• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

PlanRep Iliyoboreshwa (Web-based Planrep) itaondoa changamoto kwa watumiaji.

Posted on: July 24th, 2017

  Mfumo mpya wa kuandaa Mipango na bajeti za Mamlaka za Serikali za Mitaa (PlanRep) ulioboreshwa umetajwa kuwa muarobaini wa changamoto nyingi za mfumo wa utoaji wa huduma kwa wananchi. Mfumo huu ambao unatarajiwa kuanza kutumika Oktoba 2017 umekuwa ukifanyiwa majaribio ambayo yameonesha tija.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya matumizi ya mfumo huo kwa watendaji wa serikali yaliyofanyika katika ukumbi wa NAF Apartment ulioko mjini Mtwara leo, Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara Elias Nyabusani aliyekuwa akimuwakilisha Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara ALfed Luanda amesema Mfumo huu umekuja kama mkombozi kutokana na kutatua changamoto nyingi ambazo serikali imekuwa ikikutana nazo.

Amesema mfumo huu mpya utawawezesha wananchi kupanga mipango na bajeti kulingana kituo au mtoa huduma husika tofauti na mfumo unaotumika sasa ambao vipaumbele na mipango ya Bajeti inaishia ngazi ya Halmashauri.

Ameitaja changamoto nyingine iliyokuwepo kabla ya matumizi ya mifumo ya kielektolini kuwa serikali ilikuwa inaingia gharama kubwa kugharamia posho za Maafisa katika kufuatilia taarifa kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Amesema licha ya kupoteza gharama kubwa pia serikali ilikuwa ikipoteza muda na hivyo kupunguza ufanisi wa kazi.

Amesema kupitia mfumo huu mpya suala hilo halitakuwepo na badala yake mtumiaji anaweza kutumia kompyuta yake au simu ya mkononi kupata taarifa na kutoa mrejesho kwa haraka zaidi.

Nyabusani amewataka washiriki kuhakikisha wanatumia fursa hiyo kuonesha utendaji kazi uliotukuka. Pia amewashukuru waandaaji wa mafunzo hayo ambao ni Shirika la maendeleo la watu wa Marekani (USAID) kupitia program yao maalumu ya PS3 ambao wamekuwa wakifanya kazi kwa karibu zaidi na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za MItaa (TAMISEMI). Amesema yako mambo mengi ambayo yamefanywa na PS3 ambayo watanzania wote wanapaswa kushukuru.

Kwa upande wake Mkuu wa timu ya Rasilimali Fedha ya PS3 Gemin Mtei amesema PlanRep iliyoboreshwa inakuja kuboresha uwazi na uwajibikaji ambapo watoa huduma katika ngazi ya Halmashauri au mkoa wataweza kupata mrejesho wa kazi zao kwa urahisi zaidi kutokana na ukweli kuwa mtumiaji amepewa nafasi ya kufungua taarifa katika eneo lolote kwa kutumia Kompyuta au simu ya mkononi (Tablet).

Mafunzo ya siku Nane ya Mfumo mpya wa kuandaa mipango na bajeti za Mamlaka za Serikali za Mitaa (PlanRep) ulioboreshwa yamefunguliwa katika ukumbi wa NAF apartment yakiwahusisha Maafisa Mipango, Wahasibu, Maafisa TEHAMA, Makatibu wa Afya na Waganga Wakuu kutoka Halmshauri na Mikoa. Mikoa iliyoshiriki katika kituo cha Mtwara ni Mtwara, Ruvuma, Lindi na Dar es Salaam

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • UTEKELEZAJI KAMPENI YA CHANJO YA MIFUGO YAANZA NYASA

    July 12, 2025
  • MAKUNDI SOGOZI YA WHATSAAP YAPASWA KUJADILI MAENDELEO

    July 12, 2025
  • DC MAGIRI AZINDUA RASMI BODI YA MAJI WILAYA YA NYASA

    July 12, 2025
  • DKT.SAMIA AMWAGA TENA MAMILIONI YA MIRADI NYASA

    July 10, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.