• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

OFISI UA WAZIRI MKUU, FAO YAWAPONGEZA MAAFISA HABARI MKOA WA RUVUMA

Posted on: October 10th, 2020

MAAFISA wa Habari wa Mkoa wa Ruvuma wamepongezwa na Ofisi ya Waziri Mkuu  na Shirika la  Chakula na Kilimo  Duniani(FAO)  kwa kuwataarifa wananchi kwa kusahihi  mafunzo ya utayari wa kukabiliana na magonjwa ya mlipuko yaliofanyika kwa siku tano katika hoteli ya Tiffany Diamond mjini Mtwara.

Akizungumza wakati wa ufungaji mafunzo hayo ambayo yalishirikisha  timu za dharura za kukabili magonjwa kutoka mikoa hatarishi ya Ruvuma na Mtwara,Valentina Sanga wa Idara ya Maafa Dawati la Afya Moja Ofisi ya Waziri Mkuu,amesema wanahabari hao licha ya kushiriki katika mafunzo hayo pia wamekuwa wanatimiza kazi ya kuhabarisha umma kwa siku zote za mafunzo kupitia vyombo mbalimbali vya habari

Ametoa rai kwa wanahabari wengine nchini kuiga mfano wa wanahabari hao ambao pia katika mafunzo hayo katika mtihani wa mwisho wa kujipima wamefanya vizuri na kupewa vyeti vya kuhitimu mafunzo hayo.

Sanga amelishukuru Shirika la FAO kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu kufanikisha  mafunzo hayo  na kuwapongeza wakufunzi wote kutoka Chuo cha SUA,Wizara ya Afya na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kufanikisha mafunzo hayo ambayo yamesaidia kuelewa dhana ya afya moja ambayo itasaidia kupunguza gharama kwa kushirikiana.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Shirika la Chakula na Kilimo Duniani Dr.Niwael Mtui amesema wanahabari hao wamefanya kazi iliyotukuka na kwamba wanastahili pongezi kwa sababu wamekuwa wanapigiwa simu kutoka sehemu mbalimbali kutokana na kusoma na kuangalia habari mbalimbali zilizochapishwa kwenye magazeti,redioni,luninga za mitandaoni  na kutangazwa kwenye mitandao  mbalimbali ya kihabari.

“Wanahabari ni miongoni mwa wadau wanaounda timu za dharura za kukabiliana na magonjwa ya mlipuko,wadau wengine ni wataalam wa afya,mifugo,mazingira,maliasili hivyo naomba mafunzo yote ambayo tumepata twende kushare na  wenzetu ambao hawajapata nafasi ya mafunzo’’,alisema.

Dr.Mtui amesisitiza kuendelea kushirikiana na kwamba ndani ya siku tano wadau wameweza kufahamiana jambo ambalo litakuwa rahisi kushirikiana  kwa kupeana taarifa za milipuko ya magonjwa sita ya kipaumbele Ili kuchukua hatua haraka.

Naye Mwakilishi wa washiriki  wa mafunzo hayo ambaye pia ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dr.Jairy Khanga ameipongeza Ofisi na Waziri Mkuu na FAO kwa kutoa mafunzo ya kukabiliana na magonjwa ya mlipuko katika mikoa ya Ruvuma na Mtwara.

“Hii ndiyo mikoa pekee ambayo ilikuwa haijapata mafunzo hayo,mikoa hii ya kusini ambayo inapakana na nchi jirani ipo katika hatari ya kupata magonjwa ambukizi ya mlipuko hivyo mafunzo haya ni muhimu sana’’,a asisitiza Dr.Khanga.

Imeandikwa na maafisa Habari serikalini

Oktoba 20,2020

Mtwara

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • Jela maisha Kwa Ubakaji

    May 27, 2025
  • Msigwa aipongeza Tamisemi kikao maafisa habari

    May 24, 2025
  • SERIKALI ilivyodhamiria kuboresha Barabara na madaraja

    May 23, 2025
  • Mwenge wa Uhuru wapitia miradi 76 mkoa wa Ruvuma

    May 17, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.