• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

Mwenge wa Uhuru waridhishwa na miradi yote Nyasadc

Posted on: May 12th, 2025

MWENGE wa uhuru 2025 umepitia na kuridhishwa na utekelezaji wa miradi tisa yenye thamani ya shilingi bilioni 82 katika wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma.

Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Mheshimiwa Peres Magiri amesema kati ya miradi hiyo,Mwenge wa Uhuru umekagua miradi mitatu,umeweka jiwe la msingi mradi mmoja na kuzindua miradi mitatu na miradi miwili kugawa vyandarua

Akitoa taarifa kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2025,Meneja wa RUWASA Wilaya ya Nyasa Mhandisi Masoud Samila amesema utekelezaji wa mradi huo umefikia asilimia 40 na kwamba wananchi 4,490 watapata maji safi kupitia mradi huo.

Mwenge wa Uhuru pia umezindua mradi wa mtambo za kufua hewa tiba (Oxygen plant)  ambapo kiasi cha shilingi milioni 480 zimetumika kujenga miundombinu ya gesi na ununuzi wa mtambo wa kuchakata hewa tiba.

Mradi huu umekuwa na faida kubwa katika utoaji wa huduma za afya hospitalini ikiwemo kusogeza huduma jirani na kupunguza gharama za kununua huduma.

Mwenge wa uhuru  umekagua shughuli za kikundi cha  wajasiriamali vijana katika kijiji cha Ruhekei Kata ya Kilosa ambapo kikundi hicho kimefanikiwa kupata mkopo wa shilingi milioni 16.5 .

Akitoa taarifa ya kikundi hicho Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Nyasa Khalid Khalif amesema mkopo huo unatokana na fedha za asilimia kumi ya mapato ya ndani ya Halmashauri hiyo.

Mradi mwingine uliozinduliwa na Mwenge wa uhuru ni ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa katika shule ya sekondari Limbo ambapo serikali ilitenga shilingi milioni 72 kutekeleza mradi huo.

Kukamilika kwa mradi huo kumeboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia wanafunzi hivyo kupunguza mlundikano wa wanafunzi darasani.

Mwenge wa Uhuru pia umetembelea na kukagua mradi wa kimkakati wa ujenzi wa bandari  na  barabara ya kuingia bandari ya Mbambabay kwa kiwango cha zege.

Meneja wa Bandari katika ziwa Nyasa Manga Gassaya  amesema serikali imetenga Zaidi ya shilingi bilioni 82 kutekeleza mradi wa bandari ya Mbambabay na kwamba mradi huo unatarajia kukamilika Januari,2026.

Mwenge wa Uhuru ukiwa wilayani Nyasa pia umepitia miradi ya wapinga rushwa katika sekondari ya Kingerekiti na utekelezaji wa shughuli za lishe ambapo wilaya hiyo imetumia Zaidi ya shilingi milioni 33 sawa na asilimia 100 kugharamia afua za lishe kwa watoto 32,574.

Mwenge wa uhuru umekagua mradi wa kugawa  vyandarua vyenye thamani ya shilingi 500,000  ambapo katika wilaya ya Nyasa mwaka 2024 jumla ya watu 14,412 waliugua ugonjwa wa malaria.

Wilaya ya Nyasa inaendelea na mapambano dhini ya malaria kwa kugawa vyandarua kwa watoto chini ya miaka mitano jumla ya wajawazito 7,325 na watoto 9,114 walipatiwa vyandarua mwaka 2024.

Akizungumza baada ya kukagua miradi hiyo ukiwemo mradi mkubwa wa kimkakati  wa ujenzi bandari ya Mbambabay,Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru 2025, Ismail Ali Ussi  Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ametoa mabilioni ya fedha kuhakikisha mradi wa bandari ya kisasa unakamilika.

“Leo hii tumekuja kujionea bandari ya kisasa inayokwenda kutuunganisha na nchi jirani.serikali imefanya uwekezaji mkubwa wa bandari,mradi ambao unatarajia kukamilika mapema mwaka 2026”,alisema.

Katika hatua nyingine Kiongozi huyo wa mwenge wa Uhuru amewakumbusha wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka huu kwenda kupiga kura.

Amesema Mwenge wa uhuru ni chombo kinachomwakilisha Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan na kwamba unapouona mwenge wa Uhuru  utambue kuwa Rais yupo katika eneo hili.

Mwenge wa uhuru upo mkoani Ruvuma kuanzia Mei tisa hadi Mei 17 utakapokabidhiwa mkoani Mtwara.

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • Mwenge wa Uhuru wazindua Mtambo wa Hewa Tiba

    May 12, 2025
  • Mwenge wa Uhuru waridhishwa na miradi yote Nyasadc

    May 12, 2025
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Wilayani Nyasa

    May 11, 2025
  • Mwenyekiti wa Tume huru ya Uchaguzi Tanzania akagua vituo vya kujiandikisha Nyasa.

    May 04, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.