• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

Mwenge wa Uhuru wapitia miradi 76 mkoa wa Ruvuma

Posted on: May 17th, 2025

Mwenge wa Uhuru 2025 mkoani Ruvuma, umepitia na kuridhia jumla ya miradi 76 ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 95.

 Taarifa hiyo imetolewa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma, Bi. Mary Gasper Makondo, aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed, wakati wa hafla ya makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru kati ya Mkoa wa Ruvuma na Mtwara iliyofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Lumesule, wilayani Nanyumbu mkoani Mtwara.

Mwenge wa Uhuru uliingia mkoani Ruvuma Mei 9 na kumaliza mbio zake Mei 16, ukipitia Halmashauri zote nane za mkoa huo kwa umbali wa kilomita 1,378.9.

Katika kipindi hicho, miradi yote 76 iliyotembelewa ilifanyiwa ukaguzi na hatimaye kupitishwa na timu ya wakimbiza mwenge kitaifa, ikiwa ni ishara ya mafanikio makubwa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayogusa maisha ya wananchi moja kwa moja.

Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Katibu Tawala wa Mkoa huo, alikiri rasmi kupokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Bi. Mary Makondo na kuupongeza Mkoa wa Ruvuma kwa maandalizi mazuri na utekelezaji bora wa miradi.

 Akihutubia hadhara hiyo, Bi. Makondo alieleza kuwa wananchi wa Ruvuma wamefaidika mno na mbio za mwenge wa Uhuru ambazo zimewaamsha katika kushiriki kikamilifu kwenye masuala ya maendeleo na kuwaasa kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi mkuu 2025, sambamba na kauli mbiu ya mwaka huu isemayo "Jitokeze Kushiriki Uchaguzi Mkuu 2025 kwa Amani na Utulivu."

Aidha, Bi. Makondo alitumia fursa hiyo kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa mchango wake mkubwa katika kuleta maendeleo mkoani Ruvuma kupitia fedha za utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati.

 Miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa barabara ya Mbinga–Mbamba Bay, upanuzi wa uwanja wa ndege wa Songea, ujenzi wa bandari ya Ndumbi (Nyasa), pamoja na upanuzi unaoendelea wa bandari ya Mbamba Bay.

 Alisema kuwa miundombinu ya elimu, afya, maji na umeme pia imeimarishwa kwa kiasi kikubwa kupitia juhudi za serikali ya awamu ya sita.

Kwa upande wake, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2025, Ndg. Ismail Ali Ussi, alisisitiza kuwa ujumbe wa mwaka huu ni wito mahsusi kwa Watanzania kutunza amani na kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu.

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • Jela maisha Kwa Ubakaji

    May 27, 2025
  • Msigwa aipongeza Tamisemi kikao maafisa habari

    May 24, 2025
  • SERIKALI ilivyodhamiria kuboresha Barabara na madaraja

    May 23, 2025
  • Mwenge wa Uhuru wapitia miradi 76 mkoa wa Ruvuma

    May 17, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.