• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

Mradi wa Boost kujenga madarasa 12000 na shule salama 6000

Posted on: December 17th, 2022

WATAALAM zaidi ya 280 kutoka ngazi za Halmashauri na mikoa ya Ruvuma,Njombe na Iringa  wamepata mafunzo elekezi ya timu za utekelezaji wa mradi wa Kuimarisha Ujifunzaji katika Elimu ya Awali na Msingi (BOOST) unaogharimu sh.trilioni 1.15 wenye lengo la kujenga madarasa 12,000 na shule salama 6,000 katika nchi nzima.

Mafunzo hayo ambayo yameandaliwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI yamefanyika kwa siku mbili katika shule ya sekondari Lugalo Manispaa ya Iringa.

Akizungumza wakati anafungua mafunzo hayo,Mratibu wa Mafunzo kutoka Idara ya Usimamizi wa Elimu Ofisi ya Rais TAMISEMI Yusuph Singo  amesema TAMISEMI imeandaa mafunzo hayo katika Kanda tisa kwa lengo la kuwajengea uwezo wajumbe wa timu hizo kuhusu usimamizi wa mradi wa BOOST.

Amezitaja timu hizo kuwa zinaundwa na wajumbe 12 kutoka ngazi ya Halmashauri ambao ni Afisa Elimu Msingi,Afisa Maendeleo ya Jamii,Mhandisi,Mwalimu Mkuu,Afisa Manunuzi,Mthibiti Ubora wa Shule, Afisa Ustawi wa Jamii,Afisa Elimu Kata,Afisa Mipango,Afisa Habari na Mratibu wa Mradi.

Amesema katika ngazi ya Mkoa timu inaundwa na wajumbe wanane ambao ni Afisa Elimu Mkoa,Mratibu wa Mradi wa BOOST,Mhandisi,Afisa Habari,Afisa Maendeleo ya Jamii,Afisa Ustawi wa Jamii,Afisa Mipango na Mdhibiti Ubora wa Shule Kanda.

“Mheshimiwa Rais ametafuta fedha kiasi cha shilingi Trilioni 1.15  kwa ajili ya uboreshaji mkubwa wa elimu kupitia Mradi wa kuimarisha ujifunzaji shule za msingi na awali, utekelezaji wa mradi huu ni wa miaka mitano utaboresha mazingira ya ujifunzaji na ufundishaji, ujuzi na ubora wa walimu katika ufundishaji’’,alisisitiza Singo.Baadhi ya washiriki wa  mafunzo elekezi ya Timu za utekelezaji wa mradi wa BOJustOST kutoka mikoa ya Ruvuma,Iringa na Njombe wakiwa kwenye mafunzo katika shule ya sekondari Lugalo Manispaa ya Iringa

Amesema mradi utatekelezwa katika afua mbalimbali  ikiwemo kuboresha miundombinu ya shule za msingi kwa kuzingatia mahitaji hususan ujenzi wa madarasa, uimarishaji wa mpango wa shule salama, kuimarisha uwiano wa uandikishwaji wa wanafunzi wa elimu ya awali, kuboresha vifaa na njia za ufundishaji elimu ya awali, pamoja na kuimarisha na kuendeleza mpango wa mafunzo ya walimu kazini.

Mratibu huyo wa Mafunzo wa TAMISEMI amesema katika kipindi cha miaka mitano madarasa 12,000 yatajengwa nchi nzima katika shule za msingi kupitia mradi wa BOOST na kwamba kwa kila mwaka yanatarajiwa kujengwa madarasa 3,000 ambapo afua zote zitatekelezwa kwa utaratibu wa lipa kulingana na matokeo(EP4R).

Hata hivyo amesema kupitia mradi wa BOOST shule za msingi 800 zinatarajiwa kuwekewa vifaa vya TEHAMA ili kuwawezesha walimu kujifunza utoaji wa elimu endelevu hivyo kuboresha elimu ya msingi.

 Kwa upande wake Mratibu wa Mpango wa Shule Salama kitaifa Hilda Mgomapayo amesema kupitia mradi wa BOOST  shule salama 6,000 zinatarajiwa kujengwa katika nchi nzima katika kipindi cha miaka mitano ya utekelezaji wa mradi huu ambapo katika awamu ya kwanza zinatarajiwa kujengwa shule 1000.

Amesema shule salama zitawajengea uwezo wanafunzi kujiamini katika mfumo wa elimu,kuimarisha stadi za Maisha,mawasiliano na mahusiano hivyo Watoto kufikia malengo yao.

Kwa upande wake Mwezeshaji kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Lugalata Mwshemi akizungumzia afua ya kuongeza uandikishaji Watoto wa awali,amesema kupitia mradi wa BOOST inatarajiwa kuboresha, uandikisha wa wanafunzi elimu ya awali kwa kuongeza idadi ya wanafunzi katika kipindi cha miaka mitano ya utekelezaji.

Amesema katika utekelezaji wa mwaka wa kwanza uandikishaji wa elimu ya awali 2021/2022 unatarajiwa kuwa ni asilimia 75,mwaka 2022/2023 asilimia 80.14,mwaka 2023/204 asilimia 81.76,mwaka 2024/2025 asilimia 83.38 na mwaka 2025/2026 kuwa asilimia 85.

Hata hivyo amesema lengo ni kuhamasisha jamii kuhusu uandikishaji wanafunzi wa awali wenye umri wa kati ya miaka mitatu hadi mitano na kuhakikisha wanafunzi wote waliondikishwa wanakamilisha mafunzo kwa mwaka mmoja.

Takwimu zinaonesha kuwa hapa nchini kuna shule za msingi zaidi ya 17,000,hata hivyo kupitia mradi wa Kuimarisha Ujifunzaji katika Elimu ya Awali na Msingi (BOOST) watoto zaidi ya milioni 12 wanatarajia kunufaika na mradi huo.

 

Imeandikwa na Netho Sichali wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wilaya ya Nyasa.

Desemba 17,2022

 

Video

Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • Jela maisha Kwa Ubakaji

    May 27, 2025
  • Msigwa aipongeza Tamisemi kikao maafisa habari

    May 24, 2025
  • SERIKALI ilivyodhamiria kuboresha Barabara na madaraja

    May 23, 2025
  • Mwenge wa Uhuru wapitia miradi 76 mkoa wa Ruvuma

    May 17, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.