• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

OFISA ELIMU MSINGI NYASA,KUWAADHIBU WALIMU WAVIVU.

Posted on: February 18th, 2020

Ofisa Elimu Msingi wa Wilaya ya Nyasa Said Kalima, amewataka walimu wakuu na Maafisa Elimu Kata, kuwasimamia walimu   ili wafundishe kwa bidii ili kupandisha ufaulu Wilayani hapa.

Maagizo haya aliyatoa jana, wakati akiongea na walimu wakuu wote, na Maafisa Elimu Kata  Wilayani  hapa, walipokuwa wakifundishwa kutumia mfumo wa premu, katika Ukumbi wa wa kisasa wa Kassimu Majaliwa, uliopo katika Shule ya Sekondari Mbamba-bay Wilayani nyasa kwa lengo la kuwekeana mikakati ya kuhakikisha ufaulu unapanda kwa 100% (asilimia mia moja).

Bwana Kalima alifafanua kuwa, imefika wakati kila mwalimu atambue wajibu na majukumu yake na kufanya kazi kwa bidii, ili kupandisha ufaulu katika Wilaya ya Nyasa. Walimu wakuu na Maafisa Elimu Kata ni Wasimamizi wakuu wa kila siku wa kuhakikisha walimu wanajituma, na kufanya kazi ya kufundisha wanafunzi kwa bidii, kwa kuwa kila mwalimu akisimamiwa vizuri na akatekeleza majukumu yake,  Ufaulu nyasa utapanda na kufikia100% (asilimia mia moja).

Aliongeza kuwa hatasita kuchukua hatua za haraka kwa mwalimu mkuu yeyote atakayeshindwa kusimamia ufaulu katika Shule yake, kwa kuwa atafanya ukaguzi wa kushtukiza katika shule zote wilayani hapa, ili kubaini mapungufu, na kuchukua hatua mara moja ikiwa ni pamoja na kumshusha madaraka mwalimu, mwalimu mkuu au Ofisa Elimu kata na kumchukulia hatua za kinidhamu ikiwa ni pamoja na hatua zaidi za kiutumishi.

“Nachukukua Fursa hii kuwaagiza ninyi Maafisa Elimu Kata na Walimu wakuu, kuhakikisha kuwa mnawasimamia walimu wenu, na kuhakikisha wanafanya kazi kwa juhudi na maarifa. Kwa kuwa nyie ni viongozi katika maeneo yenu.  Mkihakikisha mnatekeleza majukumu yenu katika shule na Kata zenu Halmashauri hii itakuwa na ufaulu mzuri, na kuhakikisha tunafika asilimia mia moja. Ukiwa na cheo hakikisha unakitumia vizuri, kwa lengo la kuisaidia jamii. Kama hawa wanafunzi wakifaulu kwa 100% (asilimia mia moja) unakuwa umefuta ujinga kwa wananchi wengi na unakuwa umeipa maendeleo jamii. Nitawachukulia hatua mara moja endapo nikipata taarifa ya mwalimu mtoro, mvivu, au asiyewajibika ipasavyo,”. Alisema Kalima

Aidha aliwaagiza viongozi hao kutoa taarifa za haraka na mapema kukiwa na matukio ya walimu watoro,wavivu na wasioshirikiana na viongozi hao au kutokutekeleza maagizo kwa wakati naye atachukua hatua mara moja.

Ofisa Elimu huyo aliwaagiza walimu wakuu na maafisa Elimu kata kuhakikisha wanafanya mazoezi/majaribio ya siku,wiki,mwezi, na mitihani ya Kata ya ujirani mwema na Wilaya kwa madarasa ya Mitihani ili kuwaweka sawa wanafunzi ili waweze kujiandaa vema na mitihani.

Aidha, katika hatua nyingine alimpongeza mh Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania John pombe Magufuli kwa kuhakikisha miundombinu ya Elimu ya Wilaya ya Nyasa inavutia na kuwa rafiki kwa mazingira ya kujifunzia.Hivyo alitoa siku saba kuhakikisha walimu wakuu wote waliopokea fedha za ujenzi wa miundombinu inakamilika.

“Mh Rais ametupendelea sana wana Nyasa,ametupa fedha  za kujengea miundombinu ya Elimu na anatoa Elimu bila malipo, hata ukipita kwenye shule zetu za msingi madarasa yanapendeza na vyoo pia vinapendeza, kwa hiyo kazi iliyobaki ni kumuenzi kwa kuhakikisha ufaulu unakuwa kwa 100% (asilimia mia moja) kwa Wilaya ya Nyasa kwa mwaka 2020 na kuendelea” Alisema Kalima.

Imeandaliwa na

Netho sichali

Kaimu Afisa habari (w) Nyasa 0767417597

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • Jela maisha Kwa Ubakaji

    May 27, 2025
  • Msigwa aipongeza Tamisemi kikao maafisa habari

    May 24, 2025
  • SERIKALI ilivyodhamiria kuboresha Barabara na madaraja

    May 23, 2025
  • Mwenge wa Uhuru wapitia miradi 76 mkoa wa Ruvuma

    May 17, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.