• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

MRADI WA Tanzania project wajenga shule mpya ya lovund na waikabidhi Serikali

Posted on: March 12th, 2025

TANZANIA PROJECT YAKABIDHI SHULE kwa   HALMASHAURI YA NYASA

Mradi wa Tanzania project umejenga shule mpya ya sekondari Lovund na kuikabidhi serikali, makabidhiano yaliyofanyika katika Viwanja vya shule ya sekondari Lovund tarehe 12.03.2025 na Mgeni Rasmi akiwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed aliyewakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Mhe. Peres Magiri.

Akizungumza katika Hafya ya Makabidhiano Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma amesema anaupongeza mradi wa Tanzania Project kwa kujenga shule hii ambayo imetatua kero, kwa wananchi wa Wilaya ya Nyasa kwa kuwa walikuwa wanatembea umbali mrefu, wa zaidi ya kilometa 7 lakini kwa kwa sasa, kero hii imetatuliwa na wanafunzi wako katika hali nzuri, majengo mazuri yanayohamasisha wanafunzi kujifunza.


Ametoa wito kwa walimu ,walezi na wanafunzi kuyatunza majengo haya ili lengo la kutoa Elimu bora litimie na litatue changamoto  kwa wanafunzi wa sasa na vizazi vijavyo na kumpongeza Mratibu wa Mradi wa Tanzania Project Mwl. Dennis katumbi kwa usimamizi mzuri wa mradi huu,

Awali akitoa Taarifa fupi ya Mradi Mratibu wa Mradi Mwl.Dennis Katumbi amesema Mradi huu unatarajiwa kugharimu jumla ya Shilingi Bilioni 1.2 hadi kukamilika kwake na hadi sasa Mradi umegharimu Shilingi milioni 998na kukamilika kwa asilimia 87 ya miundombinu ya majengo ya shule. Aidha serikali kuu imetoa shilingi 20,000,000.00 kwa ajili ya ukamilishaji wa bweni la wasichana ambalo lipo hatua ya ukamilishaji.

Ameyata majengo yaliyojengwa ni vyumba vya Madarasa 8, Nyumba za Walimu 3 (3 in 1 kila moja), Nyumba ya Mkuu wa Shule 1, Jengo la Utawala, Maabara 3, Matundu ya vyoo 17 kwa Wanafunzi na 2 kwa Watumishi, Maktaba, Bwalo la Chakula, Uzio kuzunguka eneo la shule, tanki la maji Lita 5,000 pamoja na kichomea taka.

Ujenzi huu ulipangwa kufanyika kwa awamu 4 ambapo awamu tatu za awali zimekamilika kwa ujenzi wa miundombinu ifuatayo: Vyumba 8 vya madarasa, nyumba 2 za walimu (Three in One), nyumba ya Mkuu wa shule 1, Jengo la Utawala 1, Maabara 3, Vyoo matundu 17 kwa wanafunzi na matundu 2 kwa watumishi, Bwalo la Chakula likiwa pamoja na jiko la kupikia pamoja na tanki la maji (Lita 5000).

Kwa sasa mradi umeingia katika awamu ya nne (ya mwisho) ya utekelezwaji wake unaohusisha ujenzi wa Maktaba, Nyumba 1 ya walimu, kichomea taka pamoja na uwekaji wa uzio kuzunguka eneo la shule, shughuli ambazo zimeanza kufanyika na unatarajia kukamilika tarehe 31.5.2025.

Mbunge wa Jimbo la Nyasa Mhandisi Stella Manyanya akitoa salamu za serikali ameupongeza mradi wa Tanzania Project na kusisitiza kuwa elimu majengo ya elimu yatasaidia kuikimbiza nyasa kwa maendeleo. Amewataka wazazi walezi kutumia fursa hii kuwapeleka shule wanafunzi.

Mkurugenzi wa Mradi wa Tanzani Project Hanne amesema anawashukuru wafadhili wa mradi huu kutoka Nchini Norway ambao ni Familia ya INO na henca Foundation kwa kutoa fedha ambayo imefanikisha ujenzi wa shule hii.Amewataka wananchi kutumia fursa ya elimu kwa kuwa wao wanaamini elimu ni ufunguo wa maisha na ndio humfanya binadamu, kupambana na mazingira na amesema wanamatumaini shule hii itawapa mafanikio.

Akipokea Hati ya makabidhiano ya shule hii makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa amesema kuwa majengo haya yatatunzwa ili elimu bora itolewe na kuwahamasisha wananchi kuwapeleka shule watoto wao.

Mwakilishi wa Ubalozi wa Nchini Norway amesema wataendeleza ushirikiano kati ya nchi ya Tanzania na Norway na kupongeza shule uzuri na ubora wa shule ambao utatumika kuboresha wanajamii.

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • Jela maisha Kwa Ubakaji

    May 27, 2025
  • Msigwa aipongeza Tamisemi kikao maafisa habari

    May 24, 2025
  • SERIKALI ilivyodhamiria kuboresha Barabara na madaraja

    May 23, 2025
  • Mwenge wa Uhuru wapitia miradi 76 mkoa wa Ruvuma

    May 17, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.