCECC) kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huu


kwa sasa utatekelezwa kwa Mfumo wa Sanifu na jenga ('Design and Build')  ambao ni ujenzi wa barabara ya Lumecha - Londo - Malinyi - Lupiro


UJENZI WA BARABARA YA SONGEA – LUTUKIRA NA MCHEPUKO WA SONGEA


Mradi huu wa kilomita 116 unafadhiliwa na Benki ya Dunia. Ujenzi unatarajiwa kuanza wakati wowote baada ya kukamilika kwa mchakato wa zabuni.


MIRADI YA MADARAJA


DARAJA LA MITOMONI


Daraja lenye urefu wa mita 47.7 linaunganisha Wilaya za Nyasa na Songea Vijijini.


Mradi huu utatekelezwa kwa miezi 15 kwa gharama ya Tsh. 9.29 bilioni kwa ufadhili wa Serikali na Benki ya Dunia.


DARAJA LA MKILI


Daraja hili linafanana na la Mitomoni na linajengwa kwa Tsh. 3.19 bilioni kwa muda wa miezi 15.


DARAJA LA MKENDA


Daraja hili linaunganisha Tanzania na Msumbiji kupitia Mto Ruvuma. Zabuni yake ilitangazwa lakini ilihitajika kutangazwa upya baada ya mzabuni mmoja tu kujitokeza.


USANIFU WA BARABARA NA MADARAJA


Mbali na miradi inayoendelea, TANROADS inaendelea na usanifu wa barabara na madaraja muhimu kama:


• Barabara ya Mbamba Bay – Lituhi (Km 112.4)


• Barabara ya Mtwarapachani – Nalasi – Tunduru (Km 300)


• Barabara ya Madaba – Mundindi – Liganga – Mkiu (Km 46)


MATENGENEZO YA BARABARA NA HIFADHI YA BARABARA


Katika kuhakikisha barabara zinapitika muda wote, TANROADS mkoa wa Ruvuma imetenga Tsh. 17.9 bilioni kwa ajili ya matengenezo ya barabara za muda maalumu na sehemu korofi.


Aidha, jitihada za kuhifadhi hifadhi ya barabara zinaendelea kwa kuweka vigingi na kutoa notisi kwa wavamizi.


Juhudi za serikali kupitia TANROADS mkoa wa Ruvuma zinaendelea kuleta maendeleo kwa kuboresha miundombinu ya barabara na madaraja.

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • Jela maisha Kwa Ubakaji

    May 27, 2025
  • Msigwa aipongeza Tamisemi kikao maafisa habari

    May 24, 2025
  • SERIKALI ilivyodhamiria kuboresha Barabara na madaraja

    May 23, 2025
  • Mwenge wa Uhuru wapitia miradi 76 mkoa wa Ruvuma

    May 17, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.