• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

RC RUVUMA.VITUO VYOTE VYA AFYA VIFUNGWE MFUMO WA GOTHOMIS

Posted on: June 11th, 2021

MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge  ametoa miezi mitatu kwa wakuu wa wilaya na wakurugenzi kuhakikisha kuwa vituo vyote vya kutolea huduma za afya kwa umma vinafungwa mifumo ya kukusanya mapato (GOTHOMIS).Brigedia Jenerali Ibuge ametoa agizo hilo wakati anafungua kikoa cha mfumo wa ugavi wa bidhaa za afya kwa viongozi wa serikali kutoka Halmashauri na wilaya zote za Mkoa wa Ruvuma ambacho kimefanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea.Mkuu wa Mkoa ametoa agizo hilo kutokana na vituo vingi vya serikali kukosa mifumo ya kukusanya mapato (GOTHOMIS) ambapo takwimu zinaonesha kuwa kati ya vituo 280 vya kutolea huduma za afya vilivyopo mkoani Ruvuma,ni vituo kumi tu ndivyo vimefungwa mifumo hiyo.“Kufikia Septemba Mosi,2021,vituo vyote vya kutolea huduma za afya kwa umma,viwe vimefungwa mifumo ya GOTHOMIS bila kukosa,Septemba 2,2021,niwe nimepata taarifa ya utekelezaji na baada ya hapo,ukaguzi wa kushitukiza utaendelea na kuchukua hatua’’,amesisitiza RC Ibuge.Mkuu wa Mkoa pia amewaagiza wakuu wa Wilaya na wakurugenzi katika Halmashauri zote,kuhakikisha mapato na matumizi ya vyanzo vyote katika Halmashauri yanajadiliwa kwenye vikao vya kisheria na amekitaja moja ya kigezo kitakachotumika kuangalia ufanisi wa ukusanyaji mapato katika Mkoa wa Ruvuma katika mwaka wa fedha wa 2021/2022 ni lazima kufikia zaidi ya asilimia 80 ya mapato ya vyanzo vya sekta ya afya.RC Ibuge ameziagiza Halmashauri zote kuhakikisha vituo vya kutolea huduma za afya kwa umma vinatuma kila mwezi kwa wakati madai ya huduma iliyotolewa kwa wanachama wa Mfuko wa Afya Jamii ulioboreshwa(iCHF) na Mfuko waTaifa wa Bima ya Afya(NHIF).Kutokana na asilimia ndogo ya wananchi waliojiunga na (iCHF) mkoani Ruvuma,RC Ibuge ameziagiza Halmashauri zote kufanya uhamasishaji mkubwa wa jamii kujiunga na mfuko huo ambapo hadi sasa Mkoa umeandikisha kaya zilizohai 11,820 sawa na asilimia 3.3 wakati lengo ni kufikia kaya 180,085 sawa na asilimia 50.Mganga Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dr.Jairy Kanga ameahidi kutekeleza maagizo yote yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa,ikiwemo kuongeza ukusanyaji mapato kupitia mfumo wa GOTHOMIS  na kuongeza uhamasishaji kwa jamii kujiunga na (iCHF).Dr.Kanga amesema mfuko wa iCHF mkoani Ruvuma ulianza kutekelezwa mwaka 2019,ambapo kitaifa Mkoa ulishika nafasi ya mwisho ambapo hivi sasa Mkoa umepanda hadi kufikia nafasi ya 11 kitaifa na kwamba kikao kazi hicho kitaongeza ufanisi na tija.

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • UTEKELEZAJI KAMPENI YA CHANJO YA MIFUGO YAANZA NYASA

    July 12, 2025
  • MAKUNDI SOGOZI YA WHATSAAP YAPASWA KUJADILI MAENDELEO

    July 12, 2025
  • DC MAGIRI AZINDUA RASMI BODI YA MAJI WILAYA YA NYASA

    July 12, 2025
  • DKT.SAMIA AMWAGA TENA MAMILIONI YA MIRADI NYASA

    July 10, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.