• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

NYASA YAZINDUA KAMPENI YA JIONGEZE TUWAVUSHE

Posted on: July 16th, 2019

Wananchi wa kata ya Mtipwili Wilayani Nyasa, wameunda vikundi shirikishi vya kuwafichua akina mama wajawazito, wasiohudhuria kwenye vituo vya kutolea huduma ya afya na uzazi ili kuzuia vifo vya akina mama wajawazito na watoto.

Hayo yameelezwa na Mganga mkuu wa Wilaya ya Nyasa, Dkt Aron Hyera jana wakati akitoa Taarifa kwa Mkuu wa wilaya ya Nyasa, Bi isabela Chilumba, wakati wa uzinduzi wa kampeni ya “Jiongeze Tuwavushe salama”, uliofanyika jana katika viwanja vya mikutano vilivopo katika kijiji cha chiulu,Kata ya Mtipwili Wilayani hapa. Kampeni yenye lengo la kutokomeza vifo vya akina mama wajawazito na watoto.

Dkt.Hyera alifafanua kuwa, kampeni ya “Jiongeze tuwavushe salama” ina lengo la kutokomeza vifo vya akina mama waja wazito na watoto vinavyotokana na matatizo ya uzazi na wamelazimika kuzindua kampeni hiyo yenye lengo la  kuipa elimu jamii ijue kuwa kila mama mjamzito anapohisi dalili za ujauzito anatakiwa kuwahi kuja katika kituo cha kutolea huduma za Afya zilizo karibu ili, kutokomeza vifo hivyo.

Aliongeza kuwa, wamelazimika kuzindua kampeni hiyo katika kata ya Mtipwili, kwa kuwa ni moja ya Kata zilizoathirika na vifo vya akina mama wajawazito.  kwa kipindi cha miaka mitatu, vimetokea vifo  viwili (2)vya akinamama wajawazito waliopoteza maisha kwa kuchelewa kufika, katika vituo vya kutolea huduma. Kwa kuona hali hiyo wameamua kuwashirikisha wanajamii ili wachukue hatua kwa wazazi/walezi wanaochelewa kwenda katika vituo vya kutolea huduma vilivyopo katika maeneo yetu.

“Katika Kata hii ya Mtipwili tumeunda vikundi vya kuhamasisha wanajamii na kuhakikisha kuwa, kila mama mjamzito anaanza kliniki mapema ili kutokomeza vifo vinavyotokana na uzazi. kuwaelimisha wanajamii wote, kuwa kila mama anayehisi dalili za ujazito anaenda mapema katika kituo cha kutolea huduma za afya ili kutokomeza vifo vya uzazi. Tunataka kupiga vita vifo hivyo kwa kuwa Serikali yetu imetuboreshea huduma za afya katika Wilaya yetu kwa kutujengea Hospitali  Mpya ya Wilaya ya Nyasa, vituo vya afya Mkili na Kihagara ili tuwe na afya nzuri na tufanye kazi kwa juhudi na vikundi kazi hivi vimefanya kazi nzuri na akina mama wote wanahudhuria katika vituo vya kutolea huduma.” alisema Dkt hyera.

Mkuu wa Wilaya ya Nyasa, Bi Isabela Chilumba akihutubia wananchi wa kata ya Mtipwili aliwapongeza kwa kuanzisha vikundi kazi hivyo na kuwataka kuwathamini akinamama wajawazito na kupiga vita vifo vinvyotokana na uzazi katika wilaya hii, kwa kuwafikisha mapema wajawazito wote katika vituo vya afya na kuwachukulia hatua kali wale wote ambao hawatatoa ushirikiano katika jamii.

Aidha alimwagiza Mganga mkuu Dkt Aroin Hyera kuhakikisha kuwa Kata zote za Wilaya ya Nyasa zinakuwa na vikundi kazi hivyo na kuhakikisha vinafanya kazi ya kuhamasisha jamii juu ya akina mama wajawawazito kujiunga na huduma hizo mara wajisikiapo kuwa na dalili za  ujauzito.

“Nakuagiza mganga mkuu wa wilaya ya Nyasa, hakikisha kuwa kila Kata iwe na vikundi shirikishi na viwe vinafanya kazi ya kuwaelimisha,kuhamasisha wanajamii katika wilaya ili kutokomeza vifo vya akina mama wajawazito na watoto na kuwachukulia hatua kwa wale wote wasiohudhuria katika vituo vya kutolea huduma mapema.

Nao wananchi wa Kata ya Mtipwili walipongeza uongozi wa Wilaya kwa kufanyia uzinduzi katika kata ya Mtipwili na kutoa elimu hiyo, na waliahidi kutokomeza vifo hivyo kwa kuhakikisha kila mama Mjamzito anahudhuria katika kituo cha afya mapema.

“Mkuu wa wilaya yetu tunakupongeza sana kwa kazi zako nzuri za kutuletea maendeleo katika Wilaya yetu ya Nyasa na kuchagua Mtipwili kufanyia uzinduzi wa kampeni hii ya Tuwavushe salama,kwetu sisi ni faraja sana na tunakuhakikishi tutatokomeza vifo hivyo katika kata yetu” alisema Diwani wa Kata ya Mtipwili Richard Chialo wakati akifunga shughuli za uzinduzi.

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • RAIS SAMIA AMWAGA MAMILIONI YA EDHA KUIMARISHA SEKTA YA AFYA NYASA DC

    June 28, 2025
  • RAIS SAMIA AMWAGA MAMILIONI YA EDHA KUIMARISHA SEKTA YA AFYA NYASA DC

    June 28, 2025
  • TAARIFA YA MAENDELEO YA JAMII

    June 26, 2025
  • KICHEKO CHATAWALA TAFRIJA YA KUWAAGA MADIWANI

    June 19, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.