• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

RUWASA Nyasa yatambulisha Miradi Mikubwa 2, Wananchi Waipongeza Serikali

Posted on: April 16th, 2022

Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Wilaya ya Nyasa tarehe 14.04.2022, imetambulisha miradi mikubwa 2 yenye thamani ya zaidi ya  Tsh Bilioni 11.3 itakayotatua Upatikanaji wa maji safi na Salama katika Kata 4 za Lituhi, Mbaha, Liuli na Kihagara Wilayani hapa.

Miradi hiyo  imetambulishwa katika mikutano ya Hadhara yenye lengo la kuwashirikisha  wananchi, ili waweze kushirikiana na Mkandarasi atakayetekeleza Mradi, na Mkutano  iliyofanyika katika Kata ya Lituhi na Liuli na kuhudhuririwa na wananchi na Viongozi wa Chama na Serikali.

Akizungumza katika Mikutano, Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Kanali Laban Thomas, amemtaka Mkandarasi anayetekeleza Mradi, kuhakikisha anajenga mradi kwa ubora na kwa wakati na kuhakikisha maji yanatoka, na kuwa Mradi endelevu kwa kuwa Serikali inalengo la kutatua kero ya maji, hivyo fedha za Serikali ziendane na thamani halisi ya Mradi. Pia amewataka wananchi kutoa ushirikiano katika Mradi na kulinda na kutunza Vyanzo vya maji.

“Ninakutaka Mkandarasi utakayetekeleza Mradi huu kuhakikisha kuwa unajenga kwa ubora na maji yanatoka, na kuwa mradi endelevu  kwa kuwa Serikali inalenga  kutatua kero ya maji, hivyo fedha za Serikali ziendane na thamani halisi ya Mradi nitakuja kukagua. Pia ninawataka wananchi kutoa ushirikiano wa ujenzi wa Mradi huu na kulinda na kutunza vyanzo vya maji”.

Awali akitoa Taarifa ya Miradi hiyo Kaimu Meneja wa RUWASA Wilayani Nyasa Jeremiah Maduhu amemtambulisha Mkandarasi Emirates Builders co.ltd, na amesema,wamejipanga kimkakati kusimamia na  kutekeleza miradi hiyo ili iweze kutatua  changamoto ya upatikanaji wa maji safi kwa wananchi.

Amevitaja vijiji vitakavyonufaika na mradi  katika Kata ya Lituhi ni Lituhi,Kihuru,Nkaya, na Mwela mpya na Katika Kata ya Mbaha ni Mbaha,Ndumbi na Liweta na Katika Mradi Mwingine wa Liuli Vijiji  vitakavyonufaika ni Nkalachi,Hongi Mkali A na Mkali B.

Ameongeza kuwa shughuli zitakazofanyika ni Ujenzi wa vyanzo vyanzo vya maji,ukarabati wa Matanki na Ujenzi wa Matenki mapya,ununuzi wa Bomba, ujenzi wa vituo vya kuchotea  maji na Miradi hiyo itatekelezwa kwa kipindi cha miezi sita kuanzia.Ametoa wito kwa wananchi kushirikiana na Mkandarasi anayetekeleza mradi huu kwa kuwa anaanza mara moja baada ya kutambulishwa.

Wananchi wa Kata Hizo wameipongeza Serikali kwa, kutatua changamoto ya maji kitika kata zao kwa kuwa awali walikuwa na Miradi ambayo ilijengwa zamani na miundombinu yake ilikuwa imechakaa, hivyo wamempongeza Mbunge wa Jimbo la Nyasa Mhandisi Stella Manyanya na Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Nyasa Ndugu Jimson Mhagama kwa kutatua Changamoto mbalimbali katika Wilaya ya Nyasa.

Announcements

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI WILAYA YA NYASA April 18, 2023
  • Tangazo la kujiunga na jeshi la kujenga Taifa, (JKT) August 29, 2023
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • Nyasa kuadhimisha Siku ya Ukimwi Duniani Kwa kupima V. V.U na kutoa Elimu ya ukatili wa kijinsia

    November 30, 2023
  • Dc Nyasa-Wasiopeleka watoto shule wajiandae kufungwa

    November 25, 2023
  • Timu ya wataalam kutoka Ofisi ya mkuu wa Mkoa Ruvuma yakagua miradi ya Maendeleo, yampongeza Ded Nyasa USimamizi miradi

    November 18, 2023
  • Mkurugenzi Mtendaji wilaya ya Nyasa awataka watumishi wa afya kutoa huduma Bora Kwa wananchi

    November 16, 2023
  • View All

Video

JENGO JIPYA LA UTAWALA NYASADC
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.