• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

Ruwasa Nyasa yatambulisha mradi wa Maji Nangombo, kutatua Kero ya Maji Mji wa Mbamba bay

Posted on: January 28th, 2025

Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Wilaya ya Nyasa tarehe hivi karibuni, imetambulisha mradi mkubwa wa maji wenye thamani ya zaidi ya  Tsh Bilioni 3.7 utakaotatua kero ya  maji safi na Salama katika Kata 2 za Kilosa na Mbamba bay Wilayani Nyasa.

Mradi huo  umetambulishwa katika mkutano ya Hadhara wenye lengo la kuwashirikisha  wananchi, ili waweze kushirikiana na Mkandarasi atakayetekeleza Mradi, Mkutano  iliyofanyika katika Kata ya Ofisi ya Mtendaji wa Kijiji Cha Nangombo Kata ya Kilosa  na kuhudhuriwa na wananchi na Viongozi wa Chama na Serikali.

Akizungumza katika Mkutano, Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Mh.Peres Magiri, amemtaka Mkandarasi anayetekeleza Mradi, kuhakikisha anajenga mradi kwa ubora, na kwa wakati na kuhakikisha maji yanatoka, na kuwa Mradi endelevu kwa kuwa Serikali inalengo la kutatua kero ya maji, hivyo fedha za Serikali ziendane na thamani halisi ya Mradi. Pia amewataka wananchi kutoa ushirikiano katika Mradi na kulinda na kutunza Vyanzo vya maji.

“Ninakutaka Mkandarasi utakayetekeleza Mradi huu kuhakikisha kuwa unajenga kwa ubora na maji yanatoka, na kuwa mradi endelevu  kwa kuwa Serikali inalenga  kutatua kero ya maji, hivyo fedha za Serikali ziendane na thamani halisi ya Mradi,na wananchi naomba tushiriki kikamilifu Ujenzi wa mradi huu Kwa kuwa ni wetu na unalengo la kutatua kero ya maji katika mji wetu wa Mbamba bay Kwa kuwa tulikuwa na miradi midogo midogo”

Awali akitoa Taarifa ya Miradi hiyo  Meneja wa RUWASA Wilayani Nyasa mhandisi Masoud Samila,amemtambulisha Mkandarasi Mzawa RJ MUSSA CONSTRUCTION  LTD kutoka Dodoma ndie atakayetekeleza mradi huu na amesema,wamejipanga kimkakati kusimamia na  kutekeleza miradi hiyo ili iweze kutatua  changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi.Aidha amesema Mradi unatarajia kukamilika januari 23, 2026

Ameongeza Mradi huu unalenga kuhudumia wananchi wapatao 13,323 na amevitaja  vijiji vitakavyonufaika na mradi  huu ni Nangombo, Likwilu, Ruhekei, kilosa na Mbamba bay na manufa ya mradi huu ni kupunguza magojwa ya mlipuko kwa jamii na kuimarika kwa huduma ya Maji safi na salama na jamii kupata muda wa kufanya shughuli za maendeleo.

Ameongeza kuwa shughuli zitakazofanyika ni Ujenzi wa Tego la maji,ujenzi wa Tanki lenye ujazo wa Lita milioni Moja(1,000,000), ununuzi wa Bomba,ulazaji wa bomba kuu km 2.73 ulazaji wa mabomba na usambazaji km 40.6 ujenzi wa vituo 10 vya kuchotea  maji na Miradi hiyo itatekelezwa kwa kipindi cha miezi sita na unatarajia kukamilika January 2026.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Nyasa Mhandisi Stella Manyanya amesema Serikali inaendelea kutatua changamoto za wananchi hivyo wananchi washiriki kikamilifu kutekeleza mradi huu.

Wananchi wa Kata Hizo wameipongeza Serikali kwa, kutatua changamoto ya maji katika kata zao kwa kuwa awali walikuwa na Miradi ambayo ilijengwa zamani na miundombinu yake ilikuwa imechakaa, hivyo wamempongeza Mbunge wa Jimbo la Nyasa Mhandisi Stella Manyanya na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan.

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • Mwenyekiti wa Tume huru ya Uchaguzi Tanzania akagua vituo vya kujiandikisha Nyasa.

    May 04, 2025
  • Dc Nyasa awataka madiwani na watendaji kubuni vyanzo vipya vya mapato

    April 30, 2025
  • DC Nyasa azindua Kituo kipya cha Mafuta

    April 26, 2025
  • Wilaya ya Nyasa yaadhimisha miaka 61 ya Muungano kwa Kufanya Usafi

    April 26, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.