• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

RC. MNDEME. SERIKALI INATAMBUA NA KUTHAMINI MCHANGO WANAWAKE KATIKA JAMII

Posted on: March 10th, 2021

SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatambua na kuthamini mchango mkubwa unaotolewa na wanawake katika ujenzi wa Taifa.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme katika maadhimisho ya kilele ya siku ya wanawake Duniani  Mkoani Ruvuma yaliyofanyika katika kijiji cha Kalanje wilayani Tunduru.

Mndeme amesema kutokana na serikali kutambua umuhimu wa wanawake imeziagiza Halmashauri zote kutenga asilimia nne ya mapato yake ya ndani kwa lengo kuwawezesha wanawake kiuchumi.

Amesema katika kipindi cha kuanzia Julai 2020 hadi Februari 2021 katika Mkoa wa Ruvuma,serikali imetoa mikopo yenye thamani ya shilingi 444,167,441.82 kwa vikundi 603 vya wanawake,vikundi 221 vya vijana na vikundi 203 vya watu wenye ulemavu.

“Mh.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anatekeleza kauli mbiu hii ya Wanawake katika uongozi chachu kufikia dunia yenye usawa hivyo kwa vitendo, tunaona wakuu wa Mikoa/Mawaziri,wakuu wa Wilaya,Wakurugenzi na wakuu wa Idara ambao ni wanawake ni jukumu letu kuwapa wanawake nafasi ya uongozi”,alisisitiza Mndeme.

 Mndeme ameitaja siku ya wanawake kuwa ni muhimu sana kwa sababu  inaonesha nafasi kubwa waliyonayo wanawake katika jamii yetu na katika uongozi na kutoa mchango mkubwa wa malezi ya watoto.

Amesema wanawake ni nguzo kubwa katika nchi kwa sababu wanatoa dira na mwelekeo wa maendeleo katika ngazi zote za kifamilia hadi uongozi wa juu ya nchi.

Awali Afisa maendeleo ya Jamii wa Mkoa wa Ruvuma Zawadi Nyoni akitoa historia fupi ya siku ya wanawake duniani amesema ilianzishwa mwaka 1900 kufuatia maandamano ya wanawake wafanyakazi wa sekta ya viwanda nchini Marekani kupinga mazingira duni ya kazi.

Nyoni amesema wanawake walipinga ukosefu wa huduma za kijamii na kuwepo kwa vitendo vya unyanyasaji katika ajira ikiwemo wanawake kulipwa mshahara mdogo kwa kazi sawa ukilinganisha na wanaume.

Hata hivyo amewapongeza wanawake wa Mkoa wa Ruvuma kwa kuwa mstari wa mbele katika Nyanja za kuleta maendeleo endelevu kwa Jamii ikiwemo kushiriki na kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.

Amesema wanawake wamekuwa mstari wa mbele kulaani vitendo vya kikatili dhidi ya wanawake na watoto hususani wa kike,kupinga matumizi ya dawa za kulevya,na kupambana na janga la UKIMWI na magonjwa ya mlipuko kwa kutumia elimu kwa jamii kwa njia ya sanaa.

kauli mbiu ya siku ya wanawake duniani mwaka huu ni  Wanawake katika uongozi chachu ya kufikia dunia yenye usawa

Announcements

  • Tangazo la nafasi za kazi Halmashauri ya wilaya ya Nyasa December 01, 2025
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • TANGAZO la nafasi ya kazi February 03, 2023
  • View All

Latest News

  • Balozi wa Tanzania nchini Malawi atembelea Wilaya ya Nyasa

    December 06, 2025
  • Maonesho ya Nane Nane Kanda za Nyanda za juu kusini , Mguu sawa Kuanza leo

    August 01, 2025
  • UTEKELEZAJI KAMPENI YA CHANJO YA MIFUGO YAANZA NYASA

    July 12, 2025
  • MAKUNDI SOGOZI YA WHATSAAP YAPASWA KUJADILI MAENDELEO

    July 12, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.