• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

RC. Ibuge awaagiza Watendaji wasisubiri Migogoro isiwakute ofisini

Posted on: July 14th, 2021

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge amewaagiza maafisa wa ardhi kutatua migogoro ya ardhi kwa kuwatembelea wananchi katika maeneo yao badala ya kusubiri migogoro hiyo kuwakuta maofisini.

RC Ibuge ametoa maagizo hayo  wakati anazungumza katika kikao kazi cha watumishi wa sekta ya ardhi mkoani Ruvuma ambacho kimeshirikisha watendaji mbalimbali wakiwemo wakuu wa Wilaya,wakurugenzi wa Halmashauri,makatibu Tawala wa wilaya na watumishi wengine ngazi ya wilaya na Mkoa kilichofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea.

Maelekezo mengine ambayo ameyatoa RC Ibuge kwa maafisa ardhi ni kuhakikisha wanafanyakazi kwa weledi na kwa kuzingatia maadili ya kazi,kutojiuhusisha kuomba na kupokea rushwa na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu sheria mbalimbali za ardhi.

“Ikumbukwe kuwa baadhi ya migogoro ya ardhi hutokea kutokana na wananchi kutofahamu sheria za ardhi,kwa hiyo kinachohitajika hapa ni uelewa wa sheria ili wananchi kuzifahamu’’,alisisitiza Ibuge.

Brigedia Jenerali Ibuge pia ameagiza kuendelea na ukamilishaji wa kazi zote za urasimishaji wa makazi holela katika Halmashauri zote za Mkoa wa Ruvuma na kwamba kipaumbele kiwa katika  Halmashauri ya Manispaa ya Songea ambapo zoezi hilo linafanyika kwa kasi ndogo ukilinganisha na wingi wa maeneo yaliyojengwa kiholela.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa  ametoa rai kwa wananchi ambao maeneo yao yamechukuliwa kwa ajili ya uwekezaji na yanahitaji fidia kuendelea kuwa watulivu wakati serikali inatafuta fedha kwa ajili ya fidia.Maeneo yanayohitaji fidia yaliyopo Manispaa ya Songea ni Bonde la Mto Ruhila,eneo la EPZA Kata ya Mwengemshindo na barabara ya  By Pass ya Mtwara Corridor.

Katika kikao kazi hicho RC Ibuge amewaagiza wanasheria wa Halmashauri zote kwa kushirikiana na maafisa Ardhi na TAKUKURU  kutoa elimu ya namna bora ya kufany usuluhisho wa migogoro ya ardhi kwa wajumbe wa Mabaraza ya Ardhi ya Kata kwa sababu wameonekana kuwa sehemu ya kikwazo katika kutenda haki kwa wananchi.

Akizungumza kwenye kikao hicho,Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololet Mgema ameshauri ili kutatua changamoto za ardhi,bajeti ya kupima ardhi iongezwe ili eneo kubwa la ardhi lipimwe kuepusha migogoro ambayo inatokana na maeneo mengi kutopimwa.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma

Julai 13,2021

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • Jela maisha Kwa Ubakaji

    May 27, 2025
  • Msigwa aipongeza Tamisemi kikao maafisa habari

    May 24, 2025
  • SERIKALI ilivyodhamiria kuboresha Barabara na madaraja

    May 23, 2025
  • Mwenge wa Uhuru wapitia miradi 76 mkoa wa Ruvuma

    May 17, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.