• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Nyasa District Council
Nyasa District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Nyasa District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Organisation Structrure
  • Services
    • Water services
    • Education services
    • Health services
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • primary education
      • secondary education
      • planning,statistics and monitoring
      • Agriculture,Irrigation and Cooperative
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescure
      • Environmental and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Land and Natural Resource
      • Health
    • Unity/Sections
      • Information and Communication Technology
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Procurement and Supply
    • Full Council
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
      • Tourist attraction-Nyasa dc Video
    • speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Progress project

MKUU WA WILAYA YA NYASA AWATAKA WALIMU WA SEKONDARI KUFAULISHA KIDATO CHA NNE,AIPONGEZA NYASA KWETU FORUM

Posted on: August 24th, 2020

Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Bi Isabela Chilumba  leo amefanya ziara ya kikazi katika Shule ya Sekondari ya Limbo, iliyopo Kata ya Kilosa, na Shule ya Sekondari ya Mbamba bay Iliyopo, Kata ya Mbamba bay wilayani hapa.

Ziara hiyo ina  lengo la kutatua changamoto katika shule zote za Sekondari Wilayani hapa,  ili kuongeza Ufaulu wa wanafunzi wa Kidato Cha Nne na kuwapongeza Walimu wa Sekondari ya Mbamba bay, kwa kufaulisha vizuri wanafunzi wa Kidato cha Sita.

Bi Chilumba amefafanua kuwa anachohitaji ni kuona wanafunzi wa Kidato cha nne wanafaulu kama wale wa kidato cha sita kwa kuwa walimu ni hao hao.  

Akiongea na Walimu wa Limbo Sekondari,  amewataka kufanya kazi kwa kufuata maadili ya kazi , na kuwafundisha wanafunzi kwa Upendo na kuwafuatilia,  Shuleni na Nyumbani, na kuwapa mazoezi ya mara kwa mara, ili waweze kujisomea na kujifunza wawapo shuleni na Nyumbani ili kuongeza ari ya  kujifunza.

Ametoa wito kwa Walimu wa Shule hiyo kufundisha kwa bidii na kuacha visingizio mbalimbali, kwa kuwa wao kama wataalamu wa elimu wamepelekwa mashuleni ili kuwafundisha wanafunzi , wazazi, na wanajamii kutatua changamoto ili kuleta mabadiliko katika maeneo yao ya Kazi.

Aidha amewaagiza wakaguzi wa Elimu Wilayani Nyasa kupeleka nakala ya Taarifa ya ukaguzi na kusema kuwa,  hatawavumilia walimu wazembe,  ambao hawatafaulisha kwa kuwa malengo ya kila mwalimu ni kuhakikisha wanafunzi wake wanafaulu masomo anayofundisha na kamwe hatamvumilia mwalimu mzembe

“Nawaagiza walimu wakuu na wakaguzi wa elimu wilayani hapa kwamba, hamtakiwi kuwavumilia walimu wazembe ambao hawafaulishi, kazi yao ni kutoa visingizio, hatuwezi kufikia hapo tunatakiwa kubadilika, na kuhakikisha wanafunzi wanafaulu kwa kila masomo yenu  mnayofundisha. Lakini pia tunatakiwa kuwa na malengo ya kuhakikisha kuwa wanafunzi wanafaulu kwa hali yoyote ile”.Alisema Chilumba.

Katika shule ya Sekondari ya Mbamba Bay Amewapongeza walimu wa Shule hiyo kwa kufaulisha wanafuzi wote wa Kidato cha sita na kuwataka matokeo kama hayo yapatikane kidato cha nne, na mbinu walizotumia kufundisha Kidato cha sita wazitumie kufaulisha Kidato cha nne.

Aidha amewashuru na kuwapongeza wananchi wa Wilaya ya Nyasa,  kupitia ukurasa wa kijamii wa Facebook wa  Nyasa kwetu Forum kwa kufuatilia habari za Nyasa na kuchangia kwa umakini mada zinazohusu uboreshaji wa Elimu, miundombinu,na masuala mengine ya Kijamii  Kwa Wilaya ya Nyasa.

Awali walimu hao walizitaja changamoto wanazokutana nazo ni pamoja na Kutopata ushirikiano na wazazi,  kwa kuwahamasisha wanafunzi kusoma ,kutochangia chakula na kuwafanya wanafunzi kusoma na njaa, kutembea umbali mrefu na kufika shule wakiwa wamechoka na kutomudu masomo.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa bw. Jimson Mhagama aliwataka walimu kuhakikisha wanafundisha na kuhakikisha wanafunzi wanafaulu ili kufikia malengo ya Wilaya ya kufaulisha wanafunzi wote wa Kidato cha Nne, kwa kutoa Elimu kwa wazazi na walezi kwa kuwa wazazi wengine hawana ufahamu juu ya kutoa ushirikiano kwa walimu ili kuinua kiwango cha Elimu Wilayani Nyasa.

Mkuu wa Wilaya ya Nyasa katika ziara hiyo aliambatana na Kamati ya Ulizi na Usalama Wilaya ya Nyasa.Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Nyasa na Wakuu wa Idara za Elimu Sekondari,Elimu Msingi, Tume ya Utumishi wa Walimu, na Mkuu wa Idara ya Utawala na Raslimali Watu Bw.Liston Moyo.

Matokeo ya Kidato cha sita katika Wilaya ya nyasa 2020 wamefaulu kwa asilimia 100% kwa shule zote Mbambabay Sec. Na St. Pauls' Sec.=>Mbambabay: Div I->53, II->88, III->13, ->: 0, O->0.=>ST. PAULS: I->13, II->45, III->19, IV->0, O->0. Shule zote ufaulu wa 100%



Announcements

  • Fursa ya kuwekeza kilimo cha Korosho shamba Wilaya ya Nyasa October 24, 2024
  • TANGAZO la kuitwa kwenye Usaili wa waandishi Wasaidizi na waendeshaji Vifaa vya Bayometriki (BVR) December 18, 2024
  • TANGAZO LA KUHAKIKI UMILIKI WA ARDHI NYASA August 30, 2021
  • MAREKEBISHO YA TAREHE YA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 17, 2022
  • View All

Latest News

  • Jela maisha Kwa Ubakaji

    May 27, 2025
  • Msigwa aipongeza Tamisemi kikao maafisa habari

    May 24, 2025
  • SERIKALI ilivyodhamiria kuboresha Barabara na madaraja

    May 23, 2025
  • Mwenge wa Uhuru wapitia miradi 76 mkoa wa Ruvuma

    May 17, 2025
  • View All

Video

TUNAMPONGEZA Rais Samia kwa kutuletea maendeleo Nyasa na kumteua Dkt Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza
More Videos

Quick Links

  • Ruvuma Regional Website
  • Songea Municipal Website
  • Songea District Website
  • Mbinga Town Website
  • Mbinga District Website
  • Madaba District Website
  • Tunduru District Website
  • EGA WEBSITE
  • Namtumbo District Website

Related Links

  • National website
  • TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistic

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Nyasa District Council

    Postal Address: Box 90 Mbamba bay

    Telephone: 025 -2952003

    Mobile:

    Email: ps.ded@nyasadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Nyasa District Council. All rights reserved.